ATCL: Another Richmond!

ATCL: Another Richmond!

Ujumbe kwa waliotuma hii CD

"Tumefikia kutoa CD hii ili kuchangia katika utawala wa uwazi na ukweli. ATC inapojaribu kujirejesha kwenye mafanikio haina budi kufanya hivyo kwa uwazi na ikiweka maslahi ya Taifa mbele. Ndege yetu mpya tuliyokodi toka kampuni ya Wallis Trading ya Liberia inatarajiwa kuwasili nchini siku yeyote ndani ya wiki hii au siku chache zijazo endapo mambo ya logistics na permissions za kutua sehemu mbalimbali zitakamilika katika hiyo Ferry Flight.

Kwa hakika ni ndege ambayo inapendeza na itageuza shingo za watu pindi itakapopaa kwenye anga letu. Na kwa vile tayari tumepokea ndege mbili za Dash 8 siku chache zilizopita basi ni wakati muafaka kwa Watanzania kuiona mikataba inayohusiana na ndege hizo zote.

Tafadhali fungua kwanza File le PDF la "Introduction" ambalo litakupa utangulizi wa nyaraka nyingine. Baadhi ya Nyaraka zimefanyiwa marekebisho ya mwisho ambayo hayajaweza kupatikana na hivyo kuwapa wasomaji idea tu; pale ambapo marekebisho yamejulikana basi tumeyaambatanisha.

La msingi ni kutambua kuwa hadi hivi sasa tumeshaanza kuilipia ndege hiyo zaidi ya dola 400,000 kwa mwezi pamoja na faini ya kuchelewa kupata udhamini ya dola elfu sitini kwa kila mwezi ambapo udhamini huo haujapatikana. Tunatumaini Watanzania wataelewa zaidi kuhusu shirika lao hilo jipya.

Na mwisho tumeweka habari hii hadharani kama ishara ya kupinga ufukuzwaji kazi wa watumishi wenzetu watano siku chache zilizopita hasa baada ya wao kuonekana wanahoji hoji sana utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wakuu wa shirika hili."

Enigma

Mshikaji, CD ina mikwaruzo
 
Vp tena jamani mi nnahamu ya kusikiliza na kucheza, TUMEHUJUMIWA NINI???
 
Ahsante mkuu,
Mziki uko bomba, wale ambao mziki unakokoro, jaribuni kuupdate player kwenda kwenye 8.0.
 
Jamaa wanalipa elfu 60 USD kila mwezi kama faini ya kukosa udhamini. Hivi hii serikali...RICHMOND udhamini ulitolewa na serikali kwa gharama ya damu za watu. Katika mikataba ya kwelikweli serikali inasuasua kutoa udhamini, au ni mkakati mwingine wa kuiwekea kitanzi ATCL ili atafutwe kaburu mwingine wa kuiendesha?
 
jamani mimi nimeshinda kufungua hayo mafile yenye huo muziki....inaonekana yako zipped lakini kila nikifungua inasema hamana kitu...nisaidieni jamani maana mwenzenu nataka niugeuze huu muziki kuwa ngoma ya kwetu maarufu "Akasimbo"
 
Ujumbe kwa waliotuma hii CD"Tafadhali fungua kwanza File le PDF la "Introduction" ambalo litakupa utangulizi wa nyaraka nyingine. Baadhi ya Nyaraka zimefanyiwa marekebisho ya mwisho ambayo hayajaweza kupatikana na hivyo kuwapa wasomaji idea tu; pale ambapo marekebisho yamejulikana basi tumeyaambatanisha.
."
Enigma

Mimi nimeshindwa kufungua hayo mafaili....naomba mtusaidie kutuma tena jamani....
 
"dola laki sitini " ndio ngapi?, mbona unaziweka kimafumbo, fafanua pls.

Jee unamaanisha dola millioni 6? au vipi? kama ni hivyo, unaweza kutupa ushahidi wa hilo? kama si hivyo tunaomba ufute hiyo na uweke sawa.

HIVI WE MZEMBE,LINI UTAANZISHA MADA YA MSINGI WATU WAICHANGIE BADALA YA KILA SIKU KUJIFANYA CRITIC?SIKILIZA HIYO CD KWANZA KABLA YA KUKOSOA TU.GET A LIFE,ATTENTION-SEEKER
 
HIVI WE MZEMBE,LINI UTAANZISHA MADA YA MSINGI WATU WAICHANGIE BADALA YA KILA SIKU KUJIFANYA CRITIC?SIKILIZA HIYO CD KWANZA KABLA YA KUKOSOA TU.GET A LIFE,ATTENTION-SEEKER

Jibu swali wacha uppuzi wako. Kilichokukera nini hapo? huna adabu nini wewe.
 
Attempts zangu kadhaa za kudownload zinaelekea kushindwa, ninapojaribu ku-unzip/unpack napata message kwamba file lina error.
 
..ukistaajabu ya musa,utashangaa ya firauni.

..sina la kusema. ndege inapendeza,ingawa msemo wa "vyote ving'aavyo .. ......." unanijia!
 
Mimi nimeshindwa kufungua hayo mafaili....naomba mtusaidie kutuma tena jamani....

Get adobe 8 iko free hii kitu balaaa
Bwana natoka jasho na ngoma za kwetu, Mdumange, jamani nchi ina nini mbona kila kitu kina kuwa na sura ya Richmondi? Mataka atatuambia nini hapa..fisadi, fisadi
 
Get adobe 8 iko free hii kitu balaaa
Bwana natoka jasho na ngoma za kwetu, Mdumange, jamani nchini ina nini mbona kila kitu kina kuwa na sura ya Richmondi? Mataka atatuambia nini hapa..fisadi, fisadi

Kutokana na hii kashfa ya huu mkataba naunda tume kuchunguza naanza majina, Mwenyekiti Mzee wetu Mwanakijiji, Msaidizi ES, wajumbe, Lunyungu, Rev Kishoka, Bubu, Morani , Mwafrika wa kike na wajumbe wengine nitaongezea baadaye nataka ripoti na mapendekezo nitawatumia TOR, kazi ifanyike kwa wk nne kwa kuwa tunataka mikataba ijali maslahi wa wananchi na taifa...tupo pamoja jamani?
 
Mimi nimeshindwa kufungua hayo mafaili....naomba mtusaidie kutuma tena jamani....

Ndiyo kuna tatizo kwenye hilo kabrasha (santuri, aka CD!). Nimesota nalo mpaka nikapata ufumbuzi (rejea, nina Adobe toleo la nane, hivyo tatizo sio toleo la Adobe, bali ni jinsi kabrasha lilivyohifadhiwa).

Namna ya kutatua (kwa wanaotumia WINRAR, mwingine na asaidie wenye WINZIP)... Kupitia WINRAR, nenda (browse) hadi lilipo kabrasha la ATC SAGA007.zip, na kisha endelea na hatua namba mbili kwenye huu ukurasa: http://ezinearticles.com/?Repairing-A-Corrupt-.RAR/.ZIP-Archive&id=16138
 
Mimi siyo mjuvi wa hii technologia ya BILL GATES lakini mziki umefunguka bila matatizo yoyote!

Jamani hali inatisha, nasema tena, hali inatisha kwa mwendo huu, Tanzania sijui inakwenda wapi!

Hivi mnajua kwamba INAWEZEKANA TANZANIA IKAWA IMESHAUZWA KINACHOSUBIRIWA NI MWEKEZAJI KUWAHAMISHA WAKAZI WA TANZANIA AANZE JUHUDI ZA "KUENDELEZA MALI YAKE"

USHAURI WANGU: Its high time BUNGE lisimame kidete kudai waione hii miakataba, waache kusikiliza cheap politics za akina Ngasongwa kwamba mikataba ni siri! Maana kila tunachokiona ni UFISADI uliopindukia, sasa jiulize kama 95% ya mikataba iko hivi, hali iko vipi wandugu?

No way this bunge should stand up or else wananchi tuweke petition kwa JK. Hii hali si njema kabisa! si kitu cha kushangaza tena, its critical to the survival and continued existence of Tanzania as a nation!

Just a question: Hivi mwanasheria wa Serikali alisoma sheria kweli? Maana siamini kwamba these are the kinds of contracts Tanzania is signing under his watch! Kama sikosei hii mikataba si inabidi ipite ofisini kwake kwa ajiri ya verification? Nachoka!
 
Back
Top Bottom