Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,319
- 3,268
Watabisha sana lakini kauli ya waziri wa elimu kuhusu ajira za walimu ni kauli za udhalilishaji wa waalimu na Maprofesa wa vyuo husika!
Kama mitaala ya vyuo vya walimu inasimamiwa na wizara ya elimu! Kama vyuo vyetu vina ubora unaokidhi vigezo! Kwanini waziri anawataka walimu wafanye mitihani Tena kabla ya ajira? Mbona madaktari na wauguzi wasifanyiwe mitihani upya?
Ni kwa sababu waziri wa elimu ana hisi vyuo vyetu ni takataka! Na wahitimu wa vyuo vyenyewe ni mapompopo! Fikiria kwamba zaidi ya waalimu laki mbili Hawana ajira na viwango vyao vya elimu vinatofautiana hiyo mitihani itazingatia muda wao waliokaa bila ajira?
Hiyo gharama ya kuisimamia hiyo mitihani sio matumizi mabaya ya fedha? Kama vyuo vyetu vimekosa ubora basi tuambiwe ili na sisi wazazi tusipeleke watoto wetu kwenye vyuo ambavyo serikali Haina Imani navyo.
Kama serikali imekosa Imani na vyuo vyetu, tafadhali wizara itoe tamko rasmi tuvisusie hivyo vyuo havitufai kabisa ! Watoto wetu kwa sasa Wana stress kwa kuwa hawajui ninini kitatokea!
NB: Waziri wa Elimu kabla hujafanya maamuzi shirikisha wadau! Usiamue mambo peke yako kama Mtemi Mirambo wa Tabora.