Baada ya kufikisha miaka 30 uligundua kimebadilika nini katika Maisha yako?

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
18,030
45,594
Nimebakisha miaka 4 kuingia 30. Zamani tunakuwa tuliona miaka 30 ni mingi Sana ila sio kweli.

Jambo ambalo nimeona miaka 30 kwa TANZANIA Africa ndo Muda sahihi wa kujifanyia Self-Evaluation tathimini binafsi kwa kuangalia wapi ulikuwa wapi upo na wapi unahitaji ufike.

Pia katika miaka 30 unabidi una strong self-Imange uwe unajitazama Kuanzia ndani kwa picha yenye ubora na ukubwa na hii itakupelekea kuwa na self-esteem kujikubali na unapojikubali maana yake hautaendeshwa na nguvu kubwa kutoka nje ikiwemo kuzama katika Addiction zozote Kama Pombe,wanawake, bangi n.k

Maana chanzo Cha Addiction ni kukosa kujiamini Kuanzia ndani yako hivyo unatafuta Nguvu kutoka nje ili ikusaidie kukupa short pleasure.

Mwisho miaka 30 itapendeza ikukute ukiwa tayari upo na ule uimara wa ndani wa kutokubali sauti kutoka nje yako kukuambia hauwezi au hauna thamani au kuchukuliwa poa.

Vijana wengi bado tunasumbuliwa na kitu kinaitwa Limps limps ni kutokuwa na uimara wa ndani hivyo tunabidi kuwa na Uelewa mzuri kuhusu limps maana ukiwa hauna uimara wa ndani utaogopa kujaribu fursa mbalimbali kwa kuamini hizo fursa zipo kwa ajili ya watu fulani.

Aging is inevitable live ur life Enjoy and cherish every single moment.
 
Back
Top Bottom