Bakwata, Basuta Walaani DC Kuvuliwa Hijabu

Status
Not open for further replies.

propagandist

Member
Aug 12, 2011
93
9
Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa CHADEMA kuwaomba radhi waislamu.

Naibu mufti akiwa mjini Tabora alisema Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna.

CHANZO: Taarifa ya habari Radio Imaan
 

janja pwani

Senior Member
Jul 27, 2011
104
8
Baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA limewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislam kwani kitendo walichokifanya wabunge wake ni udhalilishaji dhidi ya uislam kufuatia wabunge wake kumvua hijabu DC Fatuma kimario kwani udhalilishaji waliomfanyia ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani alisema Naibu mufti.
 

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,433
7,552
Bakwata hivi hawana mambo ya kufanya mwishowe watakuja sema sambusa zipigwe marufuku (kwa kukosa la kusema)kama kudhalilishwa sio uislamu uliodhalilishwa na hiyo hijabu ni sawa na kilemba tu,acheni kulilia yu enyi Bakwata
 

The Magnificent

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
2,694
1,244
hatuombi radhi ng'o! Kwanza nyie mna mchango gani kwenye chama chetu? Make nyie ni taasisi iliyoundwa na ccm kama ilivyo kwa uvccm,uwt nk.
Tukiwaomba radhi ni kama kuiomba radhi ccm,kitu ambacho ni mwiko kwetu!
Viva CDM!
 

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
23,328
44,354
Hivi uisilam ni jina na mavazi au ni vitendo?majina mangapi ya kiislam yamehuska kwenye uhalifu tanzania na bakwata hawajaomba radhi kuonyesha kwamba hawaungi mkono?bakwata mnatumiwa kisiasa.

Mtu anapokiuka mashariti anashugulikiwa kwa mjibu wa taratibu tulizojiwekea hususani sheria mpya za uchaguziisemayo (mtu yeyote anayevuruga taratibu za uchaguzi akamatwe) bila kujari dini wala kabila lake. Mhalifu ni muhalifu tu na ukitaka kuheshimiwa jiheshimu.mia
 

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,881
1,124
wapeleke ujinga huko,wale machangudoa wanaouza mbunye kule zanzibar halafu wanafutia hijab mbona hawajaenda kuwafuata?wadili na mambo ya msingi na wawaeleze waislam ni kwa nini ccm haiwapi waislam ilichowaahidi?
bakwata ni taasisi ya ccm kama ilivyo uvccm uwt nk hawana maana hawa wamerudisha maendeleo ya waislamu nyuma miaka hamsini na wanachojua ni uchonganishi tu.
hivi ni lini wasomi wa kiislamu wataingia kwenye hizi taasisi kila taasisi inaongozwa na vilaza mara utasikia tunadhulumiwa mara nini.

watu kama january makamba,pro ibrahim lipumba,dk husein mwinyi,dk kigwangala ndio wanaotakiwa kushika taasisi za kiislamu sio hawa wanaoshindana kwa kumiliki majini dunia sasa hivi ni sayansi na teknolojia.
 

bemg

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
2,799
641
BWAKATA wafanye kazi yao na si kuingilia mambo ya siasa kwani Hijabu nini kwao.Mbona watu wanachaniwa kanzu huko kwa Libya,yemen na hawasemei?
 

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
1,298
ahaaa kumbe bakwata hawana mchango katika chama chenu cha cdm kumbe wenye mchango ni RC?

hivi unaweza kufananisha Roman Catholic na Baraza la Waislam Tanzania, hakuna comparison ya aina yoyote hapa . kinachojiri ni kuonyesha jinsi ulivyo kilaza
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA limewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislam kwani kitendo walichokifanya wabunge wake ni udhalilishaji dhidi ya uislam kufuatia wabunge wake kumvua hijabu DC Fatuma kimario kwani udhalilishaji waliomfanyia ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani alisema Naibu mufti.

Mungu ni 'haki' mungu ni 'usawa' na mungu ni 'kweli tupu'. Hivyo nilitegemea BAKWATA kama chombo kinachosimamia maadili ya 'mungu' kupitia dini ya kiislama wangemtaka DC Mama Fatma Kimario kusema 'kweli yote' kuhusu mkutano aliokuwa anafanya mahali/muda kinyume na sheria za vyama vya siasa.

Pia BAKWATA wangefanya vema kujiridhisha kuwa huyo DC hakuna anafanya jambo lolote ambalo directly or indirectly lingenyakua haki ya raia yoyote ya kupata kiongozi wanayemtaka katika uchaguzi mdogo wa Igunga. Hayo ndiyo nilitarajia toka kwa BAKWATA kama kweli wanasimamia maadili mema. Mavazi ni jambo la mbali sana ukilinganisha na HAKI ya mtu kupata kiongozi bora.

Pia ni vizuri BAKWATA watathmini tena upya kwamba wanasimamia nini hasa? Kujiingiza kwenye siasa uchwara ni kukivunjia heshma hiki chombo cha waislam. Kwa wameshamhoji huyu DC na kujua alifuata nini pale?

Na kulikuwa na ulazima gani kwa yeye (DC) kufanya mkutano hapo wakati kuna mkutano wa chama kingine? Huu ni ustarabu? AAu hii inakubalika kwa BAKWATA kwamba mtu anaweza kuvuruga shughuli halali yenye manufaa kwa wengi kwa sababu binafsi?
 

Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
hatuombi radhi ng'o! Kwanza nyie mna mchango gani kwenye chama chetu? Make nyie ni taasisi iliyoundwa na ccm kama ilivyo kwa uvccm,uwt nk.
Tukiwaomba radhi ni kama kuiomba radhi ccm,kitu ambacho ni mwiko kwetu!
Viva CDM!

Limbukeni yuko kazini.
 

Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,522
643
Kama bBkwata wametoa tamko hilo itabidi sasa tuchunguze na kujua majukumu na manufaa ya baraza hili, maana sasa kazi yao itakuwa ni kudandia hoja bila kupima, na vilevile weledi wa viongozi wao unatia shaka, wanashindwa kusimamia majukumu yao ya msingi matokeo yake wamegeuka kuwa vibaraka wa ccm na ndo maana answaar sunna wameamua kujitoa bakwata na kuanzisha baraza lao tofauti!

Kwanza kwa akili ya kawaida haiwezekani kwa chadema kuomba msamaha kwa jambo ambalo shauri lake lipo mahakamani, kufanya hivyo inaweza ikawa ni dalili tosha ya kukiri kosa na hivyo kuweza kuathiri mwenendo wa kesi! Hata hivyo bakwata lazima waelewe kuwa yule mama dc kama kweli alivuliwa hicho kilemba (ambacho wameamua kukiita hijab) wajue hakuvuliwa kwa sababu ya uislam wake la hasha!

Pia inawezekana kuwa baada ya huyo D.C kubambwa akipanga kufanya hujuma za kisiasa akiwa na kundi lake labda alitumia kilemba kile kuficha uso wake ili asijulikane kama ni yeye D.C na hivyo waliomkamata wakalazimika kumtoa kilemba ili waone sura yake!na pia inatia shaka ilikuwaje dc aende kwenye shughuli zake za kazi za ki-dc bila kuwa na ulinzi wowote!? je huyu mama dc hakuwa kwenye shughuli za ukada wa chama chake cha ccm!? Shaka bin wasiwasi...!
 

The Priest

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,030
256
Hawa ndio wanasambaza chembechembe za udini,hv hili suala mbona kila cku linakuzwa jamani,yule mama si alivaa ushungi tu..aagh!kwann bakwata wanataka ku2mika kisiasa!hapa 2shaelewa nn wanakifanya..ila wanaigunga (christian+muslim) hawawezi kusikiliza hz propaganda.
 

Mwamikili

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
417
136
Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislamu alisema Naibu mufti akiwa mjini Tabora, Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna. taarifa ya habari Radio Imani.


stupid source!
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Top Bottom