Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
EMMANUEL GEKUL ambaye ni mdogo wake mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul akimtishia kumuua kwa kumkata kichwa na kumpiga risasi PAULINA SLAA NARSIS mkazi wa Babati Mjini akimtuhumu kusambaza video za Hashimu Ally.

HASHIMU ameeleza jinsi alivyotekwa, kuteswa akiwa ameshikiwa bastola na kuwekewa chupa sehemu yake ya haja kubwa kwa amri ya Pauline Gekul, akiwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria. Wakazi wa Babati Mjini walichukizwa na kitendo hicho, wengine wakaamua kusambaza taarifa ile WhatsApp.

EMMANUEL GEKUL anasikika katika video hiyo yenye sauti akimchimba mkwara mzito na kumueleza PAULINA SLAA NARSIS atamkata kichwa na kumpiga risasi kwa kusambaza video hizo za Hashimu. Gekul ametukana matusi mengi ya nguoni. Gekul anatamba kwamba anaweza kumuua na Babati ikatulia.

PAULINE na EMMNAUEL wanapata kiburi kwa nani? RPC Manyara upo? RCO upo? Raia wa Babati anatishiwa maisha yake kwa sababu ya kusambaza taarifa za UOVU wa PAULINE GEKUL? Familia ya GEKUL imelimeza jeshi la polisi Manyara na Babati wanaitawala kifalme? Tunataka EMMANUEL anachukuliwa hatua za kisheria iwe fundisho.

PAULINA SLAA NARSIS ametoa taarifa za kutishiwa kuuwawa kwa kuchinjwa na kupigwa risasi na EMMANUEL GEKUL, lakini hadi sasa hakuna lolote ambalo linaendelea. RPC unajua vizuri hili suala. EMMANUEL GEKUL anasema jeshi la polisi Manyara kwake siyo lolote na haogopi. Je, ni kweli familia ya GEKUL imelishika jeshi la polisi Manyara?

IGP, tunataka jeshi la polisi Manyara na Babati, lichunguzwe na ikibainika kuna watu wanakula njama za kutenda uhalifu kwa kushirikiana na familia ya GEKUL, wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria. Hatuwezi kuwa na watu katika utumishi wa jeshi la polisi wanaoshirikiana na wahalifu kutenda UHALIFU wa kutisha kwa binadamu wenzao.

Pia soma:
Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto
Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023
 
Aisee anakata vichwa

OIG.bK3AneyG.c.jpeg
 
Back
Top Bottom