Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

crdb wamemkana Emanuel, my classmet pale bush sek , mwamba alikuwa ni mkimya hata hawez kuongea na mtu.
Alishapata ujanja wa kuongea hadi kutukana.

Usiombe likukute. Hii familia inahitaji faraja siyo wakat wa kushangilia matatizo ya mtu. Kuna Leo kwake kesho kwakoView attachment 2825932

Sorry familia yao inahitaji faraja? Kwa uzembe wa mtoto wao?
Only in bongo ukifanya uzembe unafarijiwa
Sisi ndio. Tunakuza hizi tabia
 
Nawewe unaamini Mbowe ampige risasi Lissu,halafu aondoe kamera za eneo la tukio,serikali ishindwe kumfanya chochote,we ni mzima sehemu ya juu ya shingo?

Au wewe ni sample ya wajinga,nikimaanisha wasiojua jambo flani?

Pole sana kama unaamini ulichokiandika,itabidi uje uhadithie baadhi ya watoto wako,tukio lile,na bilashaka wengine watakuuliza kua Mbowe ni nani hadi serikali ilishindwa kumshughulikia,utawajibu kulingana na uelewa wako muda huo unaulizwa.

Mi siyo mfuasi wa chama chochote kile,ila huwezi kuniambia ulichoandika nikakubali.
 
Yaani AIBU tupu. Emmanuel na dadake sijui ni Ma Graduate wa wapi. Wamekalia majungu na ushirikina. Mganga kamuambia kuna Vijana wawili wametumwa na mbaya wako kuja kuvuruga biashara yako kisha kukuua wewe mwenyewe. Kusikia tu hivyo kamuagiza Dereva wake kuwasha gari na Kumuambia twende nyumbani mara moja. Alipofika akaenda kuwatendea Vijana wale alichowatendea bila hata kuzungumza nao.
Product za jalalani yudizimu na yudomu kwa machakaramu hizo
 
ameharibu zaidi. na pale anasema aachie wachagga wasambaze ndio ameonyesha ukabila na ujinga mkubwa sana.
Yeye anaamini wanaosambaza ni vijana wa Mbowe,kisa dada yake alikua CHADEMA kabla ya kujiunga na CCM,asijue kua kuna wadau wanataka kutumia mwanya huo kummaliza dadaake ili jimboni wateleze kiulaini,hasahasa kipindi hiki tunaporlekea kwenye uchaguzi.Asikariri.Hajui kuna watu wanakitaka hilo jimbo pia...?
Atulie huyo kijana.
 
View attachment 2825594
EMMANUEL GEKUL ambaye ni mdogo wake mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul akimtishia kumuua kwa kumkata kichwa na kumpiga risasi PAULINA SLAA NARSIS mkazi wa Babati Mjini akimtuhumu kusambaza video za Hashimu Ally.

HASHIMU ameeleza jinsi alivyotekwa, kuteswa akiwa ameshikiwa bastola na kuwekewa chupa sehemu yake ya haja kubwa kwa amri ya Pauline Gekul, akiwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria. Wakazi wa Babati Mjini walichukizwa na kitendo hicho, wengine wakaamua kusambaza taarifa ile WhatsApp.

EMMANUEL GEKUL anasikika katika video hiyo yenye sauti akimchimba mkwara mzito na kumueleza PAULINA SLAA NARSIS atamkata kichwa na kumpiga risasi kwa kusambaza video hizo za Hashimu. Gekul ametukana matusi mengi ya nguoni. Gekul anatamba kwamba anaweza kumuua na Babati ikatulia.

PAULINE na EMMNAUEL wanapata kiburi kwa nani? RPC Manyara upo? RCO upo? Raia wa Babati anatishiwa maisha yake kwa sababu ya kusambaza taarifa za UOVU wa PAULINE GEKUL? Familia ya GEKUL imelimeza jeshi la polisi Manyara na Babati wanaitawala kifalme? Tunataka EMMANUEL anachukuliwa hatua za kisheria iwe fundisho.

PAULINA SLAA NARSIS ametoa taarifa za kutishiwa kuuwawa kwa kuchinjwa na kupigwa risasi na EMMANUEL GEKUL, lakini hadi sasa hakuna lolote ambalo linaendelea. RPC unajua vizuri hili suala. EMMANUEL GEKUL anasema jeshi la polisi Manyara kwake siyo lolote na haogopi. Je, ni kweli familia ya GEKUL imelishika jeshi la polisi Manyara?

IGP, tunataka jeshi la polisi Manyara na Babati, lichunguzwe na ikibainika kuna watu wanakula njama za kutenda uhalifu kwa kushirikiana na familia ya GEKUL, wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria. Hatuwezi kuwa na watu katika utumishi wa jeshi la polisi wanaoshirikiana na wahalifu kutenda UHALIFU wa kutisha kwa binadamu wenzao.
Paulina ni nani?

Ni Mwandishi wa Habari? Ni mwanaharakati?

Salute kwake🙏
 
Hicho kijamaa ndio kinasema kinaweza kata kichwa mtu ?

Mbona hakina ubavu huo, mwisho hapo kinabadili tu upepo kuwa akikutana nae atamkata vibao.

Hakuna mtu atapanga amkate mtu kichwa halafu aseme, hiyo ilikuwa hasira tu katika mazungumzo.

Yawezekana hata kuchinja kuku tu kwa kisu hajawahi.
 
Back
Top Bottom