SoC01 Athari za mfumo wa elimu na ongezeko la wasomi wasio na ajira, nini kifanyike

Stories of Change - 2021 Competition

MRAMIRA

New Member
Aug 6, 2021
4
4
UTANGULIZI
Kwa muda mrefu tumekuwa tunajiuliza nini hasa muarobaini wa ajira kwa wahitimu nchini? Kwanini wasomi hawaajiriwi au kuajirika? Upatikanaji wa ajira ni suala mtambuka ambalo watanzania wanajiuliza bila kupata majibu ya maswali haya:
  • Je suala ni wasomi wenyewe
  • je ni ukosefu wa stadi za maisha na stad i za ujasiriamali kwa Wahitimu!
  • Je mfumo wetu wa elimu umejikita kwenye elimu rasmi zaidi (formal educations) kuliko kuwekeza kwenye ujuzi wa mtu mmoja mmoja? (Livelihood skills).
  • Taasisi za elimu zikiwemo zile za elimu ya Juu, je kozi zinazotolewa zinaendana na mahitaji ya soko na kiuchumi?
Ni ukweli usiopingika kwamba suala la upatikanaji wa ajira kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla limekua changamoto. Afrika inakadiriwa kuwa na Idadi kubwa ya vijana ambao hawana ajira. Kutokana na [1]sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 asilimia 77% ya watu Tanzania ni vijana chini ya umri wa miaka 35
Makala hii inaangazia, Nafasi ya mfumo wa Elimu na athari zake kwa wahitimu, soko la ajira na uchumi kwa ujumla wake. Ni kwa namna wasomi wanaweza kujengewa uwezo kutumia taaluma zao na vipawa vyao katika kujikwamua kiuchumi. Namna taasisi za kifedha zinavyoweza kuwasaidia wasomi kujikwamua kiuchumi,
Majadiliano haya yanaangazia maeneo yafuatayo

ELIMU
Baada ya Nchi yetu kupata Uhuru Kampeni na mabadiliko mbalimbali yalifanyika ili kuondoa adui ujinga kama ilivyokua kampeni ya Aliyekua Raisi wa Tanzania Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere. Tunapongeza jitihada za awamu zote sita katika mabadiliko ya elimu ambayo yameongeza idadi ya wanaojiunga na elimu ya msingi Pamoja na sekondari.

Vijana wengi wamejikuta kwenye sintofahamu mara baada ya kuhitimu elimu ya vyuo vikuu wengi wakiamini elimu wanayopata haiwasaidii kujikwamua kiuchumi. Wengi wanalaumu wanasoma vitu vingi ambavyo ni nadharia kuliko uhalisia na haviwapi fursa ya kujikwamua kiuchumi.

1. Ukosefu wa mafunzo ya vitendo yenye uhalisia kwa baadhi ya tahasusi/kada
Moja ya maeneo yanayoweza kumjengea mwanafunzi ueledi na maarifa ni mafunzo kwa vitendo, hata hivyo mkazo mkubwa umebaki kwenye kada chache hasa, kwenye kada za afya, kilimo, elimu, huku kukiwa na Uhusiano mdogo wa kile walichosoma na kile wanachofanyia mafunzo kwa vitendo.

2. Ukosefu wa Ushauri kwenye uchaguzi wa kozi za kujiunga na vyuo

Ni jambo lililo wazi kwamba wanafunzi wengi wamekua wakiingia kwenye kozi za vyuo bila kufahamu kozi inahusiana na nini, na nini matokeo ya chaguzi zake baada ya kumaliza. Wengi ya wasomi wanatoka katika familia ambazo aidha yeye ndo msomi kwenye familia, hivyo kupitia muongozo wa chuo pekee hautoshi kumsaidia kujua ni kozi gani ambayo kulingana na hali ya Uchumi angepaswa kusomea.

3. Vyuo kuwa na kozi nyingi bila kutathmini uhitaji wake kwenye soko .

Vyuo vingi vimekua na kozi nyingi ambazo hazi akisi uhalisia wa hali ya Uchumi nchini, hii imepelekea wanafunzi kutumbukia kwenye sintofahamu ambayo huwa majuto baada ya kuhitimu . Vyuo vimefanya kozi kama mtaji wa kujipatia wanafunzi. Hili limepelekea kuwa na Wasomi wengi wenye kozi zenye Uwiano unaofanana jambo ambalo linatengeneza wasomi wengi ambao hawana ajira.

Ili tuweze kupunguza changamoto hizi za ajira kwa wasomi/wahitimu, mambo kadha yanatakiwa kuangaliwa.

1. Kufikiria upya Mfumo wa Elimu
Watunga sera za elimu wanapaswa kufikiria upya mfumo wa elimu nchini kwani ndio nguzo kuu kwenye ukombozi wa mwananchi.
  • Kuwa na mitaala inayochochea ubunifu. Mitaala ilenge kwenye mafunzo kwa vitendo Zaidi kuanzia elimu ya Msingi. Mitaala mingi imekua katika mfumo wa kinadharia Zaidi hivyo kumfanya mwanafunzi kutokua na ueledi. Mafunzo ya stadi za Maisha na stadi za ujasriamali ziwe nguzo kuu katika hatua za awali kabisa. Mahitaji yanabadilika siku hadi siku hivyo mitaala iendane na mabadiliko. Tupo katika Zama za sayansi na teknlojia ila maudhui ya mitaala shule za msingi hayaendani na mabadiliko haya.
  • Je kuna haja ya kuwa na kozi nyingi vyuoni ili hali hakuna soko kwenye uchumi.
Vyuo vifanye tathmini juu ya kozi kulingana na mahitaji yake kwenye soko la ajira. Kuwa na kozi nyingi bila uhitaji wake kwenye uchumi ni kupoteza muda wa wasomi kukaa muda mrefu darasani ili hali anachosoma hakitakua na soko.
  • Je kuna haja ya mwanafunzi kukaa darasani karibu miaka 16 ili aje kukaa mtaani miaka 10 akitafuta ajira? Muda mwingi darasani uendane sawa sawa na stadi wezeshi zitakazomwezesha kijana kujikwamua kiuchumi. Mfumo unamweka mwanafunzi darasani kwenye elimu rasmi kwa muda mrefu, lazima kurejelea maudhui ya elimu ili yaendane na muda anaokaa mwanafunzi darasani. Maudhui yalenge katika kumwezesha mwanafunzi kupambana na changamoto za mfumo wa Maisha baada ya Kuhitimu
    • Mkopo wa elimu utolewe kutokana na wazo bunifu la mwanafunzi.
    Katika kuimarisha namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha, mkopo wa elimu ya juu utolewe kutokana na wahitimu kuwasilisha wazo Fulani ambalo litamuingiza kwenye dhana ya kuthamini kile wanachopokea. Kigezo kiwe Mf; Mwanachuo aandike wazo la mabadiliko kwenye jamii yake ambalo ndilo litakalompa mkopo. Mkopo utolewe kutokana na ushindani wa kimawazo.

    Kubadilisha fikra na mitizamo kuhusu elimu na kuajiriwa. Tumeshuhudia ongezeko la wasomi wasio na ajira katika nchi yetu, hii inatokana na mfumo ulivyoaminisha wasomi. Mfumo uliandaa wasomi ili waje kuajiriwa na si Vinginevyo. Ni wakati sasa tukafanya kampeni ya kuhamasisha kujiajiri ili wanafunzi waweze kuwa huru kutumia karama na vipawa vyao kujikwamua kiuchumi. Wazazi hawakuamini katika vipawa hivyo mitizamo yao ilijikita katika Imani ili “ ufanikiwe lazima uingie darasani au ufike chuo kikuu” kitu ambacho hakina ukweli. Lazima tubadilishe imani na mitazamo kuwa mtu anaweza kufanikiwa bila kuwa na elimu ya chuo kikuu. Wafanyabiashara wengi hawajawah kufika chuo kikuu. Ni wakati wa kubadilisha fikra na mitizamo kuhusu elimu na kuajiriwa.
  • Elimu iwe na sera na mifumo ambayo ni endelevu (consistency) Licha ya kwamba ni kweli mfumo wa elimu unapaswa kubadilika kutokana na mazingira na mahitaji ya kiuchumi na kisiasa, lakini bado tunapaswa kuwa na sera za elimu ambazo ni endelevu ili kuupa mfumo nafasi ya kuleta mabadilko tarajiwa kwenye mfumo mzima wa elimu. Tumekua na mabadilko chungu nzima kwenye elimu, elimu ya kujitegemea, UPE, matokeo makubwa sasa, mabadiliko kwenye madaraja ya ufaulu, Mf: grade, GPA, na distinctions). Tutengeneze mfumo wetu utakaotokana na changamoto zetu na sio kuchukua mifumo kutoka katika mataifa mengine yenye mahitaji ya kiuchumi na kisiasa tofauti na yetu.
    • Elimu isitumike kama mtaji wa kisiasa.Katika nchi za Kiafrika Elimu imekua daraja ambalo wanasiasa wanalitumia kwa ajili ya kupitisha sera na agenda zao za kisiasa. Kutokana na hili elimu yetu imetumbukia katika mkumbo wa kisiasa na kuleta madhara mengi kwenye mfumo mzima wa elimu.
    • Elimu bure iwe kwa watanzania wa kipato cha chini tu.. Elimu bure itolewe kwa watanzania wasio na uwezo hasa wale wa kipato cha chini. Tathmini ifanyike kufahamu watanzania wangapi wanaweza kuwa kwenye kundi la elimu bure. Hili linaweza kufanyika kupitia serikali za mitaa ambao ndio wapo karibu na wananchi. Hii itapunguza gharama za uendeshaji na fedha zitumike kwenye maeneo mengine ya Elimu.

    2. Kuwekeza Katika kujiajiri kuliko kuajiriwaKujiajiri iwe kauli mbiu kuhakikisha wahitimu wanakua na mchango kwenye jamii zao. Dhana ya kuajiajiri iwekewe msisitizo kama ifuatavyo:
    • Msisitizo uwe kwenye vipaji na uwezo binafsi
    • Mafunzo ya stadi za Maisha na stadi za ujasiriamali yafundishwe shuleni
    • Vijana wajengewe uwezo kuanzia sekondari juu ya mikopo inayotolewa na Halmashauri inavyoweza kuwanufaisha
    • Wahitimu wapatiwe mikopo ya Vikundi baada ya Kuhitimu vyuo na wajengewe uwezo wakiwa vyuoni.
    • Serikali na vyuo vitoe fedha kwa ajili ya kudhamini na kufadhili mawazo ya kibiashara yanayoweza kuibuliwa na wasomi kwenye vyuo vyao.(mashindano ya mawazo
    • Kuanzisha Elimu maalum ya Ufundi ambayo wahitimu wa sekondari watajiunga kabla ya kwenda vyuo au kidato cha tano na sita.
    3. Nafasi ya Taasisi za kifedha katika kuwakwamua wahitimu kiuchumi
    • Benki za Serikali na benki binafsi ziandae mfumo Rafiki kwa ajili ya kuwawezesha wahitimu kupata mikopo kwa njia rahisi. Ni rahisi kupata mkop wa chuo kikuu kuliko mkopo wa Biashara. Njia za kupata Mkopo wa elimu ziwe sawa na Kupata mkopo wa kujiajiri.
    • Vigezo na masharti nafuu kwa wahitimu
    • Ianzishwe Benki ya uwekezaji ya vijana inayoshughulikia masuala ya vijana na ajira nchini
    • Taasisi za kifedha kufanya tathmini ya maeneo ambayo wanaweza kutoa mikopo kwa wahitimu/wasomi.
    • Benki zitoe mitaji kwa mawazo bunifu yanayoibuliwa na Vijana vyuoni Mf vyuo vya VETA)

    Tukapowekeza katika kujiajiri katika Hatua za awali hasa katika mfumo wa elimu si tu tutapunguza ukosefu wa jira bali tutachochochea ukuaji wa uchumi.
Mwisho!

[1] Sensa ya watu na Makazi 2012
 
Serikali inapaswa kuangalia sana soko la ajira linataka nini kwasababu kwa mfano utakuta serikali kwa mwaka mmoja inachukua intake ya waalimu vyuoni ×2 ya mahitaji ya waalimu mashuleni alafu wanachukua mwaka huu mwakan na kuendelea mwisho wa siku unapata wasomi wengi mtaani alafu field zao zimejaa
Hivyo basi serikali inapaswa ijenge wasomi ambao wanaweza ku deal na maisha ya kitengo wanachosomea na pia elimu ya ujasiriamali na biashara
 
Karibuni kwa Maoni! Maoni yako ni Muhimu
 
Kabisa! Naungana na wewe kwenye hili, kila udahili uendane na data, intake hii tuna hitaji watu kadhaa kweny kada hii na hii,
 
Hakika ni kweli
 
Mfumo wa elimu umekua changamoto katika kutatua suala la ajira nchini, ukweli ni kwamba kujiajiri sio kauli mbiu ya kitaifa hivyo mfumo unawaandaa wasomi kula chakula na sio namna ya kula chakula
 
Back
Top Bottom