KAMALELA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2011
- 226
- 113
Hivi hijabu ni vazi la DC vazi la Waislamu? Kuna uhusiano gani wa hijabu kama vazi la DC? Huyo DC kama ni mwislamu alikutwa kwenye shughuli za ibada? Ninapenda kujua yule kiongozi wa CCM aliyezini na mke wa mtu huko Igunga alikuwa wa dini gani na mwanamke alikuwa wa dini gani? Isije ikawa walikuwa Waislamu wote na bila shaka kulikuwa na kuvuana hijabu lakini Waislamu hawakutoa tamko. Kipi kibaya zaidi kati ya DC ambaye ni Mwislamu akavuliwa hijabu (kwa bahati mbaya) katika purukushani za DC kukamatwa akifanya mambo yaliyo kinyume na sheria na lile suala la kiongozi aliyefanya zinaa ( hata kuvuliwa hijabu).
Bakwata muwe macho na CCM. CCM watawatumia kama Kondomu lakini wakishamaliza kuwatumia watawatupa kwenye shimo la takataka. Kumbukeni wakati walipotaka kura za Waislamu waliweka kwenye ilani yao ya uchaguzi wa mwaka 2005 luanzishaji wa mahakama ya kadhi lakini leo hawataki kuwaeleza kwamba walikuwa na maana gani kuweka lile suala la Mahakama ya Kadhi kwenye ilani wakati hawakuwa na nia ya kutekeleza?
Mkuu Hakika we ni Great Thinker! nimeyapenda mawazo yako.