Waziri Silaa atinga Kariakoo, asema jengo lililouzwa lina Waqfu uliosajiliwa wizarani. Amshauri mnunuzi akamalizane na aliyempa hela

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
WAZIRI JERRY SILAA ATOA SOMO, KAZI YA MSIMAMIZI WA MIRATHI NI IPI, WANUNUZI WA MALI ZA MAREHEMU WAWE MAKINI NA WASIMAMIZI WA MIRATHI KWANI KAZI YAO SIYO KUUZA MALI ZA MAREHEMU BALI KUGAWA MALI KWA KUFUATANA NA USIA, SHERIA ZA DINI AU MILA

View: https://m.youtube.com/watch?v=3i97zL9ftTg

11 March 2024
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ameingilia kati mgogoro wa eneo la jengo la ghorofa lilipo Kariakoo jijini Dar es salaam ambalo sehemu ya jengo hilo lilitolewa Waqfu na marehemu Sheikh Mohamed Aldini ambaye aliacha usia.

Waziri Silaa alifika eneo hilo ambalo limekuwa na ugomvi mkubwa wa ndugu ambao ni watoto wa marehemu Ardini waliogawanyika katika pande mbili zinazokinzana kuhusu usia wa kuwekwa Waqfu eneo la Madrasa katika jengo hilo.

Aidha, baada ya kusikilizwa kwa pande mbili za ndugu ambao ni watoto wa marehem Mzee Ardini Waziri Silaa aliamuru kurejeshwa kwa Madrasa ambayo ilikuwa ndio usia wa marehemu.

Awali, ndugu wawili wanao pingana na wenzao waliamua kuhamishwa kwa madrasa hiyo nje ya eneo hilo la Kariakoo na kumuuzia mtu mwingine sehemu ya jengo hilo.

Source: Global TV Online

Pia, soma=>
Imamu wa msikiti adaiwa kushiriki kuuza nyumba ya familia Kariakoo iliyokuwa na waqfu. Mapanga yatembea nje nje
============

Vitu vya muhimu
  • Nyumba inayogombaniwa ina wosia na waqfu uliosajiliwa na marehemu wizara ya ardhi mwaka 2007 wakati wa uhai wake(madrasa iliyopo ghorofa ya pili).
  • Ndugu wanaodaiwa kuuza, wamesema wamenunua na wameanza ujenzi wa waqfu(madrasa) eneo jingine Temeke.Waziri Slaa amesema wosia haukusema kama waqfu unaweza kuhamishwa.
  • Eneo ilipokuwepo madrasa, mnunuzi amesema wamepangisha mtu.
  • Anayedaiwa mnunuzi hajaondoa mpangaji ila amewataka kulipa kodi kwake ili waendelee na biashara. Amedai ana hati lakini haijabadilishwa jina.
  • Waziri Silaa amewataka watanzania wafahamu msimamizi wa mirithi sio mmiliki wa nyumba, afanye jitihada za kuwapata warithi wote.
  • Waziri Silaa amemwambia mnunuzi Michael Makanika Nyamika hatafanikiwa kupata hati ya jina lake kwasababu amenunua mali ambayo marehemu mwenye mali yake ameacha wosia ikiwemo waqfu wa madrasa.
  • Wizara itasaidia kugawa maduka/jengo kulingana na wosia ambao marehemu aliusajili wizarani na warithi watapewa unit title.
  • Waziri Slaa amemuagiza OCD kurejesha madrasa iliyoondolewa kwasababu marehemu kwenye wosia alisema ghorofa ya pili iwe madrasa maisha yote.
  • Waziri Silaa kamwambia mnunuzi amfungulie kesi aliyemuuzia kwani hakuna msimamizi wa mirathi anayemalizana na warithi, alitakiwa amletee warithi amalizane nao mwenyewe.
  • Waziri Slaa amewataka watanzania kuandika wosia, amesema marehemu Sheikh Aldina amefundisha jambo kubwa la kuusajili kwani kumuachia mtu, watu wanaweza kuuruka baada ya msiba.
 
msimamizi wa mirathi muda wake wa usimamizi huwa unaisha lini ?
Anapofile inya jinsi alivyokusanya na kugawa mali za marehemu. LAZIMA KUFILE ACCOUNT AND INVENTORY

Furthermore, we have discovered from the High Court record, that as consistently claimed by the
appellant, he did exhibit the requisite inventory and account. In law the probate proceedings were effectively closed from that day.
 
Hongera Kwa Waziri kutatua mgogoro huo.

Kununua Mali ya urithi huwa na changamoto nyingi hasa kama ndugu wengine wanakuwa hawajaridhia.

Nimewahi kupata shida ya hivyo, bila kutumia connection nilikuwa napoteza hela yangu hivi hivi 🙌
 
WAZIRI JERRY SILAA ATOA SOMO KAZI YA MSIMAMIZI WA MIRATHI NI IPI, WANUNUZI WA MALI ZA MAREHEMU WAWE MAKINI NA WASIMAMIZI WA MIRATHI KWANI KAZI YAO SIYO KUUZA MALI ZA MAREHEMU BALI KUGAWA MALI KWA KUFUATANA NA USIA, SHERIA ZA DINI AU MILA

View: https://m.youtube.com/watch?v=3i97zL9ftTg

11 March 2024
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ameingilia kati mgogoro wa eneo la jengo la ghorofa lilipo Kariakoo jijini Dar es salaam ambalo sehemu ya jengo hilo lilitolewa Waqfu na marehemu Sheikh Mohamed Aldini ambaye aliacha usia.

Waziri Silaa alifika eneo hilo ambalo limekuwa na ugomvi mkubwa wa ndugu ambao ni watoto wa marehemu Ardini waliogawanyika katika pande mbili zinazokinzana kuhusu usia wa kuwekwa Waqfu eneo la Madrasa katika jengo hilo.

Aidha, baada ya kusikilizwa kwa pande mbili za ndugu ambao ni watoto wa marehem Mzee Ardini Waziri Silaa aliamuru kurejeshwa kwa Madrasa ambayo ilikuwa ndio usia wa marehemu.

Awali, ndugu wawili wanao pingana na wenzao waliamua kuhamishwa kwa madrasa hiyo nje ya eneo hilo la Kariakoo na kumuuzia mtu mwingine sehemu ya jengo hilo.

Source: Global TV Online

Pia, soma=>
Imamu wa msikiti adaiwa kushiriki kuuza nyumba ya familia Kariakoo iliyokuwa na waqfu. Mapanga yatembea nje nje

Wakfu ni nini?
 
anaweza akauza but with valid reason and for the benefit of heirs!

Msomi mwanasheria Jerry Silaa anasema kazi ya msimamizi wa mirathi ni tofauti na tunavyodhania kuwa kazi yake kuu ni kuuza mali nasi tunakimbilia kununua bila kwanza kutafakari kwa kina mazingira, na wasimamizi wengi hujivika jukumu hilo bila kujua ni tatizo kubwa kisheria.
 
Back
Top Bottom