Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Kumbe muda wote CHADEMA mnaongozwa na katibu jini. Pole Mbowe 😱
 
ASKOFU GWAJIMA AMJIBU DR. SLAA, AMEONGEA NA WAANDISHI WA HABARI:

Gwajima anaonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu kustaafu kwake siasa.
Gwajima: Kama Dr. Slaa anakuja aje atokee hapa akane aone mambo ya mshenga yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.
Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe rose garden. Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. Alisema ameshawaambia watu yeye atakuwa first lady, siku iliyofata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.
Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi tena. Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hiy sio kwa kumuone Slaa mbaya. Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea milele.
Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.
Mchungaji Max: Ilifika mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo, yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. Mpaka juzi nilikuwa nawasiliana nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi kuchomoka.
Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa mkewe, Dr tumeshampoteza.
Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia, nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi kuona mambo haya. Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini, mashetani yalikuwa yanamrudia.
Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna tatizo limetokea.
Slaa Serena alisema kwenye mkutano wa CHADEMA watu waliletwa na malori na mabasi, mlioenda mjiulize ni kweli? Mtu anaesema uongo wa mchana, anasema Gwajima anasema maaskofu wa katoliki wamepewa hela. Kanisa katoliki ndio kanisa credible sana duniani.
Kwanini Slaa amesema! Kwanza kuwaondolea credibility, maaskofu hawa wamemsomesha, leo maaskofu 30 anawasingizia. Kwa mtu unayemuamini Slaa unaweza kusema anasema kweli lakini nimekuonyesha mazingira kwanini!
Anatukana maaskofu wa protestant na katoliki, nani aliyemtuma! Slaa aliulizwa unalindwa na usalama wa taifa? Alisema kweli, watu wa usalama wanambeba kwenda Serena, Azam na Star Tv kutukana maaskofu. Maaskofu hawaruhusiwi kujihusisha na siasa lakini ni wapiga kura, Je, atakupa kura! Je waumini wao watakupa kura! Strategy hii imeshindikana wafikirie nyingine. Bahati mbaya hii ilikuwa silaha yao ya mwisho.
Mababa askofu wa kanisa katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa, anasema nilikuwa nazunguka kwenye ndege na Lowassa. Mimi nina ndege yangu na siombi kibali kuzungumza mtu.
Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie ndio mnatukana maaskofu, usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee na kampeni zake kwa amani.
Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha, nitasema Slaa alivyokutana na watu wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama mtapomuongoza tena huyo mtu wenu wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na macho yenu hamtafungua tena
Uadalifu wa Slaa
Gwajima: Alisema baba askofu lazima mtubu, najiuliza yeye ni msafi kuliko sisi? Slaa aliacha wito ambalo ni tatizo tayari, zaidi ya kuacha wito ukaoa! Nikija tena nitaleta watoto aliowazaa na uhusiano wa yeye kutoka. Ukaa na mke na watoto ukatelekeza, haitoshi ukaenda kuoa mke wa mtu mwingine. Kamili akaweka zuio mahakamani.
Slaa alisema Ridhwani nauza madawa ya kulevya, leo Slaa ndio anao aliowasema, anaemuongoza Slaa akome na akome kabisa. Watu wa usalama kazi yenu ni kulinda nchi iwe na amani na sio kuichafua.
Kinachosumbua ni wakati na majira, 20 BC kabla ya kristo kulikuwa ana mtu aliehubiri ubudha, akaijaza Ubudha kwa sababu yalikuwa majira yake. Baada ya hapo, karne ya kwanza alitokea Yesu kristo na kukutana na upinzani wa ajabu, ukifika wakati wakisema wamemkamata.
Kweli ukiizika ina tabia ya kufufuka na ukiizika haiwezi kufa tena, akaja kutokea Mtume Muhammad japo alipata upinzani mkubwa leo Uislam umeenea sana. Nami niseme mfuate majira, msishindane nayo. Tanzania ni kubwa kuliko watanzania.
 
kueni makini wakristo kama maaskofu wenu wanawarekodi mkiwa kwenye maongezi ya faragha,mmekwisha....

...gamba umekua mdogoo siri zenu na vikaragosi vyenu zote nje.!
 
Slaa hana uzoefu na ndoa, na hiyo itamcost milele, tunda la mti wa kati sio la kuanza nalo ukubwani, linataka experience!
Sasa experience itatokea wapi na yeye alikua utawani? Ndio ishatokea tena hivyo.
 
Mkuu hujaona thread zingine juu ya hili jambo?
 
Tulia dawa ikuingie leo.
HUU NI WAKATI WA UWAZI NA UKWELI.

Wao walianza na sasa ni zamu yao kumalizia.

Na ni ujinga sana kusema eti Siasa isizungumzwe na viongozi wa dini.. Siasa bila dini inakosa maadili na itakua ni kiama, uwepo wa dini katika siasa unafanya kupunguza chuki na uadui
kweli, maana hata Dr. Josephine kasema amestaafu siasa halafu anaitisha mikutano ya kisiasa! Acha watu waongee huu ni mwaka wa uchaguzi inabidi kila anayetaka uongozi ajadiliwe hadi kwenye ngazi ya familia.
 
'SHISHINJEMU' wana wazimu bila shaka,huyo mtawa wao mbna kakimbilia marekani kwenda kutafuna 'mihogo' alopewa na nduguze alikotoka?,slaa 'mfitini' na 'mrubuni' kama alivyofitini ndoa ya watu na alivyojaribu kuwarubuni wana UKAWA ili waparanganyike.hila zote zinashindwa kwa jina la mwenyezi MUNGU na ukawa WATASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA NA HAKUNA RAIS ALOWAHI KUSHINDA KAMA ITAKAVYOKUWA.samahani lakini,ni ukweli tu.
 
TanzaniaDaima litaandika :
GWAJIMA AWAACHA WATANZANIA MIDOMO WAZI, AMKAMUA DR SLAA KWEUPE .

Mawio litaandika :
DR SLAA AVULIWA NGUO NA GWAJIMA.

Mwanahalisi:
KICHWA CHA DR SLAA, DEREVA WAKE NI MKEWE - GWAJIMA.

Uhuru???
 
Nimesikia mengi naona hii nchi ni maskofu ndio wamekua wavurugaji na wazia v kama ingelikua mashekhe ndio wanafanya hivi leo vyombo vyote na magazti yangelikua yanandika kuusu waislam kuibgilia maswala ya siasa na . Kuitwa udini
Leo naona tunakua tunapangia urais na viobgozi wanaojiita maskofu maraprotestant mara katolik
Waislam naona borana nyie mzinduke sijawaikuona hali hii kwa mashehe hata siku moja toka nipate ufaham ndani ya nchi yangu

...baada ya vikaragosi vyenu kuachwa uchi ss mnatoa mipovu tu.!
 
only in tanzania mtu mwenye kesi mahakamani anaweza kufanya haya. Nchi ya ajabu sana hii!

only in tanzania, ambapo msanii amepigwa marufuku na baraza la sanaa lakini rais anatengue adhabu na msanii kupiga showwwww kama kawaidaaa.

😂😂😂😂
 
yale anayo yaongea dr slaa juu ya mtu. Hayo ndio sio upumbavu? Mwiba utokea ulipo ingilia ndugu.

Wacheni dr. Apewe vidonge vyake. Yeye sindio anajidai mtakatifu kuliko wote sasa amekutana na mtoto wa mjini. Anapewa za uso.

hahahahaha! mkuu umenichekeshaje! mwaka huu CCM lazima wapoteane.
 
Kila moja anatoa tuhuma then anasema aje nimbomoe tena. Movi linaendelea. Wapiga kura tuna kazi mwaka huu
 
ccm inahusikani nini hapo sasa
Ndio waliomtuma Dr. Slaa aropoke. Ushahidi ni kada wa CCM Mwakyembe aliekuwepo na Dr. Slaa hotelini chumbani muda mchache kabla ya slaa kuanza kutema pumba!!
 
Alikuwa ni rafiki wa Lowassa tangu akiwa CCM. Kwenye mkutano wa kutangaza nia wa Lowassa, Gwajima alienda. Mbona hapo hujasema km alikuwa anajihusisha na CCM?

Hahahaaa gwajima anafata pesa popote ilipo yupo
 
Back
Top Bottom