mfumo wa elimu yetu

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,524
14,395
Elimu ni msigi wa mandeleo endelevu, Hata hivyo mifumo duni ya elimu inashindwa kutoa maarifa na stadi zinazohitajika kwa ajira ya soko la kazi na kuboresha ubora wa maisha. Elimu yetu imejikia katika ajira na si kujitegemea. Elimu yetu imetufumba katika kuwa na fikra tunduizi (Crictical thinking) bali kuweza kujibu maswali. Ni elimu ya kujificha kwenye kichaka cha ajira.

VIJANA wengi wanaosoma kwa bidii ili waweze kufaulu mtihani na si kujua mambo. Kuna watu wengi walioelimika lakini pia kuna kundi ndani yake ambalo halina akili pamoja na kusoma kwao.

Wingi wa Vijana wasio na ajira na ukosefu wa fursa za Ujasiriamali ni changamoto kubwa inayosababisha kukosa motisha na kuongeza umasikini.

Vijana ndio nguvu kazi ya UTAJIRI WA TAIFA LOLOTE, iwapo vijana watageuka kuwa watafutaji wa mlo wa siku basi suala la maendeleo tulisahau.

Kuna Vijana wanaoamini katika ajira na bado ndoto zao zisizokamilika zipo huko. Ajira ndio kila kitu kwa kuwa kuna kipato cha uhakika, Lakini suala la kujiajiri linataka mambo mengi ikiwamo ELIMU na MTAJI na sisi ni MASIKINI tutasubiri sana.
 
Asante kwa Bandiko Mkuu.

VYETI VIWE MKOMBOZI KWA JAMII NA SIO MAKARATASI

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Vijana wengi waliosoma wakotayari kujiajiri shida ni mitaji
Ukitaka kuhakikisha hili vijana wengi wakishaajiriwa wanawekeza kwenye biashara mbalimbali na kuajiri wengine waliosoma na wasiosoma
 
Vijana wengi waliosoma wakotayari kujiajiri shida ni mitaji
Ukitaka kuhakikisha hili vijana wengi wakishaajiriwa wanawekeza kwenye biashara mbalimbali na kuajiri wengine waliosoma na wasiosoma
Suala la kujiajiri linataka mambo mengi ikiwamo ELIMU na MTAJI na sisi ni MASIKINI tutasubiri sana.
 
Tazania kwenye utoaji wa elimu bora tumefeli,iliyopo ni outdated na kuendelea kuikumbatia ni kukubali kuendeleza ujinga.Kuna haja ya kukaa kama taifa kulijadili swala hili huku tukishirikisha wataalamu wa nje kutoka nchi zilizofanikiwa kielimu ili kuja na mwafaka wa elimu bora inayoendana na mazingira ya kisasa.
 
Back
Top Bottom