Awamu hii kama una silaha usitembee nayo. Utawala wa kambare, kila mtu anasharubu. Unaweza jikuta unaua mtu bure

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Huko barabarani siku hizi madereva wa magari ya serikali wamekuwa wababe kupitiliza!

Nchi inaongozwa kwa sheria na taratibu!

Usalama barabarani unaongozwa na sheria za usalama barabarani.

Lakini bahati mbaya sana madereva wa magari ya serikali na polisi, Trafiki ,wanaUsalama, wanajeshi, Migambo na Greegurd wa ccm awamu ya sita wamekuwa wababe sana huko barabarani.

Nashauri ile sheria ya kuondoa NGAO ITILIWE MKAZO MAGARI YOTE YA SERIKALI YANG'OLEWE NGAO! ikiwezekana yapakwe rangi za taasisi yajulikane!

1. Majuzi hapo Tabata gari la polisi lenye NGAO lisilokuwa na plate number liliyangonga magari yaliyokuwa kwenye foleni ili kuyalazimisha yatanue ili lipite katikati yao, na baada ya kugonga wala HALIKUSIMAMA.

2. Mwezi uliopita kuna gari ya serikali ilitanua pale Lugalo Mwenge (opposite direction yaani ilipita barabara ya kwenda Tegeta ilihali inakwenda mjini nakupasua taa za daladala na haikusimama).

3. Mwezi huu huu wa tatu, maeneo ya kunduchi mtongani asubuhi mapema gari ya serikali yenye king'ora juu ilitanua na kugonga gari ndogo na kupasua taa wala haikusimama!

Kwa mifano hii michache! Nawashauri ndugu zangu kama una SILAHA yoyote hata kama ni RUNGU AU KISU AU BASTOLA bora usiibebe

maana UKIBEBA SILAHA unaweza kuitumia pasipo tarajiwa awamu hii ya sita hata kibarua wa serikali ameota sharubu!

Lakini kwa wale wenye hasira kama zangu tujitahidi kujizuia sana tusije yachoma moto hayo magari ya serikali yanayoendeshwa na madereva wajinga HATA KUWATIA NDOSI ZA UTOSI.

Viongozi hawawi mifano bora, hawa madereva wanatiwa viburi na baadhi ya tabia mbovu za viongozi!

Mambo kama hayo hutatuliwa kwa kutoa kafara gari ya kiongozi mmoja mkubwa anaevunja sheria mifano! Magufuli kipindi kile alimwamulisha yule mke wa waziri enzi hizo gari lake lilipokamatwa
 
Juzi niko moro pale stendi ya zamani mkabala na benki ya equity, kuna zebra pale za kuvukia waenda kwa miguu.

Raia tukiwa tunavuka na baadhi ya magari yakiwa yamesimama kwa mujibu wa Taratibu, Ghafla ilitoka STK moja hivi na kutanua kuyakwepa yale magari yaliyosimama kwenye zebra na nusura kugonga raia.

Afu jamaa huyooooo, nilichukia sana sana hasahasa kwa vile ni gari la serikali na linafanya makosa mpaka kuhatarisha maisha ya watu.

Tukiongea kuhusu sera mbovu za huyu bibi watasema sisi ni sukumagang.

Ila katu sitoweza kuja kusema lile neno eti “ nani kama mama” “anaupiga mwingi” wakati ni hopless kabsa huyu bibi
 
Kichwa ndio mtu.......utimamu wa kichwa unapimwa kupitia utimamu wa utendaji wa viungo vingine vya mwili.....na ubaya wa kichwa pia unapimwa kupitia ubovu wa utendaji wa viungo mwilini.......
 
Dereva ambaye ukimuudhi kidogo anashuka na panga anafahamika kama agressive driver. Ni hatari
 
Tanzania watu ni wababe sana aisee harafu wengi wanaamini bara bara ni ya magari tu sio na ya waenda kwa miguu ukiona dereva anajali waenda kwa miguu jua huyo kastaraabika wengine wanashindwa hata kusimama kuwapisha watoto wa shule Zebra...
 
Viongozi ndiyo hawawi mifano kwa watu wake
 
Juzi niko moro pale stendi ya zamani mkabala na benki ya equity, kuna zebra pale za kuvukia waenda kwa miguu.

Raia tukiwa tunavuka na baadhi ya magari yakiwa yamesimama kwa mujibu wa Taratibu, Ghafla ilitoka STK moja hivi na kutanua kuyakwepa yale magari yaliyosimama kwenye zebra na nusura kugonga raia.

Afu jamaa huyooooo, nilichukia sana sana hasahasa kwa vile ni gari la serikali na linafanya makosa mpaka kuhatarisha maisha ya watu.

Tukiongea kuhusu sera mbovu za huyu bibi watasema sisi ni sukumagang.

Ila katu sitoweza kuja kusema lile neno eti “ nani kama mama” “anaupiga mwingi” wakati ni hopless kabsa huyu bibi
Mtumishi wa umma nchii wako juu ya sheria
 
Back
Top Bottom