ATCL: Another Richmond!

ATCL: Another Richmond!

yeah.. iko njiani yaja lakini waseme tu kwa furaha.. wengine tunaangalia kwa macho ya karibu kweli...
 
..ngoja ije mkuu, wasije kutuambia tu kuwa kuirusha mara moja gharama zake ni bajeti ya wizara tutawafunga lzima wawe wamefanya analysis ya kutosha sio ndio waje kuimaliza kabisa hiyo ATCL...maana wengine hamnazo kabisa sijui hayakusoma uchumi
 
wasije kutuletea vitimbi vya "Community Airline", sasa wafanyakazi wao wanalipwa nusu mshahara! Wakae wakijua biashara ya usafiri na 10% haziendani!! Wasipoua shirika wanaua abiria!!
 
Shukrani,,kwenu Ndugu Watanzania Naitwa Henry Kejo Tofauti Na Wanaoogopa Kutaja Majina Yao..mimi Nikiwa Kama Abiria Wa Airtanzania Hapo Juzi Nikitokea South Africa Nilisikitishwa
Sana Na Uozo Uliotendeka ..kwanza Tulipanda Ndege Ya Makaburu Watupu Pili Tukiwa Tumekaa Ndege Ilikuwa Inanuka Eneo Zima La Abiria Baada Ya Muda Tukauliza....wakasema Subirini Ndege Iondoke Mtajulishwa...wale Wazungu Ni Washenzi Na Mbwa Kabisa...
Nilijiuliza Nini Kimetokea Kabla Sijapata Jibu Tukaambiwa Abiria Wote Chukua Kilicho Cheni Mrejee Mlipotoka..hakika Sikuamini Na Kila Unaemuuliza Kakaa Kimya...mimi Mwanahalisi Mtanzania Halisi Sikupenda Kukaa Kimya Nikauliza Kila Kona Ndipo Niliyoyapata Haya

Hiyo Ndege Imekodishwa Na Baadhi Ya Members Wa Management Kwa Wiki Tatu Sasa Iko Uko.kwa Mslahi Yao Binafsi Na Wala Si Ya Kampuni Kama Wengi Walivyofikiri.dar..na Habari Za Uhakika Ni Kwamba Ndege Hii Toka Imeokuja Imekuwa Ikiondoka Muda Wa Saa Sabananusu Mpaka Saa Nane..na Hizi Ni Hujuma Za Zilizozahiri...kwamba Kuna Mambo Mengi Yanafanyika Ndani Ya Atcl Bila Sisi Kujua Matokeo Yake Tunapata Shida...ndege Hii Imeanza Kunuka Toka Siku Ya Kwanza Na Wakatiwakiambiwa Wahenshimiwa Wa Atcl Wamekuwa Wakikana Mpaka Baadhi Yao Kuja Na Kunusa Harufu....ilyomo Ndani...katika Hili Naomba Huyo Naibu Waziri Wa Miundo Mbinu Badala Ya Kukaa Pale Nbc Club Na Kunywa Na Walevi Wenzake Ajaribu Kufwatilia Nini Kilichomo Atcl....na Nini Cha Kufanya...aiwezekani Mkakodisha Ndege Wiki 3 Inanuka Na Wewe Waziri Na Naibu Waziri Uko Ofisni Unasoma Tu Hizi Taarifa...
Pili Kuwepo Na Uwazi Katika Kukodisha Hizi Ndege Maana Inasemekana Kuna Watu Wachache Wao Wakisikia Mambo Ya Kukodisha Ndege Wako Mstari Wa Mbele Kuangalia Asilimia Kumi Yao..bila Kuangali Ni Ubora Wa Ndege...wakiongozwa Na Muhindi Mmoja Jina Atukuweza Lipata...tungependelea Mhe Makongoro Badala Ya Kukaa Pale Nbc Club Na Kunywa Nenda Ukachungulie Uchafu Uliopo ..kuliko Kuitwa Mlevi Ufanyi Kazi Bora Ujiuzulu.....
Tunawashukuru Baadhi Ya Wafanyakazi Wa Ndege Watanzania Waliopo Siku Hiyo.....kwa Msaada Wao...
Wenu Henry Kejo
Dsm
Tanzania
 
wooooh hongereni good nnews sie precision tushaanza na mwanza na tunaelekea angola na nairobi..nasikia linawasili kesho mchana saa nane bila viti sasa mmeleta kopo linalokuja kulala kweli jamani watanzania mtawaeleza nini ...na zile doller 360,000 mlizokuwa mkitoa zilikwenda wapi..waandishi wa habari mnaombwa mje kuona kilichomo ndani kama mlivyokuja precission ingawa mkaona hatari kutangaza tumeleta ndege shega tunashukuru pesa za wasukuma tushaanza kuzitumia...

hawa wakubwa wao kama ni kweli wana haki ya kuulizwa na kujibu,,na natumaini wataingia kimyakimya.....
 
Waandishi wa habari waende uwanja wa ndege kesho mchana majira ya saa nane hivi. Na watake waoneshwe ndani ya hiyo ndege ambayo "siyo mbovu"...
 
wooooh hongereni good nnews sie precision tushaanza na mwanza na tunaelekea angola na nairobi..nasikia linawasili kesho mchana saa nane bila viti sasa mmeleta kopo linalokuja kulala kweli jamani watanzania mtawaeleza nini ...na zile doller 360,000 mlizokuwa mkitoa zilikwenda wapi..waandishi wa habari mnaombwa mje kuona kilichomo ndani kama mlivyokuja precission ingawa mkaona hatari kutangaza tumeleta ndege shega tunashukuru pesa za wasukuma tushaanza kuzitumia...

hawa wakubwa wao kama ni kweli wana haki ya kuulizwa na kujibu,,na natumaini wataingia kimyakimya.....

Good point na waseme kilichopo humo ndani.
Maana mshahamishia mlio awamu ya TATU kwamba imejaa UFISADI wameleta jet stream kwenye box sasa ivi imelala tu kule terminal two.
Sasa je na nyiyi WAUNGWANA mmejirekebisha au ndio yale yale..........?
 
wooooh hongereni good nnews sie precision tushaanza na mwanza na tunaelekea angola na nairobi..nasikia linawasili kesho mchana saa nane bila viti sasa mmeleta kopo linalokuja kulala kweli jamani watanzania mtawaeleza nini ...na zile doller 360,000 mlizokuwa mkitoa zilikwenda wapi..waandishi wa habari mnaombwa mje kuona kilichomo ndani kama mlivyokuja precission ingawa mkaona hatari kutangaza tumeleta ndege shega tunashukuru pesa za wasukuma tushaanza kuzitumia...

hawa wakubwa wao kama ni kweli wana haki ya kuulizwa na kujibu,,na natumaini wataingia kimyakimya.....

habari ndiyo hiyooooo!
 
Tutumieni mliopata picha ya hilo dege letu
1.JPG
 
na Mobini Sarya

NAIBU Waziri wa Miundombinu, Dk. Makongoro Mahanga, ametaka wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ambao wanavujisha siri za shirika hilo kutafutwa na watakapobainika washughulikiwe mara moja.

Pamoja na kukiri kwamba taarifa hizo ni za kweli, aliwataka wafanyakazi hao kuacha tabia hiyo na kwamba wanapoona kuna tatizo, washirikiane na menejimenti ya ATCL, ili liweze kutafutiwa ufumbuzi.

"Ni lazima tushirikiane na menejimenti, tuwabaini wale wachache wanaoendekeza majungu, ili tuwashughulikie. Hawawezi kuwa na malalamiko halafu wanayapeleka kwenye vyombo vya habari na kwenye mtandao, bila kufuata utaratibu," alisema Dk. Mahanga.

Naibu waziri huyo ametoa kauli hiyo siku moja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kumjia juu kupitia chama chao cha wafanyakazi, baada ya kutoa kauli bungeni wiki iliyopita akiwatuhumu kuwa wambea na wenye majungu.

Dk. Mahanga alikuwa akizungumza jana jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Ndege wa zamani, baada ya kupokea ndege mpya aina ya Airbus A320 iliyokodiwa na ATCL.

Alisema kauli aliyoitoa bungeni ilikuwa inawalenga wafanyakazi wachache wanaotoa siri za kampuni hiyo nje.

Alisema wafanyakazi wengi wa ATCL ni wachapakazi na ndio wamefanikisha ujio wa ndege hiyo, lakini kuna wachache ambao kazi yao ni kutoa nje nyaraka za kampuni kuhusu mabaya yanayotendeka, ili yachapishwe kwenye vyombo vya habari.

"Sikueleweka vizuri nilipotoa kauli ile, lakini nilikuwa naamanisha zile taarifa zinazotolewa kwenye vyombo vya habari...ukiona nyaraka au taarifa zimechapwa kwenye mitandao ya habari utakuta ni kweli zipo ndani ya ATCL, ndiyo maana nasema kuwa wapo wafanyakazi wanaotoa siri nje," alisema Makongoro.

Hata hivyo, aliwapongeza wafanyakazi wa shirika hilo kwa kufanikiwa kuileta ndege hiyo iliyokodiwa kwa dola 37,000 za Marekani kwa mwezi kutoka Kampuni ya WALLIS Trade, kwa mkataba wa miaka sita.

Aidha, alisema huo ni mkakati wa serikali kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inakuwa na ndege nyingi za kujitegemea ambazo zitasaidia kupambana kibiashara kama yalivyo mashirika mengine ya kimataifa.

Hivi karibuni Dk. Mahanga alinukuliwa bungeni akisema kuwa wafanyakazi hao ni waongo, wambea na wanakuza majungu katika sehemu zao za kazi. Kutokana na kauli hiyo, wafanyakazi hao kupitia Chama chao cha wafanyakazi ‘COTWU', walipingna kauli hiyo.

Wafanyakazi hao walieleza kuwa kauli hiyo ya Mahanga imewasikitisha na kuwafadhaisha.

Awali, jana baada ya kuwasili ndege hiyo, Mkurugenzi wa shirika hilo, David Mattaka, alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 150 ni kutekeleza maagizo waliyopewa na serikali ya kuhakikisha wanaimarisha mtandao wa ndani.

Alisema ndege hiyo ipo katika hali nzuri na itaanza safari zake kwenda Afrika Kusini na baadaye wataanza kuitumia kutoka Dar es Salaam hadi Dubai.

"Leo ni siku ya furaha, maana katika anga yetu ndege moja imeongezeka," alisema Mattaka na kuwaomba Watanzania wawe na utamaduni wa kusafiri kwa kutumia ndege za ATCL, ambazo kwa sasa zipo sita, tatu za kukodi na nyingine za kununua

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/2/habari2.php
 
Pamoja na kukiri kwamba taarifa hizo ni za kweli, aliwataka wafanyakazi hao kuacha tabia hiyo na kwamba wanapoona kuna tatizo, washirikiane na menejimenti ya ATCL, ili liweze kutafutiwa ufumbuzi.

"Ni lazima tushirikiane na menejimenti, tuwabaini wale wachache wanaoendekeza majungu, ili tuwashughulikie. Hawawezi kuwa na malalamiko halafu wanayapeleka kwenye vyombo vya habari na kwenye mtandao, bila kufuata utaratibu," alisema Dk. Mahanga

Mahanga, sasa kama unakiri hizi taarifa ni za ukweli kwa nini unasema watu wanamajungu? huoni kuwa wewe ndo kiongozi wa majungu hapa??????
 
Sijui itamchukua muda gani Rais Kikwete kupata viongozi waadilifu na wakweli.
Huyu jamaa anatukuza ufisadi na kamwe hatawanyazisha watanzania wenye kiu ya maendeleo ya nchi yao. Ni fursa ngapi tumewaachia watani zetu wa jadi kuchuma kwa ufisadi wetu?

Ni vema akajipima mwenyewe na ikiwezekana achukue uamzi sahihi kwa manufaa ya taifa. Si miaka ya ubabe hii na wala zama hizo hazitarudi. Sisi bado tuna imani na taifa letu na hatuwezi kuwaacha watu wachache waneemeke huku taifa na watanzaia walio wengi wakifa njaa na kukosa huduma za msingi.

Enyi wafanyakzi watiifu kwa taifa lenu, endeleeni kuwafumua mafisadi ndani ya mashirika yenu na sisi tutawaunga mkono.
 
Watu kama Makongoro ndio wanamuabisha Kikwete hadi basi tu!

Hii ni aibu hata kwa watanzania ambao mtu asiyetujua atadhani wote tuko kama kina Makongoro hawa. Asante tuandamane kwa hii thread.
 
Hivi huyu bwana ni wa wapi..hebu tupate CV yake kwanza...

Anajichanganya kiasi hicho...sasa mwenye kupika jungu ni nani...asema kama taarifa hizo ni za uongo..lakini kama ni za kweli, analalamika nini..au na yeye yupo kwenye 'mfumo' wa ATC?

Au hawezi hata kusoma alama za nyakati?
 
wanandugu kama sijakosea na rekodi yangu iko kwa maandishi huyu bwana mh makongoro akiwa mkuurugenzi wa fedha pale bima motors akaiba na viongozi wenzake wakiua kabisa kile kitengo,,akaja NATIONAL HOUSING akaiba vya kutosha sasa anataka watanzania waone ATCL ikifa..
KWAKO MAKONGORO
HATUTAKUBALI KUONA ATCL IKIFA KWA AJILI YA MANUFAA BINAFSI KAMA ULIVYOUA BAADHI YA MSHIRIKA YA UMA..HATA UKIWA ATC NANIA ASIEKUJUA ULIVYOSHIRIKANA KUIBA NA WENZAKO KWENYE MA RESIT FEKI......NA KUONGEZA BEI ZA VITU ..NA KWA TAARIFA HATUTAKUBALI KUONA WATANZANIA WAKIUA KAMPUNI YAO LABDA TULETEENI WACHINA WAIUE
 
Huyu Mahanga kweli hamnazo! Taarifa kakiri mwenyewe ni za kweli zimetoka ndani ya ATCL halafu anaziita majungu? Yeye anataka wenzie wafanye madudu ya kifisadi huko ATCL halafu wenye access na taarifa hizo wanyamaze tu kwa kisingizio cha "siri za kampuni"? Hawa ndio wanaolea ufisadi!
 
Back
Top Bottom