Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 47.424 katika mwaka 2024/2025.
Dkt. Nchemba amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25.
Amesema kuwa makusanyo hayo yatatokana na vyanzo mbalimbali yakiwemo mapato ya ndani, michango kutoka kwa washirika wa maendeleo na mikopo.
"Mapato ya ndani yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 34.436 sawa na asilimia 72.6 ya bajeti yote, washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 4.291 sawa na asilimia 9.0 ya bajeti, serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 6.141 kutoka soko la ndani na shilingi trilioni 2.555 kutoka soko la nje," amesema Waziri Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba amesema kuwa maoteo ya bajeti ya serikali ya mwaka 2024/25 yamezingatia mwenendo wa ukusanyaji mapato, matarajio ya ukuaji wa uchumi, hali ya uchumi wa dunia pamoja na mikakati ambayo Serikali inaendelea kuchukua katika kuongeza mapato ya ndani.