Kila issue na wakati wake..
Mahakama itabaki kuwa issue na kuvua mwanamke hijabu itabaki kuwa issue
Besides kwani nini msimamo wa chadema kuhusu mahakama ya kadhi?
hauna tofauti na matakwa ya maaskofu...so ccm na cdm kwa issue ya waislamu wako pamoja mkuu hawana tofauti yoyote...
jitambue.
Mkuu wangu unanifanya naanza kuamini maneno ya wakristu kuhusu elimu za waislaam na yawezekana kweli imechangia sana kuwa wajinga pamoja na kwamba Mtume alisistiza elimu...
Mkuu wangu, hijab ni vazi la kike na limesisitizwa kwa malengo na makusudi kama vile mzungu anavyosisitiza kuvaa tai kwa mwanamme. Ina maana yake na sababu zake mwanamke kuvaa hijab, na akivaa haimfanyi kuwa muislaam isipokuwa tunafuata mafundisho kama vile wewe unapovaa suruali ama nguo inayovuka magoti ni maagizo ya mitume vile vile ktk mavazi.
Na kisha ebu waulize hao masheikh je mwanamke aliyevaa mtandio wa Khanga kufunika kichwa chake ni Hijab? watakwambia hiyo sio Hijab isipokuwa Hijab ni mtandio ule ulotoka Dubai au Oman na ndivyo mnavyoitafsiri Kanzu kuwa vazi la waislaam. Kesho mtu akivamia na kuchaniwa kanzu basi ni kuudhalilisha Uislaam..
Hawa waarabu wamewaharibu sana kiasi kwamba hata majina mnaamini kabisa ni majina ya kiislaam mtu akiitwa Omar au Hamza lakini sii yule anayeitwa Richard, wakati huo huo huwezi kunambia swahaba yeyote wa mtume aliyebadilisha jina lake baada ya kuuukubali Uislaam kwani majina hayo waarabu wa imani zote huyatumia. Baba yake mtume aliiitwa Abdallah na hakuwa Muislaam lakini ukienda Bongo ukisema jina lako Abdallah basi lazima utakuwa Muislaam.. Tembeeni mkaizunguke dunia myajue mengi jamani, waarabu wanayatumia majina haya bila kujali dini zao. Jamani eeeeh Uislaam ni Imani na ibada, majina, hijab na kanzu sio Uislaam ...Abu Talib mtamweka wapi nyie!
Nitarudia kusema kwamba Hijab ni vazi la kike na limesisitizwa na mitume kwa wanawake wote (ustaarabu) na sii Uislaam, bali jinsi ya mwanamke to carry herself and be respected kama ilivyo hulka ya kidunia tunapomwona mwanamme amevaa shati na tai, tai inaongeza heshima fulani hata kama hakuna sababu ya maana kwa mtu asiyevaa tai, lakini ukweli utabakia kwamba mvaa tai atatazamwa na kupokelewa na heshima fulani ndivyo inavyokuwa kwa mwanamke na Hijab..Hii ni ktk moja ya mapungufu ya kibinaadam hatujakamilika.
Ama kweli mtume alisikitika sana na kusema hakika Umma wake ni wachache sana wataingia peponi!...na hakika dalilizote zinajionyesha, hapo hapo mimi naongezea kusema Uislaam ni dini isiyokuwa na watu, hali Wakristu ni watu wasiokuwa na dini...
- Ukweli unauma, mtanisamehe nyote.