ATCL: Another Richmond!

ATCL: Another Richmond!

Jaribu hii attachment na kama bado inagoma semeni, nijaribu kutumia njia nyingine.
 
Link ya kudownload iliyonzuri ni hii hapa chini:

http://ardownload.adobe.com/pub/adobe/reader/win/8.x/8.0/enu/AdbeRdr80_en_US.exe

Nimejitahidi kuweka .Zip na .RAR kwenye servers za JF upload inashindikana. Hivyo naomba mtumie hiyo link juu kudownload moja kwa moja. Goodluck.

SteveD.

SteveD,

Huenda tatizo ni hao ambao hawana WINRAR kwenye kompyuta zao. Nimejaribu kutumia format ya ZIP na jaraibuni kama itawezekana kudownload kutoka kwenye posting yangu hapo juu.
 
Duh jamani mimi mpaka natoka jasho!! ujanja wangu wote leo nimeshindwa... hebu check attach hiyo
 

Attachments

hata mimi nimeshindwa kufungua,pls helpppppppppppppppppp
 
Nyie watu mnatumia computer za nchi gani hata mshindwe kufungua?🙂

Baada ya kusoma hizi documents, najiuliza ina maana pale ATC hamna hata kiongozi moja anayefanya kazi kwa maslahi ya shirika. Yaani wote wameoza? Nauliza hivi kwa sababu isije ikawa tunapigana vita ambayo haishindiki! Ukishawatuhuma watu wote, hamna hata moja unayekuwa na imani naye ni kazi sana kuwashughulikia wote kwa mpigo. Hata hivyo sitaki kuamini kwamba wale viongozi wote wana roho ya kifsadi tu. Kama hii itakuwa ni kweli maanake yake ni kwamba sisi watanzania wote tumeshapandikizwa roho ya ufisadi tukiwemo sisi hapa JF, maana kwa idadi yao ni wazi kuwa wanatuwakilishi sisi tulivyo kwa kiasi kikubwa.
 
Kitila
usiseme tunatumia computer gani pls tusaidie mimi na wana JF wengine ambao tumeomba sana iwekwe tena ili tuweze kuangalia manake ile ya kwanza haifunguki.pls help ,thanks in advance.
 
Kwangu imefunguka vyema tu, naendelea kuipitia, nitakuja na maoni baada ya muda.
 
Kitila
usiseme tunatumia computer gani pls tusaidie mimi kuangalia manake ile ya kwanza haifunguki.pls help ,thanks in advance.


Jamani mbona ni one click tu. Kama walivyosema wengine hiyo docs iko zipped hivyo unatakiwa kuwa na WINRAR ambayo unadownload for free. Then hiyo doc fanya ku-extract na chagua file pa kusave hiyo docs yako. Baada ya hapo utaona mafile kama 20 hivi
 
Kitila
usiseme tunatumia computer gani pls tusaidie mimi na wana JF wengine ambao tumeomba sana iwekwe tena ili tuweze kuangalia manake ile ya kwanza haifunguki.pls help ,thanks in advance.

Pole sana mkuu, tatizo langu ujanja kwenye hivi vitu sina kabisa, naweza ku-click tu. Bahati nzuri nilipo-click yakafungaka. Hope kuna jamaa watakusaidia hapa, tuna wataalamu kibao humu!
 
Semanao
nimefanya maelekezo uliyosema imeshindikana,JF member ambaye anaweza kutuwekea tena pls atusaidie...sidhani kama dancing floor imejaa kiasi cha sisi wengine kukaa nje ya club tukisikilizia mziki kwa mbaaaali....inauma sana.
 
Bandugu tusaidieni, nami nafungua lakini wapi, nimedownload adobe 8.0 likini sijafanikiwa,

ninapata msg ifuatayo,

Winzip

Cannot open file: it does not appear to be valid archive.

if you download this file, try downloading the file again.


Wajuvi wa mambo tusaidieni tusakate wote hili goma.
 
Jamani,
Saidieni na sisi wenye kompyuta za 47 tuweze kuisoma.
 
Jamani,
Saidieni na sisi wenye kompyuta za 47 tuweze kuisoma.

Kanyaga twende!
Naweka docs chache chache kwa wale ambao mtandao unagoma kushusha zip folder
 

Attachments

Ujumbe kwa waliotuma hii CD

"Tumefikia kutoa CD hii ili kuchangia katika utawala wa uwazi na ukweli. ATC inapojaribu kujirejesha kwenye mafanikio haina budi kufanya hivyo kwa uwazi na ikiweka maslahi ya Taifa mbele. Ndege yetu mpya tuliyokodi toka kampuni ya Wallis Trading ya Liberia inatarajiwa kuwasili nchini siku yeyote ndani ya wiki hii au siku chache zijazo endapo mambo ya logistics na permissions za kutua sehemu mbalimbali zitakamilika katika hiyo Ferry Flight.

Kwa hakika ni ndege ambayo inapendeza na itageuza shingo za watu pindi itakapopaa kwenye anga letu. Na kwa vile tayari tumepokea ndege mbili za Dash 8 siku chache zilizopita basi ni wakati muafaka kwa Watanzania kuiona mikataba inayohusiana na ndege hizo zote.

Tafadhali fungua kwanza File le PDF la "Introduction" ambalo litakupa utangulizi wa nyaraka nyingine. Baadhi ya Nyaraka zimefanyiwa marekebisho ya mwisho ambayo hayajaweza kupatikana na hivyo kuwapa wasomaji idea tu; pale ambapo marekebisho yamejulikana basi tumeyaambatanisha.

La msingi ni kutambua kuwa hadi hivi sasa tumeshaanza kuilipia ndege hiyo zaidi ya dola 400,000 kwa mwezi pamoja na faini ya kuchelewa kupata udhamini ya dola elfu sitini kwa kila mwezi ambapo udhamini huo haujapatikana. Tunatumaini Watanzania wataelewa zaidi kuhusu shirika lao hilo jipya.

Na mwisho tumeweka habari hii hadharani kama ishara ya kupinga ufukuzwaji kazi wa watumishi wenzetu watano siku chache zilizopita hasa baada ya wao kuonekana wanahoji hoji sana utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wakuu wa shirika hili."


Enigma

Hapa sasa Kikwete sijui kisingizio kuwa ufisadi umerithiwa toka serikali zilizopita kitatumika tena?
 
Back
Top Bottom