AZAM TV nawahama kwa kweli

AZAM TV nawahama kwa kweli

Kina shida gani kwani
Sometimes channel zinakata zenyewe.
Wana vichannel vyao vingi vingi kama star drama,star movies,star cinema yaani ni kurudia vipindi mwanzo mwisho.
Kma hiyo star cinema kila siku ni hizohizo hazijawahi badilishwa.
Channel zilizopo vizuri ni Citizen,KTN,ITV,Clouds,Eatv na na nyingine
Kama wewe ni mpenzi wa movies tens nzuri kwa hiki utakuw umelamba garasa.
Bila kusahau unaweza ukakaa wiki nzima kingamuzi hakionyeshi channel kabisa na umelipia sijui ndio wanakuwa wanatengeneza.
Saa nyingine mvua ikinyesha kinakata.
Kifurushi kikiisha hata local channel hupati utaambulia star tv peke yake.
 
Wanavyo,na unaweza ukanunua receiver ya star times kwa 39000 tu na ukatumia dish la azam bila shida yoyote
Je naweza kutumia receiver ya star times kwa dish La Zuku?
 
Nyie AZAM TV mnatujazia chaneli za makabachori utafikiri wateja wenu wengi ni makabachori?!!!.Leteni chaneli ambazo zinasisimua uchumi wa viwanda,kuwafahamisha watu wapi fursa zipo sio hizo za kuigiza maisha ya kusadikika tumechoshwa sasa.
BADILIKENI TUENDE SAWA OTHERWISE MTAANGUKIA PUA KAMA STAR TIMES SIKU SI NYINGI!!
 
Hawa azam bhana mm nangalia chanel 5 tu halafu nalipia 18000 muda wa kungalia wenyewe sina ni bora tuziwe chanel moja moja mtu unayo itaka
Nishawahi kuizungumza kwa DSTV, Sema wanajifanya kichwa maji njaa zikiwatafuna watafanya ivvyo
 
habari zenu wakuu,

Nilijiunga na Azam Tv baada ya kuona humu JF watu wanaisifia sana. na channel zangu pendwa zilikuwa mbili tu AMC series na AMC Movie. sasa wametoa hizo channel yaani Azam haina radha tena. najirudia zangu star times pamoja na mapungufu yao lkn wanaeleweka angalau. sasa hivi najitahidi kuangalia tu fox.

Mambo yakikaa sawa nahamia DSTV nafikiri hawa hawana longolongo. nimeangalia kwenye channel list nimeona AMC zipo kwenye kifurushi cha chini. Wakuu watumiaji wa DSTV naombeni mnijuze hawa DSTV na wenyewe upuuzi wa kutoa channel wanavyojisikia wanao?

Azam mnajiharibia biashara sana, tunapiga simu kuulizia majibu hayaeleweki.
DSTV ukiachilia mbali bei zao, lakini kwenye stability wako vizuri sana. Hawabadili badili sana channels.
 
Digitek hawajawahi niangusha. Kwanza ni bure, hakuna malipo yoyote baada ya kununua king'amuzi. ITV, TBC1, Channel 10, Star TV, EATV, Capital, Algezeera, Citizens TV, Emmanuel TV, Ipo nyingine ya Kiislam, na zingine kibao kama za Japan na maigizo n.k.
Kwa matumizi nyumbani na kwa kuwa sina muda wa kuangalia Tv zaidi ya taarifa ya habari nadhani hizo zinanitosha.
Ndio sh ngapi mkuu? Bei yake
 
Je naweza kutumia receiver ya star times kwa dish La Zuku?
Unatumia bila shida tena kama ulikuwa umeshafunga zuku usiitoe hapo weka tu receiver itaendelea kukamua kama kawaida.Startimes na zuku wapo kwenye satellite moja,ushauri wa buree bila kumuita fundi
 
Nyie AZAM TV mnatujazia chaneli za makabachori utafikiri wateja wenu wengi ni makabachori?!!!.Leteni chaneli ambazo zinasisimua uchumi wa viwanda,kuwafahamisha watu wapi fursa zipo sio hizo za kuigiza maisha ya kusadikika tumechoshwa sasa.
BADILIKENI TUENDE SAWA OTHERWISE MTAANGUKIA PUA KAMA STAR TIMES SIKU SI NYINGI!!

wengine hatupendi hayo mambo ya viwanda tunataka channels za burudani kama Trace tv cartoon network na E!
 
Back
Top Bottom