Baada ya video kusambaa mtuhumiwa mwenye pingu akipigwa, askari aliyehusika awekwa mahabusu

Baada ya video inayomuonesha askari akimpiga mtuhumiwa aliyekaa chini akiwa na pingu, Jeshi la Polisi limemchukulia hatua askari huyo kwa kumuweka mahabusu.

Msemaji wa Polisi, SACP David Misime amesema: “Kitendo alichofanya askati huyo si tu ni kinyume cha sheria bali pia ni kinyume cha maadili ya Polisi, tayari hatua zimechukuliwa na Kamanda wa Polisi Kinondoni.

“Kijana anayeonekana akipigwa alituhumiwa kuiba simu aina ya Samsung Galaxy Note 10 ambayo alikiri kuiba na kwenda kuonesha mtu aliyemuuzia."
Video ya tukio pls!
 
Kuna watuhumiwa wanapigwa mpaka wanavunjwa miguu mwisho wa siku wanaonekana awana hatia na ulemavu washaupata.
 
Imetolewa na Jeshi la Polisi:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Ndugu wanahabari,

Imeonekana kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha kijana mmoja akiwa na pingu huku akipigwa na askari, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Ndugu wanahabari,

Kitendo hicho si tu ni kinyume cha sheria, bali pia ni kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi.Tukio hilo limeshachukuliwa hatua kuanzia jana na kamanda wa Polisi Kinondoni na askari aliyehusika yupo mahabusu na hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.

Kijana anayeonekana katika kipande cha video hiyo akipigwa, alituhumiwa kuiba simu aina ya Samsung Galaxy Note 10 ambayo alikiri kuiba na kwenda kuonyesha kwa mtu aliyemuuzia ambaye naye alikutwa na simu hiyo.
Jeshi la Polisi chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, litaendelea kusimamia Nidhamu, Haki, Weledi a Uadilifu kwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari Polisi anayekiuka sheria na maadili ya Jeshi la Polisi.

View attachment 2332502
Badilisheni curriculum yenu iendane na wakati wa ssasa, mwana umleavyo ndivyo akuavyo
 
Viko vingi tu zaidi ya hivyo.

Napendekeza askari wenu mue mnawapiga msasa matumizi sahihi ya PGO.

Wengi wao Yale mafunzo ya CCP washayasahau Wana act kwa hisia
Hiyo PGO ina msimu na msimu, maeneo na maeneo, watu na watu
 
Hapo bila shaka askari alikuwa ashakula advance kutoka kwa mwenye simu, na kaambiwa iliyobaki utaipata simu ikipatikana...
 
Hiyo imechukuliwa hatua kwasababu ya video kusambaa,ila bila hivyo hakuna ambaye angehangaika....... police wetu wanajiona wapo juu ya sheria na ukimuhoji huwa wanakuja juu as if humuheshimu..........
 
Imetolewa na Jeshi la Polisi:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Ndugu wanahabari,

Imeonekana kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha kijana mmoja akiwa na pingu huku akipigwa na askari, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Ndugu wanahabari,

Kitendo hicho si tu ni kinyume cha sheria, bali pia ni kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi.Tukio hilo limeshachukuliwa hatua kuanzia jana na kamanda wa Polisi Kinondoni na askari aliyehusika yupo mahabusu na hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.

Kijana anayeonekana katika kipande cha video hiyo akipigwa, alituhumiwa kuiba simu aina ya Samsung Galaxy Note 10 ambayo alikiri kuiba na kwenda kuonyesha kwa mtu aliyemuuzia ambaye naye alikutwa na simu hiyo.
Jeshi la Polisi chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, litaendelea kusimamia Nidhamu, Haki, Weledi a Uadilifu kwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari Polisi anayekiuka sheria na maadili ya Jeshi la Polisi.

View attachment 2332502
Elfu 50 aliyopewa askari ndio imesababisha yote hayo
 
Elfu 50 aliyopewa askari ndio imesababisha yote hayo

wizi mbaya.

unapona kuchomwa moto na wananchi,unabahatika kuokolewa na afande nayeye anapewa 50k akuweke sawa.

hii ni funzo kwamba wizi haufai,huwezi kuwa mwizi ukawa salama.
 
Back
Top Bottom