baiser
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 1,456
- 2,181
Ndugu wana JF, mwezi wa.12 /2020 nilifiwa na mamangu mzazi.
Leo saa Tisa na dakika kumi usiku (12/5/2021) nimeota ndoto niko na mdogo wangu nashusha mteremko kwa miguu nikitokea mjini Iringa kuja Ipogolo maeneo ya kitanzini tumekutana na mama akiwa kabeba kikapu chake anapandisha mjini yaani anatoka Ipogolo anapandisha iringa mjini kwa wenyeji wa Iinga watanielewa.
Tumeongea naye na tukamwomba MTU tupige nae picha ghafla akaanza kubadilika na kuwa wa blue kupoteza nuru ya sura yake halisi na kuwa kijana, lengo tusipate picha yake halisi.
Baada ya muda akabadilika na kuwa kijana wa kiume miaka kama 15 hivi na tukaanza kushusha nae kuja Ipogolo huku nikimuuliza maswali kuwa anaishije aliko.
Akajibu maisha mazuri aliko, hela kama zote ila tu hawaruhusiwi kuja kununua vitu wenyewe kuchanganyika na binadamu halisi.
Baadaye nilimpa mkate akapokea na kuniomba kopo la maji akatumie kuchota kwenye MTO Ruaha ili anywe, na ghafla nikastuka na ndoto ikaishia hapo.
Je, hii manaake nini? Is she a walking dead?