http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/2/habari2.php
Mod kama ipo sehemu nyingine merge please au delete
Mahanga awatisha wafanyakazi ATCL
na Mobini Sarya
NAIBU Waziri wa Miundombinu, Dk. Makongoro Mahanga, ametaka wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ambao wanavujisha siri za shirika hilo kutafutwa na watakapobainika washughulikiwe mara moja.
Pamoja na kukiri kwamba taarifa hizo ni za kweli, aliwataka wafanyakazi hao kuacha tabia hiyo na kwamba wanapoona kuna tatizo, washirikiane na menejimenti ya ATCL, ili liweze kutafutiwa ufumbuzi.
Ni lazima tushirikiane na menejimenti, tuwabaini wale wachache wanaoendekeza majungu, ili tuwashughulikie. Hawawezi kuwa na malalamiko halafu wanayapeleka kwenye vyombo vya habari na kwenye mtandao, bila kufuata utaratibu, alisema Dk. Mahanga.
Naibu waziri huyo ametoa kauli hiyo siku moja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kumjia juu kupitia chama chao cha wafanyakazi, baada ya kutoa kauli bungeni wiki iliyopita akiwatuhumu kuwa wambea na wenye majungu.
Dk. Mahanga alikuwa akizungumza jana jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Ndege wa zamani, baada ya kupokea ndege mpya aina ya Airbus A320 iliyokodiwa na ATCL.
Alisema kauli aliyoitoa bungeni ilikuwa inawalenga wafanyakazi wachache wanaotoa siri za kampuni hiyo nje.
Alisema wafanyakazi wengi wa ATCL ni wachapakazi na ndio wamefanikisha ujio wa ndege hiyo, lakini kuna wachache ambao kazi yao ni kutoa nje nyaraka za kampuni kuhusu mabaya yanayotendeka, ili yachapishwe kwenye vyombo vya habari.
Sikueleweka vizuri nilipotoa kauli ile, lakini nilikuwa naamanisha zile taarifa zinazotolewa kwenye vyombo vya habari...ukiona nyaraka au taarifa zimechapwa kwenye mitandao ya habari utakuta ni kweli zipo ndani ya ATCL, ndiyo maana nasema kuwa wapo wafanyakazi wanaotoa siri nje, alisema Makongoro.
Hata hivyo, aliwapongeza wafanyakazi wa shirika hilo kwa kufanikiwa kuileta ndege hiyo iliyokodiwa kwa dola 37,000 za Marekani kwa mwezi kutoka Kampuni ya WALLIS Trade, kwa mkataba wa miaka sita.
Aidha, alisema huo ni mkakati wa serikali kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inakuwa na ndege nyingi za kujitegemea ambazo zitasaidia kupambana kibiashara kama yalivyo mashirika mengine ya kimataifa.
Hivi karibuni Dk. Mahanga alinukuliwa bungeni akisema kuwa wafanyakazi hao ni waongo, wambea na wanakuza majungu katika sehemu zao za kazi.
Kutokana na kauli hiyo, wafanyakazi hao kupitia Chama chao cha wafanyakazi COTWU, walipingna kauli hiyo.
Wafanyakazi hao walieleza kuwa kauli hiyo ya Mahanga imewasikitisha na kuwafadhaisha.
Awali, jana baada ya kuwasili ndege hiyo, Mkurugenzi wa shirika hilo, David Mattaka, alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 150 ni kutekeleza maagizo waliyopewa na serikali ya kuhakikisha wanaimarisha mtandao wa ndani.
Alisema ndege hiyo ipo katika hali nzuri na itaanza safari zake kwenda Afrika Kusini na baadaye wataanza kuitumia kutoka Dar es Salaam hadi Dubai.
Leo ni siku ya furaha, maana katika anga yetu ndege moja imeongezeka, alisema Mattaka na kuwaomba Watanzania wawe na utamaduni wa kusafiri kwa kutumia ndege za ATCL, ambazo kwa sasa zipo sita, tatu za kukodi na nyingine za kununua.
juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 33 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Hivi kwanini wanashindwa kuwa straight na Watanzania:?
a. Hii ndege imekodishwa kwa mkataba wa dola milioni 30 kwa miaka mitano (sijui kama wameongeza mmoja)
b. ATC wameshaanza kulipa (siyo "watalipa" kama vyombo vingine vilivyoripoti) Dola 370,000 kwa mwezi. Tayari wamelipa karibu dola milioni mbili.
c. Kwa kucheleweshewa kupewa udhamini wa serikali, walikuwa wanalipa dola 60,000 kwa mwezi hadi karibu mwezi mmoja uliopita kama adhabu.
d. Vyombo vya habari vimesema kuwa ndege imekodishwa toka Ufaransa. Si kweli unless wamebadili mkataba. Mkataba wao unasema kampuni ya Wallis Trading ya Liberia.
e. Kauli ya Mahanga kuwa matengenezo ya huko El Salvador ni ya kawaida ni kuzuga watu. Ndege ilikuwa inafanyiwa matengenezo ya lazima baada ya kuwa na vitu zaidi ya 100 ambavyo ni vibovu.
f. Waandishi waulize, hayo macover ya viti yamesafishwa lini na wapi na kama ATC ina mpango wa kuweka viti vipya.
ATC wawe wa kweli....
na Mwanakijiji, Kijijini - US, - 2.05.08 @ 14:27 | #9637
Huyu Mahanga Makongoro amesahau wakati wa mchakato wa kununua ndege ya rais wananchi walipiga kelele lakini wakaambiwa ndege ni nzuri rais wetu atazurura kila mahali anapotaka bila wasiwasi leo tunaambiwa ndege ni mbovu.waliokuwa wanatetea wamechukuliwa hatua gani.Tuliambiwa pia hakuna wizi wowote BOT leo waliokuwa wanatetea wako wapi,sita shangaa tukaja kuambiwa ndege imeshindwa kuruka kwasababu ni mbovu sijui kama Dr M Mahanga atajisiakiaje au atachukuliwa hatua gani.Mambo ni mengi nchi yetu viongozi hawawajibiki hata kwa kauli zao mbaya.Mahanga atatakiwa kuishi kwa kauli yake asije akawakimbia waandishi wa habari watakapo muuliza au asitafute visingizio vyovyote.
na G KABONDE, ARUSHA,TANZANIA, - 2.05.08 @ 14:33 | #9638
Makongoro Mahanga acha kutisha watu, dunia ya sasa si yakuficha uozo, siri maana yake nini? unajua maana ya siri wewe? Tanzania haitaendelea kama uongozi utakuwa kama huu anaouonyesha mahanga, uozo lazima uanikwe wazi, taarifa unazoona ni za siri siyo siri, na zile unazodhani siyo siri ndiyo siri. Taarifa za siri ni zile zinazowezesha shirika kuendelea lakini taarifa zinazohusiana na kudidimaza shirika siyo siri kwani ufanisi wa shirika utaziumbua! jamani usomi siyo madigree tu lakini vision na moyo wa dhati wa kuwatumikia walalahoi. Ningekuwa mahanga ningewataka wafanyakazi wavujishe taarifa zote ambazo ni vikwazo kwa shirika na uongozi umefumba macho, hiyo ndo njoia pekee ya kuendeleza mashirika yenye ufanisi duni.
na john, Tz, - 2.05.08 @ 14:39 | #9640
Sasa huyu waziri anatka kutuambia kuwa siasa ni kubwa kuliko ukweli halisi nini! maana hata yeye amekili kwamba yote yaliyosemwa yanaukweli, sasa nashindwa kumwelewa pale anaposema kuna watu wanapika majungu, hivi majungu ni kusema ukweli au mtu anaposema kitu kisichokuwa kweli ndo tunasema huyu ni mtu majungu, nadahani hawa wanaotoa habari hizi kweli ndo watanzania wenye uchungu na nchi kuliko hata huyu waziri mwenye kutaka kuficha ukweli. mheshimiwa utawala bora ndo unaondoa majungu la sivyo majungu yataendelea kama kawa, jilekebishe kwanza kabla hujamlekebisha mwenzio.
na yohana, tz, - 2.05.08 @ 15:00 | #9647
Ama kweli mafisadi wanaujasiri wa kifisadi, alijisemea Mwakyembe. Yaani anayetoa siri kwa manufaa ya ATC na watanzania ambao tunalipa kodi inayoishia mikononi mwa wachache ndio anaambiwa ashughulikiwe?
Kwa kauli hii waziri huyu tuanze kufuatilia nyendo zake vizuri. Huyu yupo tayari kwenye list ya mawaziri wasiofaa. Mie nalipa kodi halafu anayeteta kodi yangu ndiyo ashughulikiwe. Wananchi tumshughulikie huyo Mahanga, hafai na hana aibu wala huruma kwa Watanzania.Anaficha ufisadi na Mafisadi.
na Kawala, Ubelgiji, - 2.05.08 @ 15:00 | #9648
NI vizuri kila kitu kiwekwe bayana . hii ni hatari sana maana kama ni ndege mbovu baasi ni lazima kuwa siku moja itauwa watu. hakuna cha kufanya siri kama chombo hicho nyeti cha kusafiria kina husu maisha ya watu. Hii ni demokrasia ya kweli lazima waziri mahanga asitishe watu na badala yake aseme ukweli. Hii ndege ina muda gani tangia itengenezwe na matengenezo yake yametughalimu kiasi gani na kwa nini. Heeshimu wananchi na wao watakuwa watumishi wema!
na david ntali, usa, - 2.05.08 @ 15:15 | #9653
Mahanga zama za siri sirini zilishapitwa na wakati! Wananchi wanayo haki ya kujua kila kinachoendelea ndani ya nchi yao hususan pale ambapo maslahi yao yanachezewa na mafisadi. Naomba wananchi wazalendo waendelee na msimamo huo huo wa kutoa 'siri' kwa manufaa yetu sote katika kufichua ufisadi na maovu meigine yanayotendeka nchini mwetu.
na Madilu, dsm, - 2.05.08 @ 15:37 | #9658
Makongoro Mahanga anajulikana kwa utapeli wake. Kama siyo mfumo mchafu hakupaswa kuwa hata balozi wa nyumba kumi. Jamaa ni tapeli kama Didace Massaburi ambao udaktari wao ni kufoji sawa na Nchimbi. Hawa mbweha wanadhani yao hayajulikani?
na MAGOMA, DAR, - 2.05.08 @ 16:10 | #9674
huyu mahanga ni fisadi namba 12 maana hicho anachokisema hata hakifahamiki..tunakuomba jk huyu awe next waziri kutolewa katika baraza.
na fisadi makongoro mahanga, baghdad, - 2.05.08 @ 16:33 | #9681
Wazalendo hivi cv ya Mahanga ikoje? Nasikia anaitwa Dk. Makongoro Mahanga, Je ni daktari wa mifugo, binadamu au daktari wa falsafa.
Kama ni daktari wa falsafa hajui hata dhana ya utawala bora (good governance) inajumuisha nini. Hajui kama uwazi (transparency) ni kipengele muhimu cha utawala bora? Anataka wazalendo wa ATC wafiche habari za ufisadi? Sasa ni msomi wa chuo gani kama hajui haya mambo madogo?
Wasomi wanasiasa wanatutia aibu, Mahanga hana tofauti na akina Mukandala na Maghembe wanaofurahia kufukuza watoto wanaosoma vyuo vikuu. Wamesoma na kukakariri, masikini hawajaelimika. Hawawezi kutumia elimu yao ya nadharia kwa vitendo. Shame on our professors, and Doctors ambao ni wanasiasa wanatia aibu,. waondoke kwenye siasa, wameshindwa.
na Kawala, Ubelgiji, - 2.05.08 @ 16:36 | #9682
Huyo mahanga anataka mambo yawe siri ili akila cha juu asijulikane.Akumbuke kuwa bila wafanyakazi kufichua jipu linalofichwa na viongozi wao haya mambo yote ya ufisadi yasingejulikana pamoja na kwamba viongozi wote wa juu wanajua kila uozo wa sekta.Rais anawaambia wafanyakazi washirikiane na serikali kufichua mauzauza ya ******* kama huyo Mahanga na yeye anataka watakaofichuwa siri mbovu za viongozi wakamatwe washughulikiwe!!!
Rais atakaa na makanjanja kama Mahanga mpaka lini?Ni mangapi wafanyakazi wamekuwa wakishauri viongozi wao kabla ya kuleta madhara badala yake wao wanaonekana ndio kikwazo wanaishia kufukuzwa kazi au kuhamishwa vituo ili kuficha maovu?
Au Mahanga anataka kufunika ATCL kama alivyofunika lile la TRCL wakati wafanyakazi walishatoa siri kuwa kuna usanii unachezeka lakini yeye na Chenge wakalipiga chenga hadi sasa serikali inalipa garama hizo kubwa kwa uzembe wao .Tena itabidi tumuulize Kikwete anataka kuwalinda hawa akina CHENGE na MAHANGA [miundombinu]hadi waiuze ikulu?
Kwa nini serikali ikakubali kubeba mzigo wa ATCL wakati ule iliposhindwa kupeleka mahujaji lakini ikashindwa kuwawajibisha waliohusika na upuuzi ule?na huko TRCL nako yale yale.Kwanza huyo Mahanga akiwa kama waziri wa miundombinu alitakiwa awe wa kwanza kungamua uozo ule lakini kwa kuwa wanalindana alikaa kimya hadi Pinda alipoamua kuchukua chakula cha watoto wake na kuwapa mbwa[hao wababaishaji wa TRCL]Kwa mtindo huo ieleweke wazi kuwa Rais amezungukwa na mafisadi ambao wanazidi kutafuta njia ya kujipatia chochote kwa kuwaziba midomo wafanyakazi wasitoe siri zao.
na kimalando, tz, - 2.05.08 @ 17:05 | #9687
mimi nahisi mawaziri wote wamekuwa kama mzigo wa **** hawa kwanini jamani hatuwafukuzi hawa wanaleta enzi zile za ujamaa kila kitu kuwa siri?
na king, tz, - 2.05.08 @ 17:23 | #9692
Ashakum si ******!
Dk. Makongoro Mahanga wacha kukurupuka.Ukiona wafanyakazi hawafikishi malalamiko ya yao kwa uongozi walionao usijue hakuna anayeweza kuwasikiliza. Hata kama wewe ni mkali kwa wanao si ajabu wanao wakaeleza shida zao kwa mama yao (mkeo) na kisha mkeo ndipo akwambie wewe! Kwahivyo, haya unayoyasema na iubabe usio na maana, tafuta chanzo caha tatizo na si ajabu ni hao viongozi wa menejimenti unaowakingia kifua, bila shaka kwa masilahi yako na si ya wafanyakazi.
Tafakuri kwa makini, rejea kauli yako na uifanyie kazi kwa makiiini! Utagundua ulikurupuka.
Mtaalamu mmoja wa marekani aliwahi kusema hivi: "The only risk is the risk of thinking too small"
Eee kwaheri!
na Kasigaji, Katoro, - 2.05.08 @ 17:23 | #9693
Hii kauli ya Mhe Naibu Waziri MAHANGA ni kinyume kabisa na maelekeo ya utawala bora ambao Serikali yetu inalenga kuuendeleza.Kwa nini ATC wakatazwe kusema kama wanaona kuna kasoro,eti siri gani ya shirika?
Hakuna siri hapo kwa vile hili ni shirika la umma,wananchi tuna haki ya kujua nyendo za humo ATC.
Je huo mkakati wa kununua ndege na kulipa 37 000dollars @ mwezi ulijadiliwa kweli na Waziri /Naibu kw pamoja na wafanyakazi ATC nk nk?Sidhani,ndio maana kuna malumbano hayo.Hata hivyo hii gharama sio kubwa,kwa nini Waziri usingepanga kununua dege kabisa.Tanzania tena kama enzi za ile Alliance air.Na usalama wa hiyo ndege ukoje --- eti toka Liberia;na matengenezo EL alvador!Tusije kodisha dege bomu tena.flying ...fin).Isije ikiwa yale kati ya madege yaliyopigwa marufuku Europe kwa sababu ubovu!!Mhariri,waambie ATC wawape mkataba huo ili uhcambuliwe na wote tuujue.
Yapo mashaka na uwezo wa huyo Mhe Waziri Mahanga.Aidha,hiyo Doctorate yake ingefaa awambie umma aliisomea wapi,miaka mingapi na area of specialization? Waziri aonyeshe leo reference ya mafahali yake na Superving professor wake?
Tanzania itaendelea si kwa kubabaisha ila kwa good governance ikiwemo uwazi.
na msomaji, dar, - 2.05.08 @ 17:34 | #9695
Eti shirikianeni na menejimenti kabla ya kutoa habari kwa vyombo vya habari.Bado anafikiria serikali ya chama kimoja huyu ******.Kama yaliyosemwa yote ni ya kweli,ubaya ninini?Wangezungumza habari za uongo,hapo sawa.Hawa watu wanajeuri sana na ubabe uso maana.Mi napenda sana US maana huwezi kumbabaisha mtu.Who cares,asubuhi unamfukuza mtu kazi,mcna au jioni kapata nyingine.Sio kuleteana habari za kis**ge.Siku moja watu watacharuka na kumkana waziri live.Hiyo inakuja tu.Wache waendelee kulewa madaraka.Kwei ipo haja ya kujua CV yake huyu Mahanga.
na OH, US of A, - 2.05.08 @ 18:03 | #9699
Jamani wanaofahamu cv kama tulivyoomba hapo juu (9682) waimwage hapa tuione. Hafai, anatetea ufisadi.
na Kawala, Ubelgiji, - 2.05.08 @ 18:09 | #9700
Nawapongeza wote mliochangia hapo juu. Naipenda sana ATC lakini napata mashaka ya shirika hili kuendelea chini ya uongozi wa akina Dr Makongoro Mahanga. Tuwe wazi kwenye mikataba tuziwazuge watanzania kwani dunia ya leo siyo ya siri za akina Dr. Mahanga. Hivi huyu Mh. akiambiwa shirika letu la ATC limetangaza taarifa za mwenendo wake wa kibiashara si atawafukuza wachumi wa ATC? Kuhusu utitiri wa Madaktari viulizo waliojaa Tanzania nashauri tuache kuoneana aibu kila ajiitaye Daktari (PhD) atoe yafuatayo: 1. Kichwa cha habari (title) cha eneo alilosomea (thesis) hadi akapata huo udaktari.
2. Muhutasari wa hiyo PhD yake
3. Makala aliyoandika hata kama alichapisha kwenye jarida la kijijini kwake mfano " Uchochoroni journal of self made Bongo Doctors....au hata makala aliyochapisha kwa lugha yake ya asili, maana hawa madaktari wengine hawawezi hata kupambanua mambo kwa lugha kali kama hii ya kiswahili , achilia mbali lugha za kigeni.
Nasikia kuna taasisi moja hapa nchini inahusika na udthibiti ama kutathmini degree za watu waliosome nje, je hili ni kweli? naomba waanze na hao waliotiliwa mashaka. Vinginevyo nchi itaendelea kudidimia kwa kuwa na madaktari wenye PhD batili.
na Matata, DSM, - 2.05.08 @ 18:21 | #9701
Book title ya Mh. Makongoro hii hapa:
Urban Housing and Poverty Alleviation in Tanzania. Vitu kama hivi vinathibitisha kuwa ni daktari genuine. Lakini wale ambao hata mistari michache ya kazi zao ni adimu kama kakakuona du!!!
na Matata, DSM, - 2.05.08 @ 18:34 | #9702
Sifa za Fisadi ni:
i.kupindisha sheria hata kama anazijua
ii. kuhalalisha uovu wake
iii. kujijengea kinga kwa kuungana na waovu wenzake waliojuu yake kicheo au hata waliochini yake
iv. kufumbia macho maovu ya washirika wake na kukazia macho ya wengine
v. kutoa vitisho,kuhujumu au hata kuwaua wanaoingilia himaya yake ya uovu
Hizo ndizo baadhi ya dalili za fisadi
na majaliwa, UK, - 2.05.08 @ 19:54 | #9705
Asante Matata kwa jina la Kitabu cha Mahanga. Alisomea Chuo gani?
Mbona anadhalilisha kisomo chake, alikariri tu? Anashindwa kuoanisha dhana ya poverty (umasikini)na Urban Housing? (makazi ya mijini) au tuseme urban infrastructure (miundo mbinu ya mijini kwenye kitabu chake?. Sasa kama kuna ufisadi katika ununuzi wa tenda za ujenzi wa miundombinu ya mijini umasikini utaondokaje?
ATCL itachangia vipi kuondoa umasikini (poverty) ili kuleta hali bora ya makazi ya mijini (urban housing) kama pesa inaibiwa kwa ununuzi wa vyombo vya usafiri kitapeli. Ndiyo maana nasema amekariri huyu. Chuo gani alisomea? Je bado anastahili kuwa na cheti hicho? Anashindwa kutekeleza kwa vitendo yake aliyoandikia kitabu chake!!
Hafai huyo anakinzana na kitabu chake kwa kutetea ufisadi, atolewe uwaziri.
na Kawala, Ubelgiji, - 2.05.08 @ 20:46 | #9712
Asante Matata kwa jina la Kitabu cha Mahanga. Alisomea Chuo gani?
Mbona anadhalilisha kisomo chake, alikariri tu? Anashindwa kuoanisha dhana ya poverty (umasikini)na Urban Housing? (makazi ya mijini) au tuseme urban infrastructure (miundo mbinu ya mijini) kwenye kitabu chake?. Sasa kama kuna ufisadi katika ununuzi wa tenda za ujenzi wa miundombinu ya mijini umasikini utaondokaje?
ATCL itachangia vipi kuondoa umasikini (poverty) ili kuleta hali bora ya makazi ya mijini (urban housing) kama pesa inaibiwa kwa ununuzi wa vyombo vya usafiri kitapeli. Ndiyo maana nasema amekariri huyu. Chuo gani alisomea? Je bado anastahili kuwa na cheti hicho? Anashindwa kutekeleza kwa vitendo yake aliyoandikia kitabu chake!!
Hafai huyo anakinzana na kitabu chake kwa kutetea ufisadi, atolewe uwaziri.
na Kawala, Ubelgiji, - 2.05.08 @ 20:48 | #9713
Kuna mtu alidai kuwa wanasiasa "They don't mean what they say, they don't say what they mean". Nadhani alikuwa sahihi!
na Kibabu, USA, - 2.05.08 @ 21:38 | #9717
Niliwahi kufanya kazi, zamani na Dk Mahanga, Sikutegemea kama alishabadilika namna hivi.
Alikuwa mteteaji wa hoja, hakuridhik na dhuluma lakini sasa ameishiwa nguvu baada ya kupata unaibu waziri, nafikiri aendelee kuwa NAIBU maana akipewa Wizara ni tatizo kubwa!.
Kama watu wanavujisha siri za kweli zinazowakandamiza ni 'dhambi' kubwa kuendelea kufunika siri kama hizo katika jamii ya leo ya utandawazi.
Dk Makongoro kama mpiganaji na msomi uliyehangaika na kuhama sehemu mbali2 ukitetea hali bora ya masiha,tafadhali rudi kwenye hoja ya utetezi na uwaombe radhi watanzania.
Kwa hali hii tunakuombea Mhs Rais aendelee kukuweka NAIBU hujakomaa kupewa wizara!
na T.MUZUMA, Darwin-Australia, - 3.05.08 @ 04:11 | #9720
Kwisha huyu MAKONGORO MAHANGA atamfuata ndg yake ANDREW CHENGE!amekwisha fanya kosa kubwa sana kuwatukana wafanyakazi wa ATCL!hii dhambi itamwandama hadi aangamie
na jingo - 3.05.08 @ 10:44 | #9725
Mahanga, Mahanga, Mahanga!
Bado unamambo ya zamani ya kutishana tu mwanangu! Ni nani alikupa u dokta wa aina yako? Yaani bado unaota masuala ya kina Idd Amin, Mussolin, Bokassa na Akina Mobutu? Hujui watu wa aina yako leo tunaweza kuwahesabu! Ngoja nikupe idadi yenu. Yupo Mugabe, Museveni, Kagame....... duh wachache sana! haaaaaa na wewe nilitaka kukusahau! Acha mambo yako ya zamani!
na LCD, Pyongyang, Korea ya Kaskazini, - 3.05.08 @ 10:51 | #9727
phd yake amesoma washington university.ni zile za kutengenezewa na wajanja.
na chuma ulete, us, - 3.05.08 @ 08:43 | #9729
Kikwete hembu tuondolee mtu huyu maana ni mzigo kwako. Kauli mbiu yako(uliyoiboresha) ni 'Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana iwapo mafisadi watadhibitiwa' huyu Mahanga anaelekeza kukamatwa wale wanaofichua mafisadi, je tutafika? Watanzania tuunganishe nguvu tumwandame na tuhakikishe Mahanga anaondolewa kwenye baraza la mawaziri tuone hiyo jeuri yake kama ni kubwa kuliko jeuri ya wananchi. Pamoja na Mattaka kuwa Mkurugenzi mkuu wa ATCL bado wananchi hatujasahau jeuri yake alipokuwa PPF ndio maana JICHO kali lazima limmulike wakati wowote. Si huyu MATTAKA(alipokua PPF) na TEMU (alipokuwa BIMA)walifanya kufuru Butiama wakati wa msiba wa Mwalimu kwa hela ya watanzania. Na kama kweli ana hela yake iliyomfanya akufuru kwa nini arudie uongozi ATCL? Mbona kuna mashirika yako hoi yanatakiwa hao wanaojidai kuwa na uwezo wakayafufue kama shirika la UDA, si aende huko akalifufue? Watanzania wazalendo na wafanyakazi wa ATCL muangalieni sana huyo Mattaka na Mahanga wake maana shirika likifa nyie na watoto wenu ndio mtakaokufa njaa na sio huyo mjinga mjinga Mahanga.
na Mfuatiliaji - 3.05.08 @ 11:14 | #9741
Mfuatiliaji ni kweli wafanyakazi wa shirika la ATCL wanawajibu wa kulinda shirika lao/letu lisife sababu ya ufisadi unaolindwa na Mahanga.
Ni ukweli mtupu kuwa shirika likifa watoto na familia zinazowategemea zitakuwa na hali mbaya kimaisha. Wafanyakazi wa ATCL mnawajibu wa kuzidisha juhudi kutoa siri za kuhujumu shirika kwa wizi.
Lakini pia ATCL inaendeshwa kwa pesa zetu wananchi tunaolipa kodi ambayo huchangia bajeti ya wizara husika. Ninyi wafanyakazi wa ATCL mnapolinda shirika dhidi ya ufisadi mnatulinda wananchi dhidi ya umaskini. Teteeni shirika, teteeni familia zenu, teteeni kodi zetu. Mahanga aondolewe hafai kuwa waziri. Mafisadi wa ATCL waondolewe pia.
na Kawala, Ubelgiji, - 3.05.08 @ 11:49 | #9748
Ujumbe huu ni kwa ajili ya Mh. Zito Kabwe, maana viongozi wetu wengi hawasitahili kuitwa waheshimiwa, sitahili yao ni kuitwa mafisadi.
Mh. Ninasikia unakutana na watanzania waliopo Michigan Marekani. Hawa wanatuwakilisha watanzania wengine pia. Kati ya mambo utakayoongea naomba ueleze vyama mbadala (sipendi kusema vyama vya upinzani) mna mikakati gani ya kuongeza wabunge wa upinzani mwaka 2010. Ueleze jinsi mnavyowafikia wananchi wa vijijini kuelimisha demokrasia, kufungua matawi na kueleza umuhimu wa vyama mbadala. Wingi wa wabunge wa vyama mbadala ni muhimu katika kuhakikisha kuwa hakuna ufisadi Tanzania na kuwa maliasili yetu inaendeleza nchi yetu mfano kujenga mtandao mzuri wa miundo mbinu.
Kujikita vijijini ni muhimu kwa sababu kuna wapiga kura wengi na ndiko wanakodanganywa na kutishwa. Halafu uwe unatoa taarifa ya mafanikio ya kujikita kwenu vijijini kwa wananchi mara kwa mara. Tumieni muda mwingi vijijini.
Ninaomba aliyekaribu na Mh. Zito amwambie asome ujumbe huu. Ninatanguliza shukrani.
na Kawala, Ubelgiji, - 3.05.08 @ 16:30 | #9767
Mahanga unahofu ya kumfuata bosi wako? njia siyo kuwatisha watanzania bali ni kuwa mkweli na muwajibikaji na mwenye daima kuikiri unataka kuifanyia nini Tanzania na siyo Tanzania ikufanyie nini. Kwa mtizamo wetu, hofu yako inadhihirisha wewe hauko mbali na bosi wako, inabidi uma wa Watanzania waelekeze macho yao kwako sasa. Inawezekana hata shutuma za utapeli wa milioni 50, zilizowahi kusikika miaka ya nyuma kidogo zilikuwa za ukweli. Tutaomba kuzisikia vyema sasa!
na Mtanzania, TZ, - 3.05.08 @ 19:50 | #9770
Mahanga bado anaota masuala ya zamani ambayo yameshapitwa na wakati! Mikakati yote anayoiita siri ni ujinga ambao umeriporomosha shirika huku viongozi wake wakiporomosha masinagogi huko kunduchi na kwingineko!
na LCD, Pyongyang, Korea Kaskazini, - 4.05.08 @ 12:50 | #9782
HIVI WATANZANIA TUNASUBIRI NINI,KIONGOZI KAMA HUYU CHINA ANACHINJWA HADHARANI. TUNAHITAJI KUANZA KUWAADHIBU HAWA VIONGOZI HADHARANI...MAKONGORO HAFAI NI FISADI SANA NA ANASHIRIKIANA NA MATAKA!JK MUONDOE HUYU HATUFAI SAFISHA HIYO WIZARA LASIVYO UTASHUHUDIA MAAFA YA YA HIYO NDEGE.ISIMAMISHE ISIFANYE KAZI NI MBOVU HAIFAI!
na makundi, Cardiff,UK, - 5.05.08 @ 10:22 | #9801
Kampuni hii ya Mbowe imefilisika?
Hivi sasa nina siku kadhaa silioni gazeti la Tanzania Daima katika mtandao! Gazeti lilianza kutoka kwa kuchelewa sana hadi limesababisha malalamiko lukuki kutoka kwetu hasa tulio mbali na nyumbani! Baadhi ya siku gazeti hili limefikia hatua ya kuchelewa zaidi ya siku moja na hivi sasa halionekani kabisa. Naomba sasa mwenyekiti wa board ya wakurugenzi, mheshimiwa Freeman Mbowe atangaze kufilisika kwa kitengo kinachotoa gazeti hili ili uchunguzi uanze kama kuna fisadi limetembelea huko!
na LCD, Pyongyang, Korea, - 5.05.08 @ 09:46 | #9810