ATCL: Another Richmond!

ATCL: Another Richmond!

JK fukuza hii MAKONGORO tayari imeshakuharibia hivi kaka JK kule mjengo hakuna watu wasafi ukawapa vitengo????maana huyu tayari ni FISADI au unataka Dr.Slaa amlipue ndo ushituke??
Mwajibishe anakushafulia,huyu jamaa CV zake zilisha chafuka kwa nn unalea mifisadi hii tunakushindwa kukuelewa mkuu.


.........WAZEE NINI KIMEMKUTA MAKONGOZO ..NAONA HAJAAMBATANA NA RAIS KWENYE UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA BARABARA YA SHELUI..,SINGIDA....NAONA RIPOTI ZOTE ALIZOTAKIWA KUSOMA WAIRI WA MIUNDOMBINU...ANAZISOMA OMARI CHAMBO,KATIBU MKUU
 
Huyu na yeye anatengeneza kaufisadi kake kadogo katako msumbua wakati wa uchaguzi maana watu watamuuliza yeye kama naibu waziri alichukua hatua gani na atakosa jibu. Mwenzake mzee wa kula majani mambo yake sio mazuri sasa halafu yeye anakingia kifua vitu ambavyo hana uhakika.

Hivi anafikiri mfanyakazi gani atasimama na kumwambia mataka kuwa wewe ni fisadi, amewasaidia vipi watu waliofunguliwa kesi kwa kuwauliza viongozi maswali. This guy doesnt think.
 

.........WAZEE NINI KIMEMKUTA MAKONGOZO ..NAONA HAJAAMBATANA NA RAIS KWENYE UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA BARABARA YA SHELUI..,SINGIDA....NAONA RIPOTI ZOTE ALIZOTAKIWA KUSOMA WAIRI WA MIUNDOMBINU...ANAZISOMA OMARI CHAMBO,KATIBU MKUU

Tuendelee kutega masikio...
 
Tuendelee kutega masikio...
Hivi unafikiri Jk ajui Uwezo wa Makongoro Mahanga??unafikiri ni kwanini watu kama Ngeleja walipewa unaibu na kumkuta mahanga ila kwa sasa ni Full Ministers??ana uwezo mdogo sana katika kutatua matatizo
 
Hivi unafikiri Jk ajui Uwezo wa Makongoro Mahanga??unafikiri ni kwanini watu kama Ngeleja walipewa unaibu na kumkuta mahanga ila kwa sasa ni Full Ministers??ana uwezo mdogo sana katika kutatua matatizo

Gembe,
Ninakubaliana na wewe moja kwa moja. Mahanga si mtu mwenye vision nzuri na kweli hawezi kutatua matatizo nadhani hata kama ni ya familia yake.

Hizi kauli anazotoa alidhani zitamnufaisha kisiasa mbele ya bosi wake hususan wakati huu ambapo Ofisi ya Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Miundo Mbinu iko wazi. Tamaa inamponza hadi kukurupuka kuongea maneno yanayoidhalilisha serikali.

Upande mmoja wa serikali unasisitiza wafanyakazi wafichue maovu na upande wa Mahanga unasisitiza wafanyakazi wafiche maovu. Nadhani awe muungwana asahihishe kauli yake kama alivyofanya Mh.'Vijisenti'
 
Juzi juzi yaani mei mosi Risala ya Raisi kwa wafanyakazi iliyosomwa na Pinda Iringa, alisema wafanyakazi wasikubali kutumiwa na Mafisadi, sasa wafanyakazi wa ATc wanakata kutumika, lakini Bw Maokongoro Mahanga ana fikra tofauti, sasa sijui kauli ya nani iliyo juu ya mwengine?
Pili nini Msimamo wa serekali kuhusu hili la kufichua maovu, ni wa Mahanga au wa Raisi? Tatu huyu mahanga ni mtaalamu wa manunuzi na alikuwa Regestrar wa NBMM, sasa kama na anapigia pande ununuzi usiofuata taratibu , je kuna haja ya kusoma au kuwa na hiyo nbmm? Kazi kwako Jakaya, BP inakukaribia na mengineo, siku watanzania wakiamua mzigo ni wako , sio wa Mahanga.

Ni kweli kabisa kuwa Rais Kikwete alishasimama kidete na kubainisha wazi kuwa katika URAIS wake na hivyo madaraka ya kuongoza serikali ya awamu ya nne HANA UBIA na mtu yeyote zaidi ya Makamu wake, Dkt. Mohamed Shein. Kudhihirisha hilo, aliacha Lowassa, Msabaha, Karamagi na Chenge aka Vijisenti waende na maji kuonyesha kuwa hakuwa na ubia. Sasa huyu Makongoro Mahanga (PhD???) ambaye ni NAIBU WAZIRI anapotoa kauri inayopingana na Mkuu wa Kaya tunamshangaa, hapa Makongoro Mahanga labda analazimisha ubia na Kikwete au anajikomba bila kipimo. Tusubiri tuone kama Mkuu wetu wa nchi anakubali huu ubia au vipi, yetu masikio na macho. Chonde chonde RAIS wetu, tuondolee huyu mtu hapo MIUNDO MBINU utuletee timu mpya labda itakuwa makini zaidi kuhusu suala la ATCL na MIUNDO MBINU kwa ujumla katika mtazamo wa kupambana na UFISADI.
 
Mhanga anajipendekeza kwa Sababu anajua JK na Mataka na Mwenyekiti wa Bodi ni Maswahiba Alhaji Mustafa Nyanganyi aka Mzee wa Chelezo kilichoitwa Pantoon, so mpaka Panga limpate yeye anajua anakinga ya Hao watu Wa wili
 
Ndugu msomaji si dhumuni langu kuanza kuuliza maswali haya ila ni kwa ajili ya kampuni na msalahi ya taifa..kama tunavyojua hivi sasa limerudi baada ya kuwepo kwenye mikono ya mafisadi makaburu...sasa badala ya kujiimarisha nasikitika masikini na kukumbuka enzi za marehemu sanare mko wapi ndugu zetu muokoe jahazi hili...mungu ampe rehema zake..si wakati wa kunyoosheana vidole ila inapofika wakati taifa likiwa na njaa kila mtu akiwemo adui hushiriki kutoamsaada....,wakata watu wakiwa na hamu kubwa kusikiliza nani atateuliwa mkurugenzi wa ATCL. Kila mtu alikuwa ana hamu kuona likipata mzawa mwenye upendo na nia njema ya kampuni Lah hasha...muda ukafika mwali akatolewa si mwingine bali ni yule aliesimamisha majumba kila kona ya dar es salaam MH DAVID MATTAKA......kila mmoja alikuwa akitarajia makubwa natumaini hata sie tulie nje ya ATCL tulikuwa na shauku kuona wapi ruti za DUBAI MAURITIUS LONDON NA KWINGINEKO..

muda umepita hivi sasa mhe baada ya kuingia tu natumaini alipewa meno ya kuchagua management yake alijaribu kuweka marafiki zake ambao hivi sasa wanazidi kumtafuna na kusubiri siku atakapopewa notes ndipo watakapomcheka.......nilikuwa na akina mh makongoro kipindi hicho na nilijashangaa hata kuona ndugu yangu akiongea maneno ya ajabu bungeni kuhusu wafanyakazi ...na kama mnakumbuka nilitoa mwawazo makongoro hauna muda hapo ulipo..masallah shukuru kijana mwenzako ameogopa kukutupa kijiweni....

Ni wakati mh alipoingia tukaanza kusikia ansafiri kila leo...hongera zenu wafanyakazi tunasikia mkaongezea mshahara na mkiwa nje doller 250-400..ndani sh 250 sio mbaya hii ni nguvu mpya..wakiwa wanacheekela ndugu zetu wafanyakazi mh alianza kuruka safari moja baada ya nyingine na ka ma si member mmoja wa JF KUPASHA HABARI NATUMAINI ALIZISOMA NDIPO ALIPOAMUA KUPUNGUZA SAFARI NA NASIKIA HATIMAE KAAMUA kuwa ofisini..nasikitika kuna kipindi wakiwa wanajirussha na kulipana doller 400..yeye 500./.nilipata kwenda ofisini kwake na kukuta anakaimu manager muajiri..hii ilikuwa hatari kila manag ameenda nje.....si vibaya wakiwa na mafanikio makubwa wafanyakazi wao...ikaanza minongono ndege inakuja mpya wachina wanakuja mmmmmhhh ilikuwa heri...sasa david rafiki yangu wa karibu sana kaka yangu nduguyangu na hata kijiwe tuko pamoja,,,nimeuishwa kuongea hivi baada kunitokea haya yafuatayo

wiki iliyopita nilikuwa niende mwanza kukagua kazi asb mapema gafla nikaambiwa ndege imejaa tukaaka kama watu 30..kuuliza ndege ndogo...tukarudi..mamayangu mzazi akiwa anaenda mwanza juzi mkamrudisha ndge ndogo..juzi nikiwa naenda UGANDA kikazi nimepanda nndege ndogo inaondoka na kufika mwsho inarudi
 
Ghafla tukashuka nikakutana na ndugu zangu niliokuwa nao ATCL BAADHI PALE CHINI NIKAULIZA KULIKONI..MBONA KUNA NYINGINENE IKO PALE MBONA MMELETA AIRBUS HAIRUKI? Kwa kweli majibu yake yalikuwa ni kujuta kwanini wameondoka makaburu... Nikaambiwa ndege imeletwa watu wanapelekwa shule nusunusu...hawamaliziwi kuuliza why hakuna pesa..

PILI:: nikaambiwa ile ndege kubwa AIRBUS kweli iko pale ila wakati mkiwa mnasaini mkataba ati hamkuona kuna kipengele kinawaitaji kuwapa doller milion 700 watu wa matengenezo ya ndege...

TATU:: hiki kiliniumiza zaidi kuambiwa kuna ndege ya boingi iko imepaki haina matairi kampuni haina hela ya kutuma matairi..jamani wapi kakayanagu unaipeleka kampuni hii?

kibaya kuna tetesi nimesikia mlikodisha ndege toka south africa nikaja kuisoma hapa JAMBOFORUMS..INANUKA ...MMEINGIA MKATABA MNAILIPA DOLLAR 185,000 KWA MWEZI MUITUMIE MSIITUMIE...HIVI SASA TUMESIKIA HAIPO NA MNAENDELEA KUILIPA DOLLAR 185,000 ..BAYA ZAIDI NDEGE NYINGINE IKO CHINI HAKUNA HELA YA KUMLIPA IJINIA SASA MNAFANYA KAZI GANI HAPO?

TUSAIDIE WAPI UNAIPELEKA KAMPUNI HILI NDILO SWALI LANGU
 
Predeshee,

Mimi huwa nashindwa kuelewa. Mheshimiwa Muungwana anapenda sana urafiki, huyu bwana Mataka hawezi kuliongoza lile shirika. Hana mawazo mapya.

Haya mambo ya super managers kama wakati wa JKN, ambapo Kaduma akiharibu hapa anapelekwa kule zitatumaliza. Unakumbuka wakati huo Mwapachu, Kaduma na wengineo wanaharibu lakini wanahamishiwa pengine... Super managers!!!

Bado Muungwana hajaona hilo, siku akielewa basi mashirika ya umma yatasonga mbele!
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma nipo, ninawasikiliza!......
 
Zitto,

Kama upo, basi shauri jamaa wasiwe recycled. Kwanini mashirika ya nje yanayoongozwa na waTanzania tena wengine vijana tu yanafanya vizuri? halafu kwanini uozo ukianikwa hadharani mawaziri wanakuja juu (Mahanga)? kama ni uzushi si wapuuzie? kama ni kweli kwanini wasifanyie kazi?

Pia checking hiyo mikataba. Kwanini ndege inakuja ndio watu wanapelekwa mafunzoni?, kwani hawakujua ndege inakuja lini?

Ni hayo tu kwa sasa.
 
Zitto,

Kwanini mashirika ya nje yanayoongozwa na waTanzania tena wengine vijana tu yanafanya vizuri?

Ni hayo tu kwa sasa.

Asante sana kwa hili Mkuu.

Nafikiri hapa hakuna Siasa za kombolea(kupeana peana ulaji), Hawa wakuu wetu mara nyingi akimchagua Mkuu wa Shirika huwa anampa sehemu ya kula(kupata ulaji) na siyo kufanya kazi kwa ufanisi.

Ndio maana watu kama Mattaka ukifuatilia wakati mwingine wanaenda kuwaangukia wakubwa wawape kazi ya kula. Lakini mashirika ya nje mtu anaomba kazi anafanya interview anapewa kazi kulingana na utaalamu wake ktk kuleta ufanisi.

Tusipobadilisha hili tukachukua watu kulingana na ufanisi tukawashindanisha watanzania katika kuwapa Mtendaji bora ktk mashirika yetu na tukaondoa siasa kamwe tusitegemee mafanikio. Nenda duniani kote angalia mashirika makubwa wakuu wake wanapatikanaje.

Tutapata majibu kwa nini mashirika yetu ya akina Mattaka hayawezi kushindana na kuendelea ktk ulimwengu wa sasa.
 
Sasa hivi wanavyofanya ni makusudi au kazi hawajui yaan sijawahi kuona popote pale duniani mtu ana abuse kazi yake kama TZ ona ya balali sasa huyu Mattaka
Pole sana Kikwete yaani kila mtu ameoza
 
Huyu Mtu Nafikiri Anaitaji Uweza Wa Mungu Aiwezekani Kila Akiteua Anateua Kasa Mbona Hiviiii Jamani Niwewe Kikwete Tuliekujua...ooondoa Bbasi Urafiki Tukuone 2010..yetu Macho
 
breaking nyuzi
----CEO aitwa IKULU KUJIELEZA


naambiwa kwamba ile ndege iliopigiwa makelele na mh makongoro imeshafika inapotakiwa hakuna kuruka wala tataka yake kuruka walio bongo tupeni data...na kwa taarifa kila mwezi ukiacha dollar 370,000 za mwezi kuna doller 200,000 za maintenance kule Mauritius na ndicho kinachogomba kulirusha ...hawa watu inaonekana wakati wakiila pesa za safari hawakuwa wanajua kwamba ipo siku pesa itaisha na hivi juzi kuna ndugu yangu wizara ya fedha anasema wameomba BILLION 21,,, KUWEZA KUENDELEA NA KAZI ZA KILA SIKU... MGONJA DHAMBI ULIZOFANYA EPA ZINATOSHA UKIIDHINISHA NA HIZI MUNGU HATAKUACHA, NA LA UTAKUFA NA HILO NDEGE MKIWA JUU......

MASIKITIKO MENGINE TUMESIKIA ZILE NDEGE NDOGO NAZO NI MBOVU KUFA MTU NA HAKUNA MWENYE UJUZI WA KUZITENGENEZA KATIKA HAO MATECH WAO..HII NI HATARI SANA. JK UNAHITAJI KULIOKOA MAPEMA HILI SHIRIKA .....KUNA NDUGU YANGU ALISAFIRI NAVYO ALARUDI NA PRECISION ALIPOULIZA MBONA VIMEPAKI VYOTE AKAAMBIWA HUJUI???? WANAKULA HADI WANASHINDWA KULIPA MA ENGINEER...

HII NI HATARI SANA KAMA KWELI KUNA MTANZANIA MPENDA NCHI YAKE YUPO ATCL TUELEKEZENI KUHU HILI...HAWA WATU NOW IS TOOOOOOOOOOOOO MUCCCCCCCCCCCCHHHHHHHHH

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Allah Ibarik.........


Mheshimiwa Zitto madamu ndo mwenyekiti, hebu jaribu kuangalia hii mikataba ili nayo ifikishwe bungeni ikiwezekana watu wawajibishwe kama kawaida...kazi yako inatambulika...hawa watu sio wa kuwavumilia HATA KIDOGO!
 
Back
Top Bottom