SoC03 Tutapata wapi viongozi bora wenye maadili?

Stories of Change - 2023 Competition

October 2pm

Member
May 2, 2023
31
28
Habarini wakuu!

Rushwa. Ufisadi, uhujumu uchumi na ubadhirifu wa mali za umma, ukandamizaji na ubinyaji wa haki za binadamu ikiwemo uhuru wa vyombo ya habari,Upindishaji wa haki na sheria, matumizi mabaya ya vyombo vya dola, unyanyasaji na ukosefu wa usawa wa kijinsia miongoni mwa kero na madhila yanayofanyika katika nchi yetu. Yote hayo kwa pamoja huwekwa katika dhana ya ‘mmomonyoko wa maadili” ambacho ni kiini kikuu cha matatizo ndani ya jamii na nchi yetu. Mwanasaikolojia nguli wa Marekani Lawrence Kohlberg alifafanua maadili kama “chanzo cha mtu kitabia. Mchakato wa kufikiri wakati wa mtanziko wa kitabia ambao hutumika kuamua nini kilichochema na nini kilichokibaya, kisha matokeo ya tabia”

Maadili ni mafundisho ya kifalsafa au kisheria ambayo yanalenga kuwafanya watu kuwa na tabia njema, mienendo yenye kufaa ndani ya jamii kusudi waweze kuishi kwa pamoja na amani. Kwamba watu watende mambo Mema na kuacha mambo mabaya.

Maadili kama uadilifu, uwajibikaji, heshima, uchapakazi, ukarimu, na uzalendo ndani ya jamii chanzo chake ni;
  1. Taasisi ya Ndoa, Familia.
  2. Taasisi za Elimu kama shule na vyuo
  3. Taasisi za dini
  4. Serikali
Uimara wa taasisi hizo na serikali utaamua aina ya maadili ya jamii na taifa husika, Tanzania ili iweze kuwa na jamii yenye maadili haina budi kuhakikisha inaweka mazingira thabiti katika kuziwezesha taasisi hizo. Jamii na taifa huhitaji mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu ambacho kitakuwa sauti ya watu wengine, mwenye uwezo, nguvu, maono, ustadi na vipaji, na mamlaka ya kuwaongoza wengine kufikia malengo na maendeleo ndani ya taifa, hii inamaanisha kuwa kiongozi ni mwakilishi wa wengine, na uongozi ni uwakilishi, kuwa kwaajili ya wengine. Kiongozi lazima awe na fikra zenye maono ili kuweza kukabiliana na kutatua matatizo ya wananchi. Mwaka 1995, Baba wa taifa, Mwl. Nyerere alisema; “Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa Maono, ni umaskini mbaya sana” kauli ya Baba wa taifa inatuamsha na kutuongoza kuwa ili jamii iweze kutoka katika umaskini sharti iwe ni jamii yenye watu wenye maono, iongozwe na watu wenye fikra zenye maono.

Lakini Fikra zenye maono pekee yake hazitoshi, isipokuwa fikra zenye maono yenye uadilifu ambazo viongozi wa nchi yetu wanapaswa kuwa nazo. Hii inamaanisha hatuwezi kutenganisha uongozi na maadili mema ikiwa tunahitaji taifa lenye maendeleo na jamii yenye amani na furaha.

Lakini ni wapi wanapatikana viongozi bora? Tutawapata wapi?
Ni ukweli wa hakika kuwa kamwe viongozi hawatoki mbinguni, isipokuwa ndani ya jamii yetu. Hivyo jamii yenye maadili mema huzalisha viongozi wenye maadili mema. Bila kujali viongozi hao watapatikana katika mfumo upi, uwe mfumo wa kifalme au mfumo wa kidemokrasia ambapo watu wazima wenye akili kwa hiyari wanapata fursa za kuchagua kiongozi atakayewaongoza. Demokrasia inafaida nyingi mno, lakini demokrasia bila maadili haina maana yoyote ile. Kama jamii haina maadili mema bila shaka upo uwezekano mkubwa wa kuchagua viongozi wasio na maadili mema.

Hatuna budi kuzirejelea zile taasisi muhimu ambazo ndio msingi au kiini cha maadili ndani ya jamii. Kama ifuatavyo;
1. Taasisi ya Ndoa iboreshwe na kuimarishwa;
Familia ndio mzizi na kiini cha taifa. Familia ni chanzo kikuu cha maadili. Wazazi na Walezi wanajukumu la kuhakikisha wanalea watoto katika misingi ya maadili mema. Mwandishi wa kitabu cha Mithali katika biblia ameandika; “ Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee”(Mithali 22:6) Malezi ya watoto yalenga mambo yafuatayo;
  • Kuheshimu watu bila kuwabagua, namna bora ya kujiheshimu ni kuheshimu wengine,
  • Kufanya kazi kwa bidii, kuwafundisha stadi za maisha na kula kwa jasho lao mwenyewe.
  • Kuwa muadilifu, msafi na mwaminifu.
  • Kuwa jasiri, mzalendo na kupinga uovu na uhalifu.
  • Kuheshimu wakati hii ikiwa ni pamoja na kuwafundisha watoto jinsi ya kufanya mambo kwa wakati sahihi katika mazingira sahihi
  • Kusaidia jamii hasa watu wasiojiweza,
  • Kuwafundisha Elimu ya Fedha
1000_F_338195270_EdiuWa7o09BFAytVB8SsOR1N9jhBjJio.jpg

( picha kwa hisani ya tovuti ya adobe stock, google)
2. Kuboresha taasisi na mfumo wa Elimu.
  • Kuboresha mitaala na miongozo ya elimu kama kuweka somo la maadili ambalo litafundishwa kama somo.
  • Waalimu wawe mfano bora kwa kuwa na tabia njema kwa kufuata maadili ya kazi zao na kubeba wajibu kama walezi wa watoto.
  • Ziundwe Programu, matamasha ya kuhamasisha na kukuza maadili ya jamii.
  • Wazazi na waalimu wawe karibu na washirikiane. Wazazi wasiwaachie majukumu walimu.
regular_428313f8-84d6-4e24-9f96-6e5b392f25d7.jpg

(Picha kwa hisani ya google)
3. Taasisi za Dini
  • Yatolewe Mafundisho ya dini kwa watoto yanayolenga kuchukia tabia mbaya
  • Kila dini iwe na program za kuwafunza watoto somo la dini na maadili kama ilivyo kwa Wakatoliki Kupitia Sunday Schools, na kwa waislam Kupitia Madrasa.
  • Viongozi wa dini wote wawe na vyeti vya taaluma na uthibitisho kutoka kwenye mamlaka za serikali.

lrqGw8oyhHMadrassa.PNG

( Picha kwa hisani ya google, watoto wakiwa madrasa wakifundishwa elimu ya dini)
images

(Picha kwa hisani ya Google, watoto wakiwa kanisani wakifundishwa elimu ya dini)
4. Serikali
  • Iundwe Katiba Mpya inayoendana na wakati na mazingira ambayo itawafanya watu wote kuwajibika bila kujali ni kiongozi au sio kiongozi. Pasiwepo na kinga ya Rais au kiongozi yeyote. Hii itachochea uwajibikaji.
  • Vyombo vya sheria, na vyombo vya dola na Vyombo ya habari viwe huru pasipo kuingiliwa kimajukumu.
  • Seriksli idhibiti uhusika wa watu mashuhuri wenye maudhui yanayoharibu maadili ya jamii.
  • Pawe na dhamira ya dhati na Adhabu kali katika kupambana na Wala Rushwa, wahujumu uchumi na Wauza madawa ya Kulevya
  • Serikali itoe elimu na kuhamasisha jamii kuwa na maadili mema.
1965NyerereandKarumeinDaresSalaamAiport.jpg

(Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kushoto, na Abeid Karume wanakumbukwa kwa kusisitiza maadili ya viongozi na jamii kwa ujumla, picha kwa hisani ya google).

Maadili mema ni muarobaini katika kutatua matatizo mengi katika nchi kama ifuatavyo;
  • Kuchochea Maendeleo kutokana na kuwa na viongozi bora na jamii yenye kuwajibika.
  • Kupungua kwa Vitendo vya uhalifu na jinai kama ufisadi, rushwa, utapeli, makosa ya mtandaoni, uzaji wa madawa ya kulevya, jamii ikiwa na maadili hata uhalifu unapungua
  • Kutatua tatizo la ajira, kwani vijana watakuwa wachapakazi bila kubagua kazi, viongozi watatengeneza fursa za ajira kwa vijana na wanawake kwani ni sehemu ya wajibu wao.
  • Itachochea utawala bora unaoheshimu haki za binadamu. Jamii nayo itaishi kwa kuheshimiana huku ikifuata utawala wa sheria pasipo kujichukulia sheria mkononi.
  • Itaboresha huduma za kijamii, watumishi wa umma watakuwa na maadili ya kazi, malalamiko ya kuchelewa kazini au kuwatolea lugha chafu wananchi yatapungua kabisa. Huduma bora za upatikaniji wa haki kwenye vyombo vya dola na mahakamani itaifanya jamii iishi kwa amani.
Hivyo ndivyo tutakavyoweza kupata viongozi bora wenye maadili kwa ajili ya kujenga taifa bora lenye maendeleo ya kweli.

Karibuni kwa mjadala, Kura yako ni Muhimu. Ahsante!
 
1. Wizi wa Kura, utekaji na mauaji, uhujumu uchumi ni moja ya athari Mbaya inayotokana na viongozi kutokuwa n maadili.
 
Unaweza kuelezea kisa chako, nini kiliwahi kukutokea ulipoenda Kupata huduma labda ya afya hospitalini? Je watumishi uliowakuta walikuwa waadilifu?
 
Mada ni nzuri. Swali langu👉👉 Nani anaamua kuwa haya ni Maadili Mema na haya sio Maadili Mema? Vigezo gani vinatumika?
 
Mada ni nzuri. Swali langu👉👉 Nani anaamua kuwa haya ni Maadili Mema na haya sio Maadili Mema? Vigezo gani vinatumika?

Kama nilivyoeleza kwenye taasisi zinazoweza kuwa chanzo na wasimamizi wa malezi na Maadili ambazo ni Familia(wazazi), Taasisi za Elimu na Dini pamoja na serikali. Ndio zinaweza kuamua haya ni Maadili Mema Kwa kuyatofautisha na Maadili mabaya.

Noamba unipigie Kura.
 
Viongozi kuwa na uadilifu na Maadili Mema itawapa faraja n kuwahamasisha wananchi kuipenda nchi Yao na kuwa na uzalendo.

Wananchi wanakatishwa tamaa na kukosa Ari ya kuipenda nchi Yao pindi wakiona viongozi wakiwa sio waadilifu, Ufisadi wa mabilioni ya Pesa inachangia pakubwa kuzorotesha Imani ya wananchi Kwa serikali.
 
Kama nilivyoeleza kwenye taasisi zinazoweza kuwa chanzo na wasimamizi wa malezi na Maadili ambazo ni Familia(wazazi), Taasisi za Elimu na Dini pamoja na serikali. Ndio zinaweza kuamua haya ni Maadili Mema Kwa kuyatofautisha na Maadili mabaya.

Noamba unipigie Kura.

Unajua kuwa Maadili ya nchi moja yanaweza yasiwe Maadili ya nchi nyingine. Katika Ulimwengu wa utandawazi huoni kama hiyo inaweza kuwa changamoto.
Mfano, Kwa mfano mapenzi Kwa jinsia moja Kwa baadhi ya nchi sio maadili mazuri Wakati nchi zingine ni Maadili. Hii unazungumziaje? Ndio maana nikakuuliza ni vigezo gani vinatumika kuamua hayo Maadili. Hujanijibu.
 
Unajua kuwa Maadili ya nchi moja yanaweza yasiwe Maadili ya nchi nyingine. Katika Ulimwengu wa utandawazi huoni kama hiyo inaweza kuwa changamoto.
Mfano, Kwa mfano mapenzi Kwa jinsia moja Kwa baadhi ya nchi sio maadili mazuri Wakati nchi zingine ni Maadili. Hii unazungumziaje? Ndio maana nikakuuliza ni vigezo gani vinatumika kuamua hayo Maadili. Hujanijibu.

Maadili katika jamii yetu msingi wake mkuu ni Mila na desturi zetu kama Watanzania, na Mila na desturi zinasimamiwa na Familia na koo tulizotoka, nje ya Mila n desturi pia tuna dini km Ukristo na uislam ambao tunapata miongozo ya kimaadili kupitia imani.

Serikali nayo inanafasi yake kubwa katika kusimamia Maadili, mfano wa mapenzi ya jinsia moja Kwa nchi yetu ni Kosa kisheria Kwa mujibu wa Katiba yetu kwani haruhusiwi kumuingilia mtu kinyume na maumbile, pia dini, Mila na desturi zetu haziruhusu Jambo Hilo.
 
Ripoti ya CAG itakuwa na maana gani ikiwa hakuna uwajibikaji?
Uwajibikaji NI sehemu ya maadili. Kam viongozi wanashindwa kuwajibishana kumaanisha wanalindana, je wananchi watakuwa na Imani na serikali Yao? Kamwe Hilo halitowezekana.
 
Maadili katika jamii yetu msingi wake mkuu ni Mila na desturi zetu kama Watanzania, na Mila na desturi zinasimamiwa na Familia na koo tulizotoka, nje ya Mila n desturi pia tuna dini km Ukristo na uislam ambao tunapata miongozo ya kimaadili kupitia imani.

Serikali nayo inanafasi yake kubwa katika kusimamia Maadili, mfano wa mapenzi ya jinsia moja Kwa nchi yetu ni Kosa kisheria Kwa mujibu wa Katiba yetu kwani haruhusiwi kumuingilia mtu kinyume na maumbile, pia dini, Mila na desturi zetu haziruhusu Jambo Hilo.

Anyway
 
Back
Top Bottom