Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Bajeti yapendekeza Elimu ya kidato cha tano na sita kutolewa bure. Wanafunzi 90000 wa kidato cha tano na wanafunzi 50000 wa kidato cha sita. Ili kupunguza adha wanazokumbana nazo ada za watu hao imefutwa.

Hivyo elimu bila ada itakuwa kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita. Pia inaangaliwa namna ya kusaidia vyuo vya kati (colleges) kama uwezo wa fedha utaruhusu.

----
Mheshimiwa Spika, kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takriban 90,825 na kidato cha sita ni 56,880. Mahitaji ya fedha ni shilingi 10,339,350,000. Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Mheshimiwa Rais alivyoielekeza

Wizara, inapendekeza kufuta ADA kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Kwa hatua hiyo, Elimu bila Ada ni kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha sita.

Serikali itajipanga kuangalia namna ya kusaidia vyuo vya kati kadiri hali ya uchumi itakavyotengemaa.

Nani kama SAMIA? Nani kama Mama? Nani kama CCM? CCM ni Na. 1.
 
Mama yenu huyu anawalambisha asali huku rasilimali zetu anaziuza 😂
Ndio anaziuza ili wananchi wafaidike na hayo mauzo co rasilimali unaziangalia tu huku wananchi waña shida ya elimu, maji, usafirishaji, njaa najuwa umezoweya kumuona magufuli akizurura na mabegi ya mamilioni ya shilingi akigawa mabarabarani na kugeuza wananchi omba omba wakati rasilimali wakiziangalia lakini mama hayuko hivyo.
 
Jiheshimu we dada,mbona hapo nimetoka maoni yangu au wewe ndo waziri wa elimu? Utafirimbwa bure
Shida ya hii nchi hao machawa. Pengine hata waziri mwenyewe wa elimu wala asingekasirika na maoni yako na hata angeweza kufurahia. Ila chawa sasa
 
Viongozi wa nchi hii sijui kwa nini akili zao huwaga nusu hazifikagi zikawa nzima zikawaza kwa mapana na marefu. Mlituambia kwamba watoto wengi huacha shule kwa kukosa ada tukasema ewaaah! Kwa kuwa ada ya o level ilikuwa ni 20000 kwa mwaka ni kweli Kuna wazazi hawana uwezo wa kulipa pesa hiyo. Lakini cha ajabu ni kwamba kama mzazi hana uwezo wa kulipa 20000 tu kwa mwaka na Advance saizi mmesema mnafuta ambapo ada ni 70000 pamoja na Karo, je nimiujiza gani huyu mzazi akapata uwezo wa kulipa ada ya million moja mpaka mbili ya chuo kikuu ili mwanae asome.

Shida inakuja hapo mnapenda kupigiwa makofi hamjui kuwa mnaruka mikojo na kukanyaga Mavi, yani mtoto anakuja chuo kikuu hapati mkopo mwingine mnampa 50%halafu hiyo laki 7 au 8 yakujazia anaitoa wapi ilihali mlibwatuka kuwa Kuna wazazi hawana uwezo wa kulipa elfu ishirini kwa mwaka. Halafu oooh anaupiga mwingi, labda upupu!

1655219572820.jpg
 
Mimi naamini hakuna elimi ya bure; haya mambo ya siasa ni kuwafubaza akili wananchi.

Wote wanapiga makofi Bungeni hapo hakuna mtu anasomesha haya mashule yenu ya bure bure, watoto wao wanaandaliwa kwa elimu bora kabisa.

Mimi nakubali kulipa 5m kwa mwaka walau sababu najua hakuna elimu ya bure Africa.

Siasa ni kitu kibqya mno hasa hizi siasa za watu walewale, mawazo yaleyale kuwapangia mambo yaleyale miaka nenda rudi.

Haya somesha mwanao kayumba hadi form Six afu utapata majibu yake, tena tunaomba usife mapema ili ushuhudie mwanao akihaha kutafuta kibarua..akiishia kuwa bodaboda, dereva ama mlinzi.
 
Breaking: Rais Samia Afuta Ada kidato Cha ,5 &6

Mama anajichukulia points tu
Watoto wanapata mimba sababu hakuna mabweni; walimu wanahaha kila kukicha mikopo mishaharaduni; makazi ya walimu duni kabisa
Vyumba vya madarasa majanga, miundo binu ya vyoo na maji hakuna
Vitabu ...

Afu unafuta ada... Msichezee elimu nyie watu

Ningekuelewa kama unafuta ada huku hayo hapo juu yote yamekuwa addressed.
 
Back
Top Bottom