Askofu Kilaini: Ni Wajibu wa Viongozi wa Dini kutetea maadili na Utawala bora

kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
4,314
8,306
Akichangia Mjadala Katika Kipindi cha Minzani Kilichorushwa mubashara na TBC Kilichowajumuisha pia Shehe Salim Aliyekuwa Shehe mkuu Wa Dsm, Hamadi Rashid M/kiti Wa ADC na Mkongwe Steven Wasira.

Askofu Kilaini Amesema Si vyema Viongozi wa Dini Kutumia Mimbari Ukiwa bado umevaa Cheo chako au Joho lako la kichungaji Kuhubiri Siasa hasa Ukiwa Una Tiketi ya Chama fulani.

Lakini ni Wajibu Kamili Kukemea Uvunjivu Wa Maadili,Kutetea Uadilifu kwa wananchi na Hasa hasa Viongozi kwa Maslahi Mapana ya Wote kwenye nchi.

Nalo hilo muende mkalitazame!
 
Lakini ni Wajibu Kamili Kukemea Uvunjivu Wa Maadili,Kutetea Uadilifu kwa wananchi na Hasa hasa Viongozi kwa Maslahi Mapana ya Wote kwenye nchi..!

Nalo hilo muende mkalitazame ..!
Ni kweli kabisa! Viongozi wa dini ni wadau na washiriki wa maendeleo ya taifa kutokana na huduma taasisi zao zinazotoa kwa jamii/umma wa Watanzania katika sekta mbalimbali.

Kwa upande mmoja, huwezi kusema hawana cha kusema kwa mambo yanayohusu maisha yao na maisha ya waumini kwa sababu tu ni viongozi wa dini. Hapana kama wanaona kuna jambo fulani wana wajibu wa kusema/kuchangia katika kutafuta utatuzi wa tatizo linalojitokeza.

Kwa upande mwingine, viongozi wa dini hawapaswi kujihusisha 'party politics' na ni kwa hapa tu tunaweza kusema "wasichanganye dini na siasa" - mfano kuegemea chama kimoja na kupiga kampeni dhidi ya chama au vyama vingine.

Kwa bahati mbaya, wakosoaji wengi wa viongozi wa dini hawawakosoi kwa hili, bali kwa mchango wao katika utatuzi au ufumbuzi wa migogoro inayojitokeza nchini - wakati na wao wanalipa kodi na kama ni uwekezaji usio na tija ukifanyika utawaathiri hata wao.

Kwa hiyo, ni haki yao kwa mujibu wa Ibara 18 ya Katiba kutoa maoni na kueleza mawazo yao na kufanya hivyo siyo kuvunja sheria za nchi na wala siyo "kuchanganya dini na siasa".
 
Akichangia Mjadala Katika Kipindi cha Minzani Kilichorushwa mubashara na TBC Kilichowajumuisha pia Shehe Salim Aliyekuwa Shehe mkuu Wa Dsm, Hamadi Rashid M/kiti Wa ADC na Mkongwe Steven Wasira.

Askofu Kilaini Amesema Si vyema Viongozi wa Dini Kutumia Mimbari Ukiwa bado umevaa Cheo chako au Joho lako la kichungaji Kuhubiri Siasa hasa Ukiwa Una Tiketi ya Chama fulani.

Lakini ni Wajibu Kamili Kukemea Uvunjivu Wa Maadili,Kutetea Uadilifu kwa wananchi na Hasa hasa Viongozi kwa Maslahi Mapana ya Wote kwenye nchi.

Nalo hilo muende mkalitazame!
Maadili na Utawala bora......mwisho wa Kunukuu
 
Hiyo TBC bado inarusha matangazo yake? Kwa jinsi hiyo TV ya umma ilivyojigeuza kipaza sauti cha CCM, huwa nasikia kinyaa hata kuitazama.
 
Mambo ya Waraka haikuwa ajenda..!

Aligusia dhana nzima Ya Kiongozi Wa Dini Kutumia Mimbari kwa Minaajiri ya Kunufaika..!

Akasema ikifikia hapo basi Vua joho Lako Hamia Kwenye Siasa..!

Akasema Pia Viongozi wa Dini Wasiache kbs, Wapaze Sauti Pale Viongozi wenye dhamana Wanapokengeuka ili Taifa Na Mali Zake Zibaki Salama....!
Sasa kwanini viongozi wa dini wakikemea uovu mnawafunga midomo kisa wao sio wanasiasa?

Kama mnawakubali mpaka kuwaita viongozi wa dini, kwanini tena mnawalazimisha wavue majoho ili kuwakemea? hamuoni wakivua majoho hawatakuwa tena viongozi wa dini?

Nani aliyewapa wanasiasa haki ya kusema hapa Tanganyika zaidi ya wengine?

Mambo ya siasa ni yapi na mambo mengine ni yapi ili tuyatenganishe tuone kama yapo mambo ambayo ni ya wanasiasa pekee yasiyowahusu wanajamii wengine?

Huu ujinga wa wanasiasa kujiona kundi maalum, lisilotakiwa kukemewa hata kwa mabaya wanayofanya wakiwa siasani unatakiwa ukome, tena ufie mbali kabisa, hii Tanganyika ni yetu sote, wanasiasa na wasio wanasiasa.

Ndio maana huyo Kilaini amealikwa hapo TBC kwa sababu ya huo ujinga aliozungumza, angekuwa na mawazo huru asingealikwa hapo, kitendo cha kukaa meza moja na Hamad Rashid amejishushia heshima sana.
 
Back
Top Bottom