Nimeona video inatrend ya ugomvi mkubwa wa nyumba ya urithi Kariakoo mtaa wa Manyema.
Nyumba hiyo ya ghorofa 5 ilijengwa na mzee anaeitwa Mohammed Alidina ambae alifariki miaka kazaa iliyopita.
Mzee huyo wakati akiwa hai alitoa sehemu ya nyumba hiyo. Floor ya juu itumike kama madrassa na kufanya taratibu za kukabidhi kwa msikiti ambazo waislamu wanaziita waqfu. Ghorofa zilizobaki aliendelea kuzitumia kuishi na zingine kupangisha appartments na fremu kwa wafanyabiashara Kariakoo.
Baada ya huyo mzee kufariki aliacha watoto 11, ambao watoto wao waligawana hizo appartments na fremu na kuendelea na maisha.
Mbeleni watoto wachache wa kiume wa marehemu mzee huyo wakapendekeza wazo la kutaka nyumba hiyo iuzwe kila mtu akajenge kwake. watoto wengine wakapinga kwamba hawataki nyumba iuzwe maana baba yao enzi za uhai alisema nyumba isiuzwe na akatoa sehemu ya nyumba iwe madrassa inayomilikiwa na waislamu wote. sasa watauzaje nyumba yenye wakfu ambayo ni mali ya waislamu wote.
Watoto wenye wazo la kuuza wakaona hapa kuuza ngumu. wakaamua kwenda kumshirikisha imamu wa msikiti ambao ulipewa wakfu sehemu ya nyumba hiyo. maana msikiti ulikuwa na documents za wakfu walizopewa na marehemu baba yao.
Kimya kimya wakashirikiana na imamu wa msikiti uliopewa hizo documents. wakatafuta mteja Mkinga mmoja wakamuuzia nyumba bila watoto wengine kujua.
Mbeleni mkinga huyo ambae ni mnunuzi aliyonunua hiyo nyumba akaenda kuchukua mali yake. Ndipo watoto wengine wakagundua nyumba imeuzwa. Ndipo ugomvi mkubwa ukaibuka na mapanga juu.