Bajeti ya Serikali 2021/2022 ni Trilioni 36.33, Bodaboda na Madiwani Waneemeka, Barabara hadi Vijijini, Miradi kuendelea, Watanzania Kufunga Mkanda

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,522
2,000
Mama aliletwa SMT na Mzee Kikwete na huo ukweli aliusema siku analihutubia bunge.

Hawezi kuwa na ujasiri wa kumpinga JK na ukizingatia ni mama ndio ushawishi wa awamu ya nne unavyozidi kujikita.

Mwigulu pia ni nguvu ya JK kufika alipofika hivyo hawezi kupindua kwa ushawishi wake.

Mwigulu anafaa uwaziri na hafai kabisa kuwa rais.
Mwigulu hafai kuwa kiongozi wa watu labda msafara wa panya.
 

M2mishi

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
697
250
Hii tengua tengua ni moja ya jambo ulilosema jana kuwa lilifanywa na late Magufuli kwa pupa kwa maana alitoa kadi hata bila kuona kosa bali kwa kuambiwa. Hukuishia hapo ukamunanga Mh Rais SAMIA kuwa amefundishwa siasa na JK huku ukisahau kuwa AWAMU YA 5 ndiyo iliyomtambulisha mama Kwenye OPEN EYE politics na kumheshimisha zaidi. Kwa ufupi ulichokifanya jana ni uchonganishi na dharau kubwa kwa viongozi wakuu wa nchi. Namalizia kwa kusema JIANDAE your political carrier will be fated to end badly. Mwigulu Nchemba.
Mwigulu Nchemba hajafanya kosa lolote kusema kile alicho ki experience na alicho kishudia. Tatizo lenu kubwa kawakera pale alipo msifia Kikwete na kuacha kumsifia mwendazake? Muacheni Mwigulu afanye kazi bwana
MAMA SAMIA TUNAMUELEWA SANA KAZI IENDELEE
 

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,004
2,000
Kwa miaka ya hivi karibuni huwa sifuatilii Bajeti za Serikali kwa sababu siyo bajeti halisia na ni danganya toto.

Kinachotakiwa kwenye bajeti:
(1) Mapato yote yaliyopatikana kwa mwaka unaoisha ni kiasi gani
(2) Pengo ni kiasi gani
(3) Kila sekta iliyopangiwa fedha zake mfano:- Wizara ya Afya, Viwanda na Biashara, Halmashauri ya Liwale, OC kwa kila Halmashauri nk zilienda ngapi na kama kuna pengo basi sababu zitolewe.

Bajeti ya Serikali ni budi iwe na mpangilio ili hata Mwananchi wa kawaida aweze kuielewa.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
38,048
2,000
Haya ni maneno ya waziri wa fedha Mwigulu Nchemba katika hotuba yake ya bajeti jana.
5bmE.jpg
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,673
2,000
Mapendekezo ya Bajeti iliyotangazwa jana yanaakisi hali halisi ya uchumi wa nchi hii, kama ifuatavyo:
● yanalenga nchi kujitegemea kwa kila mmoja wetu kuchangia kulingana na uwezo wake;
● yatakuwa na faida kubwa katika kurejesha wawekezaji kwa kuwa yanapendekeza hatua kadhaa zinazolenga kuboresha mazingira ya biashara na kupunguza urasimu
katika kutoa misamaha;
● yanalenga kudumisha utulivu katika mfumo wa kodi, kiungo katika kuvutia wawekezaji wa nje (FDIs).
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,673
2,000
...
Kinachotakiwa kwenye bajeti:
(1) Mapato yote yaliyopatikana kwa mwaka unaoisha ni kiasi gani
(2) Pengo ni kiasi gani
(3) Kila sekta iliyopangiwa fedha zake mfano:- Wizara ya Afya, Viwanda na Biashara, Halmashauri ya Liwale, OC kwa kila Halmashauri nk zilienda ngapi na kama kuna pengo basi sababu zitolewe.

Bajeti ya Serikali ni budi iwe na mpangilio ili hata Mwananchi wa kawaida aweze kuielewa.

Ungefuatilia hotuba za Mawaziri kuhusu bajeti zao na majadiliano yaliyofuata, naamini usingekuja na hoja hiyo.
 

SHIGOTTO

Senior Member
Sep 4, 2018
107
250
Ndugu wana JF naomba kujuzwa katika bajet ya mwaka huuu serikali imetenga wapi kiasi kikubwa cha fedha? Hi itasidia kujuwa kipao mbele cha serikali kwa mwaka huu+

Naomba kuwakilisha
 

Mtoto wa Nyerere

Senior Member
May 21, 2021
129
1,000
Unapandisha kodi ya mpesa

Unapunguza kodi ya bia

Unapunguza kodi ya private plate number

Unakuwa una akili kweli?

Hii budget ni ya matajiri Mwigulu sioni kama ana uwezo wa kufikiri vizuri juu ya uchumi naomba ujiuzulu.
IMG_20210629_163423.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom