Baada ya video kusambaa mtuhumiwa mwenye pingu akipigwa, askari aliyehusika awekwa mahabusu

Umenikulbusha hichi kitabu
Screenshot_20220823-224740.png
 
hawa dawa yao unaenda umtrombea mkewe na mama yake, ni raha sana ukiwafanyia hivyo 😊
 
Maaskari wengi wa bongo hawana akili na huko kutokuwa na akili kunawafanya wasijue sheria.Yaan mtu ni askari lkn sheria hajui dah huruma sana kwa kweli wao wanachojua ni kutumia nguvu tu
 
Imetolewa na Jeshi la Polisi:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Ndugu wanahabari,

Imeonekana kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha kijana mmoja akiwa na pingu huku akipigwa na askari, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Ndugu wanahabari,

Kitendo hicho si tu ni kinyume cha sheria, bali pia ni kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi.Tukio hilo limeshachukuliwa hatua kuanzia jana na kamanda wa Polisi Kinondoni na askari aliyehusika yupo mahabusu na hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.

Kijana anayeonekana katika kipande cha video hiyo akipigwa, alituhumiwa kuiba simu aina ya Samsung Galaxy Note 10 ambayo alikiri kuiba na kwenda kuonyesha kwa mtu aliyemuuzia ambaye naye alikutwa na simu hiyo.
Jeshi la Polisi chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, litaendelea kusimamia Nidhamu, Haki, Weledi a Uadilifu kwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari Polisi anayekiuka sheria na maadili ya Jeshi la Polisi.


View attachment 2332502
Hiyo ni smartphone imesaidia. Sijui ambapo hakuna simu hali ipoje.
 
Hiyo video imeonyesha treatment anoyopewa mtoto wa waziri akifanya kosa na kuwa kituoni pamoja na mimi raia wa kawaida, hivi yule dogo wa simbachawene alipandishwa mahakamani?
 
Askari atoke bhna, wezi wapigwe wafe, ningekuwa na mamlaka ya kunyonga ninge nyonga wezi wenye kukamatika ni wezi, ushahidi ukiwepo mwizi afe tu.
 
Spidi iliyotumiwa na Jeshi la Polisi kuchunguza, kumkamata mtuhumiwa na hadi kupata Simu pamoja na mnunuaji ni la kupongezwa...Kama tu wanaweza fanya vivyohivyo na uhalifu- unaotokea kwenye nyara/rasilimali za Taifa-.ofisi za umma. Kuna tuhumu bwelele.

Huyo askari aliyefanya hilo ana walakin, yaani ana nguvu za kipolisi kisheria ana nguvu kama askari na ni dume na inawezekana alikuwa na bunduk, ni nguvu pia lakini kumbe ni bwegeeeee! Mtu ana pingu halafu askari anajifanya bruce lee!
Wacha sheria ifanye.
 
Back
Top Bottom