Aliyekata rufaa kupinga kifungo cha miaka 30 afungwa maisha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Rufaa ya pili aliyokata mkazi wa Kijiji cha Mwanambaya, Wilaya ya Mkuranga, Denis Joseph, kupinga kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanafunzi imegeuka msiba baada ya kujikuta akiambulia kifungo cha maisha.

Mahakama ya Rufani imekubaliana na Wakili wa Serikali, Elizabeth Olomi kuwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 alichopewa Joseph, maarufu kama Saa Moja kwa shitaka la ulawiti ilikuwa kinyume na sheria.

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Olomi aliikumbusha Mahakama kuwa kifungo alichopewa Joseph kilikuwa kinyume na kifungu cha 154 (2) cha Kanuni ya Adhabu kinachotoa adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu yeyote anayetiwa hatiani kwa kulawiti mtoto cha umri wa chini ya miaka 18.

“Katika kesi iliyo mbele yetu, kwa kuwa mwathirika wa kosa hilo alikuwa na umri wa miaka 10 siku ya tukio, kifungo sahihi kilitakiwa kiwe kama kilivyotamkwa na sheria.

“Kwa hiyo, tunatumia mamlaka tuliyopewa kuweka kando kifungo cha miaka 30 na kutoa kifungo cha maisha,” walisema majaji Rehema Mkuye, Mwanaisha Kwariko na Patricia Fikirini katika hukumu yao ya hivi karibuni.

Tayari Joseph alikuwa ametumikia miaka minne gerezani tangu alipotiwa hatiani kwa mara ya kwanza na kufungwa miaka 30 na Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga mwaka 2019.

Siri ilivyofichuka

Dalili za kufichuka kwa unyama uliodaiwa kufanywa na Joseph dhidi ya mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) ambazo familia hizo zilikuwa jirani, zilianza Juni 2018 baada ya baba wa mtoto huyo kupokea taarifa za kushtua kutoka kwa mke wake.

Aliiambia Mahakama wakati akitoa ushahidi kuwa mke wake alimweleza kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa mke wa mrufani (Joseph) kuwa mtoto wao ana uhusiano wa kimapenzi na mume wake na kuwataka wamuonye.

Kufuatia taarifa hiyo, baba wa mwathirika alimbana mwanaye amueleze ukweli na mtoto huyo alifunguka na kueleza kuwa amekuwa akifanya mapenzi na mrufani kwa kubakwa na kulawitiwa.

Ushahidi wa mwathirika

Akitoa ushahidi, binti huyo aliyekuwa akisoma katika shule moja ya msingi wilayani Mkuranga alisema siku moja wakati akitoka kuteka maji alikutana na Joseph ambaye ni jirani yao.

Alidai siku hiyo mrufani akamrukia na kusababisha ndoo ya maji aliyobeba kuanguka.

“Alinivuta hadi kichakani, akanivua nguo zangu na kushusha suruali yake hadi kwenye magoti. Alinilaza chini kwa nguvu na kuingiza uume wake sehemu zangu za siri,” alisema mwathirika huyo wakati akitoa ushahidi.

Kwa mujibu wa mwathirika, kitendo kile kilimsababishia maumivu makali yaliyomfanya apige kelele.

“Kabla hajaondoka (Joseph) alinionya nisiwaambie wazazi wangu kilichotokea. Nilivaa nguo zangu likini sikuweza kutembea vizuri. Nilirudi tena kuchota maji na kuelekea nyumbani,” alisema.

Mwathirika huyo aliieleza Mahakama kuwa, mara ya pili alipokutana na unyama wa Joseph, alipokuwa njiani kwenda kumsaidia mama yake kazi katika shamba.

“Wakati napita karibu na nyumbani kwake (Joseph) alinikamata na kujaribu kunivutia ndani ya nyumba yake, bahati nzuri mke wake akatokea na yeye (Joseph) akaonyesha hakuna kilichotokea,” alisema mwathirika huyo.Katika tukio la mara ya tatu, mwathirika huyo alidai kuwa siku moja wakati akielekea kanisani, mrufani aliibuka kutoka nyuma yake na kumvuta pembeni kabla ya kumbaka na kumlawiti ambapo baada ya kumaliza alielekea kanisani.

Alisema matukio hayo yalifichuka baada ya mke wa Joseph kumweleza mama yake wasiwasi alionao juu ya uhusiano wa mtoto wake na mume wake.

Ni hadi wazazi wa binti huyo walipomhoji ndipo alipotoa siri hiyo iliyosababisha mrufani kukamatwa.

Ushahidi wa daktari

Daktari Seif Mussa Mkwinda, aliyemfanyia uchunguzi mwathirika, aliieleza Mahakama kuwa alikuta makovu sehemu za siri za binti huyo, bikira ikiwa imetoka na sehemu hiyo kuonekana kuwa pana ukilinganisha na umri wake.

Pia, aligundua kuwa sehemu ya nyuma ya binti huyo ilikuwa na makovu ya siku nyingi. Alihitimisha kuwa alikuwa ameingiliwa na kubakwa.

Utetezi wa Joseph

Katika utetezi wake, mrufani huyo alieleza kuwa anakumbuka Februari 2018, baba wa mwathirika alikuja nyumbani kwake akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaye. “Nilishtushwa na hizo tuhuma kwa kuwa familia zetu mbili zilikuwa na uhusiano mzuri kama ndugu, kwa hiyo nilidhani utani tu. Jirani yangu akasema atashughulika na mimi.

“Hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa hadi Juni 2018 pale mke wake alipokuja kuniambia ninahitajika kwenye ofisi ya kijiji,” alisema.

Bendera haipepei

Joseph alidai asingeweza kufanya kitendo anachodaiwa kufanya kwa kuwa hakuwa na nguvu za kiume; na japokuwa alikuwa ameoa hakuweza kumtimizia mke wake haja zake kama mume.

Alidai mke wake alikuwa na matatizo ya akili, hivyo malalamiko dhidi yake ya kujihusisha na mapenzi nje ya ndoa hayakupaswa kupewa uzito.

Pia, alilalamika kuwa kesi dhidi yake ilikuwa ya kupika japokuwa hakuwa na ugomvi wowote na familia ya mwathirika kwa kuwa waliishi kwa amani kama ndugu.

Mwisho wa siku, Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga iliukataa ushahidi wake, ikamtia hatiani na kumpa kifungo cha miaka 30 jela.

Jaribio lake la kwanza kupinga kutiwa hatiani na kufungwa lilikwama pale Mahakama Kuu ilipokataa rufaa yake.

Aenda Mahakama ya Rufani

Joseph hakuridhika na kukataliwa kwa rufaa yake na Mahakama Kuu, hivyo aliamua kukata rufaa mahakama ya juu kabisa nchini, Mahakama ya Rufani.

Alisema maelezo ya kosa katika hati ya mashitaka yalikinzana na ushahidi wa mwathirika.

Pia, alidai kuwa Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga ilikiuka kifungu cha 234 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Jinai kinachompa mshitakiwa haki ya kujibu tena shitaka au kuita tena mashahidi kutoa ushahidi upya au kuhojiwa upya mshitakiwa au wakili wake pale upande wa mashitaka unapoamua kubadili kosa katika hati ya mashitaka.

Mawakili wa Serikali, Elizabeth Olomi na Rachel Mwaipyana waliiwakilisha Serikali katika rufaa hiyo. Mawakili hao walisisitiza kuwa upande wa mashitaka ulithibitisha kosa dhidi ya mshitakiwa bila kuacha shaka na kwamba Mahakama Kuu haikukosea kukataa rufaa yake ya kwanza.

MWANANCHI
 
Pamoja na kufungwa maisha, mbakaji huyo angepitishiwa hukumu y kuhasiwa.
 
very disturbing indeed.
 
Attachments

  • rape mkuranga life imprisoment.pdf
    365.9 KB · Views: 10
Babu Seya alijitetea kuwa hasimamishi ,lakini alipotoka jela akaja Songea kuoa.
Huyo mwamba Naye kajitetea kuwa hasimamishi lakini ana mke na watoto.
Kwanini wabakaji wengi hupenda kusingizia hiyo kitu?
Hivi hakuna njia ya kupima Kama unasimamisha au la?
 
Back
Top Bottom