Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,622
2,459
Eti, Rais hakushauriwa vizuri kuhusu mradi wa ujenzi bandari ya Bagamoyo, Wakati huohuo yeye ndiye mshauri mkuu wa serikali, alikuwa wapi?

Raisi wetu amefariki ndo kunampa mwanya wa kumwandama na kumkandia kila Neno Baya, sasa tunataka mtwambie kama Kweli kazi yenu ni kuishauri serikali na kuisimamia

Kabla ya tamko lako Jana kuhusu ujenzi na uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo, uliwahi pia kutamka kwamba, mradi huo ni hasara Kwa Serikali Kwa jinsi Mkataba wake ulivyokaa, na kama ndivyo, wewe ndiye umetufanya kama Taifa tuchelewe kuwa na mradi huo, unapaswa kujibu hili

Sasa Sisi tushike lipi?

Najiuliza, Yeye kama mkuu wa mhilimili huo, anaongoza chombo chenye kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali, Alikuwa wapi, mbona alitaka Raisi aongezewe muda wa kutawala? Si ni yeye jamani au ni mwingine!! Je, hakuwa analiona tatizo la ufisadi uliokuwa unaendelea?

Istoshe, yeye huyohuyo ndiye aliyekataa kufanya kazi na CAG msomi bwana Assad, alimaanisha nini??

Kwa tarifa iliyosomwa na CAG bwana Kichere, imeibua madudu makubwa na ufisadi wa kutisha, badara ya yeye na mawaziri wote kama sio Bunge loote kuwajibika Kwa kushindwa kuisimamia serikali anaibuka na Jambo la ajabu tu ili masikio yetu ayaondoe kusikia tarifa za CAG, na ili tu tuanze kusikia habari za ujenzi bandari yetu pale Bagamoyo na yeye aone kama anapata pa kujipatia Kiki!! Haitawezekana,

Uliogopa nini kumshauri Raisi hapo awali kama kweli mradi haukuwa na tatizo, Kwa hiyo uliamua kumpaka uji Kwa mgongo wa chupa??

Tukionyesha hasira zetu wananchi tuliowatuma kwenda kusimamia rasilimali zetu mnatutumia wasiojulikana, ni Sawa Kwani kufa ni kutangulizana Tu

Tunalitaka Bunge liwajibike katika hili, la sivyo mtuambie ni Kwa nini mlitaka Raisi aongezewe muda

Tunataka pia, mradi wa Ujenzi bandari ya Bagamoyo, Mkataba wake uwekwe mezani tuambie yaliyomo na Kisha Bunge loote livunjwe, Kwani ni hasara tupu!!

Acha tupige 🏋️🏋️🏋️

Ni wakati wa speeker kuwajibishwa na Bunge lake

Kumbe hamuaminiki tena!!
 
Huyu Speaker wetu nadhani Haijapata kutokea wa namna hii toka Dunia hii iumbwe.. "Huyu Huyu Ndie alikuwa anasema Mwendazake atake asitake ataongezewa Muda" Wenye ile Clip ebu tuwekeeni. Ni aibu sana Kwa CCM maana hii nafasi huyu mtu wenu Inampwaya sana...Kaputura la MAX by Keizirahabi.
 
Kwa kumbukumbu zangu Ndugai alisema bungeni akiwa ktk kiti cha spika kwamba mradi wa Bagamoyo ni wa faida sana ameupitia kwa kina Mpaka huko China.

Baada ya muda mfupi Hayati akaukandia kwa kutoa nukuu ya vipengele kadhaa vya kiunyonyaji ambavyo sisi wananchi hatujui kama ni kweli au sivyo.Hapo ndipo Ndugai ikabidi atumie kanuni ya The boss is always right

Binafsi Siamini yale yaliyosemwa na JPM juu ya mradi huo wala yanayosemwa na wanaoutaka sasa Mpaka nipate "bahati"ya kusoma mkataba huo.

Serikali iruhusu mikataba yenye mivutano kama huu upelekwe bungeni kwa mjadala hapo sisi wananchi tutajua mbivu na mbichi
 
Kwa kumbu kumbu zangu Ndugai alisema bungeni akiwa ktk kiti cha spika kwamba mradi wa Bagamoyo ni wa faida sana ameupitia kwa kina Mpaka huko China.

Baada ya muda mfupi Hayati akaukandia kwa kutoa nukuu ya vipengele kadhaa vya kiunyonyaji ambavyo sisi wananchi hatujui kama ni kweli au sivyo.Hapo ndipo Ndugai ikabidi atumie kanuni ya The boss is always right

Binafsi Siamini yale yaliyosemwa na JPM juu ya mradi huo wala yanayosemwa na wanaoutaka sasa Mpaka nipate "bahati"ya kusoma mkataba huo.

Serikali iruhusu mikataba yenye mivutano kama huu upelekwe bungeni kwa mjadala hapo sisi wananchi tutajua mbivu na mbichi
Ukweli ni kuwa ukifanya comparison analysis ukiwa objectively kabisa kati ya mikataba iliyoingiwa wakati wa JK na ile ya wakati wa JPM utaona mikataba karibia yote ya wakati wa JK ilikuwa ya kipigaji kuliko ya wakati wa JPM.
 
Back
Top Bottom