Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Uko sahihi kabisa, huyu Pslmp akubali mikataba yote tata ipelekwe bungeni. Kelele hazijaanza leo kwa huu wa Bagamoyo, yote yenye ukakasi ikajadiliwe tupate mwanga. Ununuzi wa ndege umepigiwa kelele sana, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, kelele tumezisikia, kwa nini huyu Pslmp anataka huu wa Bagamoyo tu?
 
Huyu ni sura halisi ya MCHUMIA TUMBO, ambaye anakwenda na "upepo"; na kwa akili yake, anadhani kesha jua na kufahamu "upepo" huu wa sasa hivi UNAVUMAJE? Ananchofanya ni kubahatisha tu, hivyo aangalie isije IKALA KWAKE!
Tuna hasara kubwa Sana Watanzania, huwezi kaa kimya miaka sita yote husemei Bandari, halafu leo tena baada ya Raisi kufariki ndipo uje kutuonyesha uzuri wa uwekezaji huo

Kwani isiwe 2015, ni Kweli yeye alikuja na ushauri huo baada ya kwenda China, akapendezwa na Ile ramani na bandari ya wawekezaji hao Kwa jinsi ilivyo kubwa na nzuri, lkn mkuu aliposoma Mkataba ule akasema, nanukuu, Ni mwenda wazimu pekee wa kuruhusu ujenzi wa Bandali hiyo baada ya hapo mkuu wa mhimili wa Bunge naye akaunganishia hapohapo, mjadala ukazimwa

Kwa nini leo auone ni Mradi Safi tena baada ya kifo cha Raisi alitekuwepo?? Je aliahidiwa Lupia kutoka Kwa wawekezaji hao??

Tunataka Mkataba wote usomwe bungeni Maana tunajua, sio Bunge loote likakosa mtu muungwana hata mmoja ingawa CCM siiamini tena!
 
Sawa mkuu, ulitaka kuhitimishaje
Kwenye chaguzi zijazo, tuache demokrasia ichukue mkondo wake. Uvurugaji wa uchaguzi wa 28 October 2020, hautasahalika katika historia ya chaguzi Tanzania. Hicho kilichopo bungeni ndicho JPM na wana CCM walikishangilia na kukiita ushindi wa kishindo na wakihistoria.
 
Si unajua Watanzania ni kama bendera na upepo!!
 
Ukweli ni kuwa ukifanya comparison analysis ukiwa objectively kabisa kati ya mikataba iliyoingiwa wakati wa JK na ile ya wakati wa JPM utaona mikataba karibia yote ya wakati wa JK ilikuwa ya kipigaji kuliko ya wakati wa JPM.
Umeshaona mikataba mingapi mkuu? K
 
Usemi huo hapo juu wa Hayati Rais Magufuli utasimamiwa na Watanzania wapenda haki kwa kupinga kwa nguvu zote huo mradi wa KIJINGA NA HOVYO, hata hao Wabunge sidhani kama wataunga mkono UPUUZI HUO. Ndugai na Wanamtandao wenzake hawana ubavu wa kuutetea mradi huo wa kjinga, alichofanya huyu ni KUJARIBU KUPIMA MAJI KWA MIGUU, yataondoka naye!
 
Hawa wachumia matumbo wasitake kumchanganya yoyote ni miradi ya MATUMBO YAO. Huyu alikuwa mstari wa mbele kusifu na kuitia NDIYO kwa mambo yote aliyosema Hayati Rais wetu Magufuli. Leo anakuja na upuuzi wa kuitaka Bandari ya Bagamoyowakati wa mjadala wake wakati ule Bungeni alikiri kuwa ni MRADI WA HOVYO. leo anauona ni mradi mzuri; na anasimamndani ya chombo kitakataifu kama Bunge na kuanza kusemasema maneno ya UONGO. ASHINDWE NA ALEGEE na Wanamtandao wenzake.

Nimemsikia pia kuhusu ndege za Air Tanzania! Huyu mtu VIPI!? Anaanza kupiga U-TURN hata yule aliyekuwa akimuunga mkono, hatujamsahau!? Kweli hawa watu vipi!? U - ndio na U - yes kwa Hayati umeisha mapema hivi? Kweli hakujua kuwa Air Tanzania kuna matatizo, hadi CAG aseme ndio na yeye atie neno, ubabaishaji gani huu?

Tusubiri tutawaona wengi wakipiga U-TURN na KUGEUKA MAWE kwa maslahi na matumbo yao wenyewe. Ila wakumbuke CCM bado ni imara na itasimamia maslahi mapana ya Taifa hili.
Walipenda kuimba wimbo uliopendwa na aliyewalipa. "Anayemlipa mpiga zumari, ndiye huchagua wimbo aupendao" By J K Nyerere.
 
Eti, Raisi hakushauriwa vizuri kuhusu mradi wa ujenzi bandari ya Bagamoyo, Wakati huohuo yeye ndiye mshauri mkuu wa serikali, alikuwa wapi?

Raisi wetu amefariki ndo kunakupa mwanya wa kumwandama na kumkandia kila Neno Baya, sasa tunataka mtwambie kama Kweli kazi yenu ni kuishauri serikali na kuisimamia

Kabla ya tamko lake Jana kuhusu ujenzi na uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo, aliwahi pia kutamka kwamba, mradi huo ni hasara Kwa Serikali Kwa jinsi Mkataba wake ulivyokaa, na kama ndivyo, yeye ndiye ametufanya kama Taifa tuchelewe kuwa na mradi huo,

Sasa Sisi tushike lipi?

Najiuliza, Yeye kama mkuu wa mhilimili huo, anaongoza chombo chenye kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali, Alikuwa wapi, mbona alitaka Raisi aongezewe muda wa kutawala? Si ni yeye jamani au ni mwingine!! Je, hakuwa analiona tatizo la ufisadi uliokuwa unaendelea?

Kwa tarifa ya CAG imeibua madudu makubwa na ufisadi wa kutisha, badara ya yeye na mawaziri wote kama sio Bunge loote kuwajibike Kwa kushindwa kuisimamia serikali anaibuka na Jambo la ajabu tu ili kutuondoa kwenye Hilo la ufisadi, hivi mnaaibu kweli nyinyi watu!

Tukionyesha hasira zetu wananchi tuliowatuma kwenda kusimamia rasilimali zetu mnatutumia wasiojulikana, ni Sawa Kwani kufa ni kutangulizana Tu

Tunalitaka Bunge liwajibike katika hili, la sivyo mtuambie ni Kwa nini mlitaka Raisi aongezewe muda

Tunataka pia, mradi wa Ujenzi bandari ya Bagamoyo, Mkataba wake uwekwe mezani tuambie yaliyomo na Kisha Bunge loote livunjwe, Kwani ni hasara tupu!!

Acha tupige 🏋️🏋️🏋️

Kumbe hamuaminiki tena!!
Ndugai ana yake ya kujibu sioni kama anastahili kuwepo hadi mwisho wa mwaka huu.
 
Ndugai ana yake ya kujibu sioni kama anastahili kuwepo hadi mwisho wa mwaka huu.
Swali langu ni moja tu, Kwa nini alitaka amwongezee muda wa utawala?

Ni Kwa sababu alizuia Mradi wa bandari ya Bagamoyo.. ama nini hasa!!
 
Kwa hiyo hapa unataka kuniambia Professor Assad alikuwa sahihi???
Mkuu, alikuwa Sawa kabisaa

Ni mnafiki mno huyu jamaa, anayumba vibaya, utamsikia atavyofoka Leo na hizi nyuzi za kumponda kuruhusu wizi huu makubwa,
 
Eti, Raisi hakushauriwa vizuri kuhusu mradi wa ujenzi bandari ya Bagamoyo, Wakati huohuo yeye ndiye mshauri mkuu wa serikali, alikuwa wapi?

Raisi wetu amefariki ndo kunakupa mwanya wa kumwandama na kumkandia kila Neno Baya, sasa tunataka mtwambie kama Kweli kazi yenu ni kuishauri serikali na kuisimamia

Kabla ya tamko lake Jana kuhusu ujenzi na uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo, aliwahi pia kutamka kwamba, mradi huo ni hasara Kwa Serikali Kwa jinsi Mkataba wake ulivyokaa, na kama ndivyo, yeye ndiye ametufanya kama Taifa tuchelewe kuwa na mradi huo,

Sasa Sisi tushike lipi?

Najiuliza, Yeye kama mkuu wa mhilimili huo, anaongoza chombo chenye kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali, Alikuwa wapi, mbona alitaka Raisi aongezewe muda wa kutawala? Si ni yeye jamani au ni mwingine!! Je, hakuwa analiona tatizo la ufisadi uliokuwa unaendelea?

Kwa tarifa ya CAG imeibua madudu makubwa na ufisadi wa kutisha, badara ya yeye na mawaziri wote kama sio Bunge loote kuwajibike Kwa kushindwa kuisimamia serikali anaibuka na Jambo la ajabu tu ili kutuondoa kwenye Hilo la ufisadi, hivi mnaaibu kweli nyinyi watu!

Tukionyesha hasira zetu wananchi tuliowatuma kwenda kusimamia rasilimali zetu mnatutumia wasiojulikana, ni Sawa Kwani kufa ni kutangulizana Tu

Tunalitaka Bunge liwajibike katika hili, la sivyo mtuambie ni Kwa nini mlitaka Raisi aongezewe muda

Tunataka pia, mradi wa Ujenzi bandari ya Bagamoyo, Mkataba wake uwekwe mezani tuambie yaliyomo na Kisha Bunge loote livunjwe, Kwani ni hasara tupu!!

Acha tupige

Kumbe hamuaminiki tena!!
Ndugu zangu haya yaliyoibuliwa na CAG ni machache ya mengi ya yanayoendelea humu nchini kwa mfano nikizungumzia miradi ya maendelee hususani mradi wa reli ya SGR kuna madudu ya kufa MTU nikianza tuu na maswala ya rasilimali watu waturuki waliokuja hawajui kitu. Kuna makampuni Tanzu (sub) hazina usajili wowote kama vile CRB na bodi imekaa tuu wala hawafuatilii ukija kwa ma Engineer ndio kabisa wapo wakutosha hawajasajiliwa na bodi ERB na bodi IPO tuu ikumbukwe sio pesa tuu za registration tunapoteza ila pia hawajamaa wana jeopardize nafasi za wazawa na pia kuikosesha serikali mapato payee.

Quality ya kazi ni mbovu kupata kuona transformer mbovu zimefungwa tusubiri wakati wa operation tutaona mengi maana maintenance itakuwa ya garama sana maana vitu vilivyofungwa ni repair tuu kwa mfano km153 DATS-03 transformer mojawapo ilipo pale ni mbovu. Na mambo mengine ya ovyo kabisa nasikitika sana maana serikali yetu imeashindwa kuwa na watalamu wa kutosha kusimamia hivi vitu ili hali tupo watu wenye ujuzi na utaalamu wa kutosha tupo tuu mtaani.
 
Mkuu, alikuwa Sawa kabisaa

Ni mnafiki mno huyu jamaa, anayumba vibaya, utamsikia atavyofoka Leo na hizi nyuzi za kumponda kuruhusu wizi huu makubwa,
Mkuu mambo ni ya ovyo huko serikalini hamna haja ya kuwa na serikali kama MTU mwenye dhamana ya kuisimamia serikali unasema eti alishauriwa vibaya wewe ulikuwa wapi wakati unalipwa kwa kazi hiyo.
 
Unasema Hana msimamo ,ivi wewe unaweza bishana na boss wako au kiongoz wa nchi?

Je na sisi wananchi tunaowaza mbali Zaid tutajuaje huenda rais nae aliona mradi ule hawez pata 10percent Kama wapatavyo kwenye mirad mingine ndio maana akauponda?

Kijana zinduka usimwamin mwasiasa yeyote yule ,wote ni wapigaji dili tu ,awe jiwe kashatuliza sana tena sana ni vile rais hajadiliw lakin watu wana mafail yake mengi .

Mayanga construction unajua ni ya Nan ,
Unajua mashart ya ule mkataba yalikuaje ? Ukiona mtu anapinga mradi Fulani ujue haufaidishi yeye Kama yeye na ukiona unaupambania jua huo mrad unamfaidisha binafs either kwa kuweka kampuni yake kwa mlango wa nyuma au kupata asilimia fulan.

Ni mpumbavu tu atamwamin jiwe kuwa ule mrad ulikuwa na madudu mengi ,vipi atcl yake iliyoingiza hasara ya 155b kwa miaka mitano tu .

Unajua huyo jiwe kapiga kias gani kwenye hii miradi ya ujenz wa barabara na mirad mingine ?

Unaweza kuwa sahihi kwamba huenda spika alihongwa chochote ili aupigie debe lakin pia upande wa pil unaweza kuta yeye aliona kabisa hapat kitu Kama ganji kwa hao jamaa kwa hasira aliamua kuukataa ,yote yanawezekana so usiwe upande mmoja

Tutaongea mambo meeengi then hakuna muafaka.

Hapa mkataba wa mradi uwekwe wazi tujue nani mwendawazimu ama kichaa kati ya wanao ukubali na yule alieukataa full stop.
 
Back
Top Bottom