ATCL: Another Richmond!

ATCL: Another Richmond!

Hongera sana JF kuwa kimbilio la wanyonge.Halafu leo anakuja Mwema na kundi lake wanatuita sisi Magaidi? JK ungeyajulia wapi haya ? JK sisi tunakusaidia kuijua Nchi unayo iongoza ulipashwa kukata fungu toka kwenye vile vifungu Votes am sub votes na utupatie tuwe Taasisi ambayo hatutaki uweke mkono wako .Hapa tungejua unataka kupambana na UFISADI.

Hivi huyu Mattaka ndiye ambaye amekuwa akisifiwa kwa Uongozi na Ubunifu ama ni mimi nachanganya madawa hapa ?
 
Huu Ufisadi naona una baraka za wazee. otherwise hatua zingekuwa zimeisha-chukuliwa
 
Jamani mambo ya nchi hii yanasikitisha, hivyo CHADEMA mnafikiri inaweza kubadilisha hali? Kama wanaweza basi tujitoe tuwape inaweza kutusadia maisha duni ya sisi walalahoi yakaonyesha tofauti.
 
Naapa Katu Sintorudi Tanzania Maana Sioni Sababu Ya Kufa Kwa Msongo Wa Mawazo Labda Nisikie Huo Uozo Wote Umefutika, Na Tuna Kizazi Kipya Chenye Maadili. Maana Kwa Mahala Uozo Ulipofikia Sasa Hivi,akili Yangu Inazimika Nashindwa Kujua Mtaanza Kulisafisha Lipi Na Kumalizia Na Lipi
 
Major

Ujumbe wako umenigusa mpaka nimeshindwa kukaa kimya. Uovu hushamiri Wema unapojificha. Uwongo hujitapa ukweli unapokataa kujitokeza. Hivi kama kila mtu akakata tamaa kama wewe ni lini hicho kizazi kipya chenye maadili kitakuwepo? Ni lini uozo huo utafutika? Kupata msongo wa mawazo ni hatua kuelekea fikra mbadala. Endelea tu kuwasusia fisi bucha kama ni uamuzi wa busara, labda ipo siku watamaliza nyama yote na kufa njaa wenyewe! Lakini kwa maoni yangu, sikulazimishi urudi nyumbani; lakini popote pale ulipo usisite kutoa mchango wango wa kiakili, kiroho na kimwili katika kuisaficha nyumba yako. Ukiona uovu unaibuka kwa wingi zaidi basi ni ishara ya anguko la uovu wote. Ukiona kelele za radi kali, mawingu nk ujue mvua inakaribia kunyesha. Usikate tamaa, bado kitambo kidogo tu- ukombozi u karibu. Haya yalikuwa hayatoki hadharani, sasa yameanza kutoka. Sasa usilalamike kuwa yanatoka kwa wingi! Furahi kwa kuwa yanatoka!. Tuendelee kuyatoa tu, na tusiishie kuyatoa tu. Tujiandae kuchukua hatua.

JJ

Ps: Jasusi, nitatoa maoni yangu kuhusu Hotuba ya Kikwete. Rev Kishoka, nitazungumzia kuhusu Kiteto kama nilivyoahidi. Kwa sasa wakati ukuta.
 
Ujumbe kwa waliotuma hii CD

"Tumefikia kutoa CD hii ili kuchangia katika utawala wa uwazi na ukweli. ATC inapojaribu kujirejesha kwenye mafanikio haina budi kufanya hivyo kwa uwazi na ikiweka maslahi ya Taifa mbele. Ndege yetu mpya tuliyokodi toka kampuni ya Wallis Trading ya Liberia inatarajiwa kuwasili nchini siku yeyote ndani ya wiki hii au siku chache zijazo endapo mambo ya logistics na permissions za kutua sehemu mbalimbali zitakamilika katika hiyo Ferry Flight.

Kwa hakika ni ndege ambayo inapendeza na itageuza shingo za watu pindi itakapopaa kwenye anga letu. Na kwa vile tayari tumepokea ndege mbili za Dash 8 siku chache zilizopita basi ni wakati muafaka kwa Watanzania kuiona mikataba inayohusiana na ndege hizo zote.

Tafadhali fungua kwanza File le PDF la "Introduction" ambalo litakupa utangulizi wa nyaraka nyingine. Baadhi ya Nyaraka zimefanyiwa marekebisho ya mwisho ambayo hayajaweza kupatikana na hivyo kuwapa wasomaji idea tu; pale ambapo marekebisho yamejulikana basi tumeyaambatanisha.

La msingi ni kutambua kuwa hadi hivi sasa tumeshaanza kuilipia ndege hiyo zaidi ya dola 400,000 kwa mwezi pamoja na faini ya kuchelewa kupata udhamini ya dola elfu sitini kwa kila mwezi ambapo udhamini huo haujapatikana. Tunatumaini Watanzania wataelewa zaidi kuhusu shirika lao hilo jipya.

Na mwisho tumeweka habari hii hadharani kama ishara ya kupinga ufukuzwaji kazi wa watumishi wenzetu watano siku chache zilizopita hasa baada ya wao kuonekana wanahoji hoji sana utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wakuu wa shirika hili."

Enigma
 
Uuuwiiii ngoj nilie kama mchaga, sasa hii si inahitaji Ipod maana ni ndefu mno... Watalia mwaka huu!
 
Phew!.. haya ngoja tuanze kuchungulia kilichomo; naona tutakesha maana wengine tuliganda kama wachezao mganda!
 
Lakini mbona CD inacheza mganda kwenye baahi ya nyimbo na kuzima redio? Halafu lease mwanzoni inasema mkataba ni wa October 2007 lakini mwishoni unasema October 2006!
 
Hiyo CD kwangu inaonekana Blank, naona majina ya nyimbo lakini nyimbo hazisikiki!
 
duh pouwa maana na mimi nilidhania mafisadi wamefanya vitu vyao tena.. maana hawachelewi.
 
hizi ndege sio mitumba.... ni zaidi ya mitumba...20yrs!!
Hii nchi imeoza vbaya... can't talk no more!
 
wakuu kwa usawa huu taifa limekwisha! Heeheheh.....

Mziki mzito, ama kweli sijui kama serikali itapigana hii vita ya tecnhologia na watanzania! Haiwezi. Mataka atashikwa na BP akijua haya mambo yamekuwa exposed hapa! Inatisha aise!

Thanks Enigma! Keep the ball rolling!

The struggle continues!
 
Nashindwa hata kwenda kulala.... sasa najua kwanini walitaka kutuzima humu.. nadhani kuna haja ya kuanza kufanya maombezi ya Taifa letu..
 
Ujumbe kwa waliotuma hii CD

"Tumefikia kutoa CD hii ili kuchangia katika utawala wa uwazi na ukweli. ATC inapojaribu kujirejesha kwenye mafanikio haina budi kufanya hivyo kwa uwazi na ikiweka maslahi ya Taifa mbele. Ndege yetu mpya tuliyokodi toka kampuni ya Wallis Trading ya Liberia inatarajiwa kuwasili nchini siku yeyote ndani ya wiki hii au siku chache zijazo endapo mambo ya logistics na permissions za kutua sehemu mbalimbali zitakamilika katika hiyo Ferry Flight.

Kwa hakika ni ndege ambayo inapendeza na itageuza shingo za watu pindi itakapopaa kwenye anga letu. Na kwa vile tayari tumepokea ndege mbili za Dash 8 siku chache zilizopita basi ni wakati muafaka kwa Watanzania kuiona mikataba inayohusiana na ndege hizo zote.

Tafadhali fungua kwanza File le PDF la "Introduction" ambalo litakupa utangulizi wa nyaraka nyingine. Baadhi ya Nyaraka zimefanyiwa marekebisho ya mwisho ambayo hayajaweza kupatikana na hivyo kuwapa wasomaji idea tu; pale ambapo marekebisho yamejulikana basi tumeyaambatanisha.

La msingi ni kutambua kuwa hadi hivi sasa tumeshaanza kuilipia ndege hiyo zaidi ya dola 400,000 kwa mwezi pamoja na faini ya kuchelewa kupata udhamini ya dola laki sitini kwa kila mwezi ambapo udhamini huo haujapatikana. Tunatumaini Watanzania wataelewa zaidi kuhusu shirika lao hilo jipya.

Na mwisho tumeweka habari hii hadharani kama ishara ya kupinga ufukuzwaji kazi wa watumishi wenzetu watano siku chache zilizopita hasa baada ya wao kuonekana wanahoji hoji sana utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wakuu wa shirika hili."

Enigma

"dola laki sitini " ndio ngapi?, mbona unaziweka kimafumbo, fafanua pls.

Jee unamaanisha dola millioni 6? au vipi? kama ni hivyo, unaweza kutupa ushahidi wa hilo? kama si hivyo tunaomba ufute hiyo na uweke sawa.
 
Back
Top Bottom