Bakwata songea na upigaji kwenye dili la ununuzi wa nyumba ya mtekateka

Adjoub Adjoub

Member
Sep 11, 2017
82
48
Sheria dini ya Kiislamu zinakataza mtu kufanya aina yeyote ya dhuluma, utapeli, ulaghai na hiyana katika hatua nzima ya ufanyaji wa biashara iwe kwenye manunuzi au uuzaji.

Lakini utaratibu huo inaonekana kutozingatiwa na Kamati ya Manunuzi ya Baraza Kuu la Waislamu Manispaa ya Songea (BAKWATA) ikiongozwa na Mohammed Mfyule, Muqtar Simba, Sheikh Kitete, Songambele n.k, kudanganya waumini wa Msikiti wa Manispaa ya Songea kwamba wamenunua nyumba ya Marehemu Mzee Sefu Mtekateka yenye viwanja namba '8 K' na '10 K' kwa bei ya Tshs. 300 Milioni ilihali wauzaji wanadai wameiuza kwa Tshs. 240 Milioni pekee. Huku waumini wakihoji ziliko Tshs. 60 Milioni na nani aliyehusika kwenye matumizi yake.

Harufu ya upigaji imeanza kujitokeza hivi karibu baada ya baadhi ya waumini wa Msikiti huo kuanza kuhoji kiwango halisi cha bei na kukosekana kwa uwazi kwenye manunuzi ya viwanja hivyo. Wauzaji wa viwanja hivyo ambao ni watoto wa Marehemu Sefu Mtekateka wakiongozwa na msimamizi wa Mirathi aliyeteuliwa na Mahakama, Amina Sefu Mtekateka, wamekuwa wakiilalamikia Kamati hiyo ya manunuzi kwa kuwalaghai kwenye hatua za awali za Makubaliano ambapo Msikiti ulitaka Tshs. 60 Milioni ziwe kama sadaka ya lazima na 240 Milioni wagawane wauzaji.

Mkataba wa mauziano ya viwanja hivyo viwili vilivyo nyuma tu ya Msikiti huo mkongwe mkoani Ruvuma, uliitaka Kamati hiyo imalize malipo ya awamu ya mwisho mwezi Aprili mwaka huu (2023) lakini haikuweza kutekeleza makubaliano hayo kutokana na kuwepo kwa kesi dhidi ya Msimamizi wa Mirathi hiyo, Bi Amina.

Kesi dhidi ya Msimamiz wa Mirathi hiyo, imefunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mjini na aliyekuwa mke wa Marehemu Sefu Mtekateka na wajukuu kadhaa walioachwa na wanufaika wa Mirathi hiyo ambao inadaiwa 'walipigwa panga ' kwenye pesa ya mgao na msimamizi wa mirathi.

Pamoja na malalamiko hayo ya waumini, viongozi hao wa BAKWATA wamekuwa wakiwakwepa waumini wanaoonesha kuhoji suala hilo na wakati mwingine kuwapiga marufuku kufika msikitini hapo wale ambao wanaothubutu kuleta 'kidomo domo' dhidi yao.

Inadaiwa kuwa toka mwaka 2018, waumini wa Msikiti huo wa Manispaa na misikiti mingine wamekuwa wakifanya harambee ya kuchangisha pesa kwa ajili ya ununuzi wa viwanja hivyo viwili ikiwa ni sehemu ya jitihada za BAKWATA Manispaa kutanua Msikiti huo kwa lengo la kuweza kuwezesha kuingiza idadi kubwa ya waumini kufanya ibada zao tofauti na sasa ambapo Msikiti haukidhi mahitaji halisi.

Jitihada za mwandishi wa habari hii kuwatafuta viongozi hao wa BAKWATA ili kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma zinazowakabili zimegonga mwamba kutokana na hatua za viongozi hao kugoma kutoa ushirikiano pale wanapofuatwa ofisini kwao na wakati mwingine kutishia kuchukua hatua dhidi ya mwandishi.
 
Familia hiyo nayo ni chenga,sasa,kama hiyo mil60 si wameitoa kama sadaka?

Matumizi yake wanayaulizia nn?
 
Back
Top Bottom