DC Kilosa aagiza polisi kuwachukulia hatua kali madereva wa IT wanaobeba abiria

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,375
8,115
Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Alhaji Majid Mwanga ameliagiza jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoani humo kuweka utaratibu wa kuyakagua magari yanayosafirishwa kwenda nje ya nchi maarifu kama IT na kuwachukulia hatua madereva wanaobeba abiria katika magari hayo.

Mwanga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, ametoa agizo hílo wakati akitoa salamu za rambirambi kwa ndugu wa marehemu watano waliofariki katika ajali baada ya gari dogo la IT kugonganga na gari lori eneo la Iyovi wilaya ya Kilosa katika barabara ya Morogoro - Iringa.

Amesema ajali hiyo ni mbaya na imeleta simanzi kwa familia na jamii kwa ujumla kwa kuwa miongoni mwa waliofariki ni pamoja na wanandoa ambao walikuwa wakielekea kwao jijini Mbeya.

“Hizi gari za IT zinasafirishwa kutoka bandarini kwenda nje ya nchi, hivyo zinapaswa kuwa na dereva tu na sio kubeba abiria, lazima tusimamie sheria,” amesema Mwanga.

Wakati huohuo, mkuu huyo wa wilaya amewataka madereva kuchukua tahadhari hasa wanapofika katika eneo la Iyovi ambalo limekuwa hatarishi na limekuwa na ajali za mara kwa mara zinazosababisha vifo na majeruhi.

“Lile eneo la Iyovi lina milima, miteremko na kona kali, taarifa nilizopata yule dereva alikuwa kwenye mwendo mkali na alikuwa akiyapita magari mengine bila tahadhari na ndipo akaenda kugonga lori, nitoe rai kwa madereva wengine wanapofika katika eneo lile lazima wachukukue tahadhari,” amesema Mwanga.

Kwa upande wa mabasi, amewataka abiria kukemea tabia na uzembe unaofanywa na madereva wanapokuwa safarini ikiwemo mwendokasi, kupita magari mengine bila tahadhari, kuongea na simu ama kujaza abiria kuliko uwezo wa mabasi hayo.

Mmoja wa madereva anayesafiri mara kwa mara, Gilbert Selemani amesema ipo haja kwa Serikali kupanua barabara katika eneo la Iyovi kwa kuwa eneo hilo ili kuweza kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.

MWANANCHI
 
Daah sema naona ajali nyingi ni za wanafamilia sijajua hapo ingetumika njia gani kupunguza hilo Janga kwa kweli maana watu wakinunua gari tuu wanadhani wanaweza kuendesha kufika Sumbawanga kumbe kununua ni ishu ingine na kuendesha ni ishu ingine kabisaa tunapoteza sana ndugu huko kuliko hata hizo IT...
 
Hili taifa huwa linaendeshwa kishamba sana, yani huwa wanasubiri tukio litokee ndo wanajifanya kutoa matamko halafu baada ya muda mambo ya hovyo yanaendelea kama kawaida.

Kama taifa bado tuna safari ndefu sana ya kufikia hadhi ya maisha anayositahili kuishi mtu mwenye akili timamu.
 
Iyovi inawezekana ndio kipande cha barabara hatari kabisa nchi hii... spidi kali, kona kali, miteremko na miinuko, hakuna matuta, hakuna askari
 
Back
Top Bottom