Mfumo wa kubaini madereva wanaochati, kuongea na simu waingia Dar

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Katika kupunguza ajali za barabarani zianazotokana na madereva wanaoendesha vyombo vya moto nchini, Kampuni ya Cogsnet Technologies imekuja na teknolojia mpya ya kufunga mfumo wa kielectroniki utakaokuwa unarekodi na kupiga picha makosa yote yanayofanywa na madereva wa magari wanapokuwa barabarani.

Teknolojia hiyo, ambayo ni mpya nchini itakuwa na uwezo wa kurekodi na kupiga picha gari zaidi ya 10 zikiwa barabarani kwa wakati mmoja, pia itakuwezo wa kupiga picha dereva anayeongea na simu au anayechati wakati akiwa anaendesha gari barabarani.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Novemba 16, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya biashara kutoka kampuni hiyo, Oscar Kissanga, wakati akitambulisha teknolojia hiyo kwa waandishi wa habari, ambapo amesema teknolojia hiyo imekuja kwa ajili ya kupunguza ajali za barabarani zinazofanywa na madereva wazembe nchini.

"Mfumo huu utachukua makosa yote yanayofanywa na mabasi, magari madogo, bajaji na pikipiki na utakuwa unaweza wa kurekodi magari 2000 kwa saa moja," anabainisha

Amesema teknolojia hiyo iliyopo katika majaribio kwa sasa itashirikiana na jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani na itatumika katika barabara korofi na zile zinazosababisha ajali za mara kwa mara Tanzania bara na Zanzibar na kwa kuanza watazifunga katika barabara ya Morogoro, ufukwe wa Coco, Mikumi, ambapo wanyama wengi wanagongwa na gari wakati wa usiku na mikoa mingine kama Dodoma, Arusha.

"Teknolojia hii unakuja kupunguza ajali nchini kwani tayari nchini kama Rwanda, Burundi, Kenya na Ivory Coast zinatumia teknolojia hii na zimepunguza ajali," amesema Kissanga na kuongeza:

"Jana katika fukwe ya Coco, kwa muda wa dakika 30, tuliweza kurekodi gari 432 zikiwa zimevunja sheria kwa kupita kwa mwendokasi, kulipita gari jingine bila tahadhari na kutanua, sasa kama kwa muda mfupi Hali iko hivi, je siku nzima mfumo huu utarekodi makosa mangapi," amehoji.

"Pia teknolojia hii tulienda kurekodi magari katika barabara ya Morogoro eneo la magari saba, ambapo ndani ya dakika 40, magari 375 yalipigwa picha na mfumo wetu na kurekodiwa kuwa yamevunja sheria ya usalama barabarani kwa kuendeshwa kwa speed na kutanua," amesema.

Akifafanua utendaji kazi wa teknolojia hiyo inayotumia mtambo wa Vitronic Mashine Vision Middle East LLC na namna inavyotunza umeme, amesema kifaa hicho kinatunza umeme kwa siku saba hadi 10 na wapo katika majaribio ya kuonesha jinsi mfumo huo unavyofanya kazi na unavyoweza kutatua migogoro kati ya madereva na matrafiki barabarani.

"Mfumo huo unachukua makosa katika nyanja tatu ambapo kama dereva ataendesha kwa spidi kubwa, atakayapita magari kwenye mataa yanayoonesha rangi nyekundu na dereva akipita kwa kutanua, kifaa hiki kitarekodi na kupiga picha gari husika na Kisha kitatuma taarifa moja kwa moja katika mfumo wa data uliounganishwa na jeshi la Polis," anafafanua

"Hapa makosa hayo yote yatakuwa captured na huu mfumo na itakuwa inawasiliana na data centre moja kwa moja kwa ajili ya kutoa taarifa ya makosa ya usalama barabarani na dereva wa gari husika atapelekewa ujumbe mfupi utakaomuonyesha kuwa ametenda kosa na anatakiwa kulipa faini," amesema Kisanga

Amesema mfumo huo pia utakuwa umeunganisha na Leseni za madereva na mamba za vitambulisho vya Taifa (NIDA) na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ili kumbaini mtu aliyefanya kosa barabarani kwa kuonesha muda na eneo ambalo dereva amefanya kosa lake.

Ametolewa mfano kwa madereva wanaotembea usiku ambao hupita kwenye taa nyekundu bila tahadhari, hivyo kupitia mfumo huo sasa utawabaini na kuwakatia tiketi ya kosa lake na kutakiwa kulipia faini.

Amesema kuwa Jeshi la polisi usalama barabarani watatakiwa kwenda kwenye kituo cha taarifa ili waweze kuwabaini wale ambao wamepigwa faini na hawajalipia kulingana na sheria za jeshi la polisi usalama barabarani.

Amebainisha mfumo huo utawafunza Watanzania kuwa na nidhamu barabarani kwani nchi nyingi duniani zimefanikiwa kwa kutumia mfumo huo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Uperesheni usalama barabarani Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Adam Maro amesema teknolojia hiyo imechelewa kuja nchini ndio maana serikali inaharaka kufanya utafiti wa kuweza kupata mfumo utakaosaidia Kudhibiti ajali za barabarani

ACP Maro amesema katika majaribio yaliyofanyika jana ufukwe wa Coco amasema kuwa makosa yaliyopatikana ni makosa zaidi ya 417 ambayo ni changamoto kukamatwa na Trafiki wa Usalama barabarani kwa macho ya kawaida.

"Tunaamini hii ni mwarobaini kabisa kwa sababu magari yameongezeka, unakuta dereva amelikurupusha gari kama amekatwa kichwa haangalii kama kunawatumiaji wengine wa barabara kwa hiyo mwarobaini wao ndio huu hapa," amesema Maro

Amesema anaamini kuwa watalazimika kubadilika na ile ya kusema, "askari alinipiga tochi amenionea mfumo huo hautamwonea mtu kwa sababu ikishasetiwa basi kinachokuwa kinasomeka hapo ndio ushahidi ambao unaweza kupelekwa hata mahakamani."

Vilevile amesema mfumo huo unaweza kupambana na majambazi ambao wanapora simu au mkoba karibu na mataa barabarani kwani utakuwa unarekodi na kupiga picha.

Ashura Kipepo yeye ni dereva anasema kuwepo kwa teknolojia hiyo kutasaidia kupambana na ajali zinazozuilika, ususani barabara kuu.

MWANANCHI
 
Ulaya hukuti traffic road. Mie Naona wangeunganisha na akaunti ya boss ama dereva iwe inafanya automatic bank transfer yeye anapata ujumbe kwa sms kuwa ,this amount is deducted because of this and this at that time Basi. Akibisha ndio anaenda. It itusaidie kutatua changamoto.spidi Ni 120kmph wewe tembea 110 uone Moto wake
 
kamradi kapya kaingizwa kimkakati. wote mashahidi mataa buguruni gari zinaruhusiwa taa nyekundu zkiwa zinawaka na zinastopishwa kukiwa na taa za kijani
 
Sasa buku buku tunazotoa sisi madereva wa daladala haka ka mashine katazipokea au ndio kila kosa cheti 30k mtatufirisi jamani.
 
Wale wanao azima gari inapigwa faini hawamwambii mmiliki,itakula kwao hii,maana mwenye gari chap itaingia notification
 
Technologia kwenye nchi ambayo miundombinu ni hafif is just a waste...

Mwanya mwingine tu wa ulaj Rushwa hapo... vijana wanapambana nao wapate pesa za ku download
 
Back
Top Bottom