Polisi kushirikisha Wadau wa Haki Jinai kuchunguza malalamiko ya Wananchi kuonewa na Askari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Jeshi la Polisi nchini limesema limeona taarifa katika baadhi ya Mitandao ya Kijamii zikionyesha taarifa za Wananchi ambao wanalalamika kufanyiwa vitendo ambavyo ni kinyume cha Sheria na Haki za Binadamu na baadhi ya Askari Polisi.
IMG-20231207-WA0002.jpg

SACP David Misime

Akitoa taarifa hiyo Disemba 21, 2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema Wananchi hao ni pamoja na Getrude Masanja anayelalamika kufanyiwa vitendo kinyume cha Sheria huko Mkoani Kilimanjaro.

Pia Msemaji wa Jeshi hilo SACP Misime amesema kuwa taarifa nyingine ni ya Mwananchi aliyetambulishwa kwa jina la Kalamba anayelalamika kufanyiwa vitendo kinyume cha sheria huko Mkoani Dodoma.

Aidha, Misime amesema Jeshi la Polisi limeziona video hizo za malalamiko hayo na limeanza kuyafanyia uchunguzi mara moja wa malalamiko hayo kwa uzito mkubwa huku akiwaamba Wananchi kuwa watulivu kipindi hiki ambacho Jeshi hilo linafanya uchunguzi watuhuma hizo.

Ameeleza Jeshi hilo linafanya uchunguzi wa kina Ili kuhakikisha haki inatendeka huku akiongeza kuwa Jeshi la Polisi litashirikisha wataalam wengine wa Haki Jinai kuchunguza malalamiko hayo.

SACP Misime amewaomba Wananchi mwenye ushahidi kulingana na malalamiko yalivyowasilishwa na walalamikaji katika mitaandao ya kijamii asisite kujitokeza ili uchunguzi huo ukamilike mapema na hatua nyingine za kisheria zifuate.
 
Back
Top Bottom