Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Gwajima amedhihirisha ushenga wake kwa kumtukana muuliza swali.
 
toka lini gwajima anawaheshimu maaskofu wa kanisa katoriki au anasahau yeye ndie alimtukana baba askofu kadinali Pengo, halafu anajifanya anajua sana maana ya ndoa lakini anasahau yeye ni mtuhumiwa wa kuivunja ndoa ya Flora Mbasha bahati mbaya waandishi huwa wanaenda kama masanamu wanashindwa kuuliza maswali

Waandishi nao wananunuliwa labda ndio maana wanashindwa kuuliza maswali ya hivi.
 
toka lini gwajima anawaheshimu maaskofu wa kanisa katoriki au anasahau yeye ndie alimtukana baba askofu kadinali Pengo, halafu anajifanya anajua sana maana ya ndoa lakini anasahau yeye ni mtuhumiwa wa kuivunja ndoa ya Flora Mbasha bahati mbaya waandishi huwa wanaenda kama masanamu wanashindwa kuuliza maswali

Sikiliza vizuri ile clip ya Gwajima, hakutukana wala kuwadharau maaskofu wa katoliki bali alisema kuhusu Pengo peke yake kwa kwenda kinyume na makubaliano ya maaskofu. Mkuu usitugawanye kidini
 
Slaa katekwa na Josephine...
Mkuu hatuwezi kuanzisha RESCUE TEAM tukaenda pale nje ya geti lao tukapiga kambi kujaribu kumuokoa huyu mzee aisee? si vizuri kumuacha anapotea hivihivi mchana kweupe
 
watanzania ndoa ya dr slaa sie haituhusu, hayo ni mambo binafsi na kujadili mambo binafisi ya mtu kwenye social media ni upumbavu uliokithiri kila mtu anamapungufu yake kwenye ndoa yake. HAPA KAZI TU.
 
toka lini gwajima anawaheshimu maaskofu wa kanisa katoriki au anasahau yeye ndie alimtukana baba askofu kadinali Pengo, halafu anajifanya anajua sana maana ya ndoa lakini anasahau yeye ni mtuhumiwa wa kuivunja ndoa ya Flora Mbasha bahati mbaya waandishi huwa wanaenda kama masanamu wanashindwa kuuliza maswali

Maskofu wako wangapi kwani?
 

Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia, nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi kuona mambo haya. Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini, mashetani yalikuwa yanamrudia.

Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna tatizo limetokea.


Jamani hii ya kutoa siri za matatizo ya WAUMINI linaondoa kabisa credibility ya hawa wachungaji.
 
Kumshambulia mtu on personal issues, ni dalili ya udhaifu wa mtu!
Mchungaji kabugi saaaanaaaaa.

Mkuu inabidi tuwe objective...

Juzi niliongelea Slaa "kulipua" watu zaidi ya issues....nilionekana mjinga kwa pro-CCM

Alimgusa Gwajima pia km mtu hivyo nae ana haki kujibu..

Ujinga huu hauwezi kukoma mpk wote tukubali kuacha ujinga wa kutaka kusikia issues za kijinga.....tukiziendekeza kwa sababu zinatupendeza na kuonekana kuiegemezea mizani upande wetu, basi tukubali na za kijinga zinazoelekezea mizani zaidi upande wa wenzetu
 
Ndugu watanzania wote ungana nami kwa Taarifa za Uhakika kutoka katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Askofu Gwajima sasa hivi.

Vituo vya TV vilivyoko hewani ni Channel 10 na Sibuka TV

More updates to follow!

12:28 PM
Waandishi wa habari waliofika mpaka ni kutoka:
Radio:
BBC, DW, RADIO ONE, CLOUDS FM, EAST AFRICA RADIO, WAPO RADIO na E-fm

Television:
Clouds Tv, Channel 10, Mlimani Tv, EA TV na Sibuka Tv

Bado waandishi wanaingia kwa wingi!

UPDATE
Askofu Gwajima ameshafika hapa Landmark Hotel, wageni na waandishi wanamsubiri Ukumbini
=========

Gwajima anaonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu kustaafu kwake siasa

Gwajima: Kama Dr. Slaa anakaja aje atoke hapa akane aone mambo ya mshenga yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.

Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe rose garden. Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. Alisema ameshawaambia watu yeye atakuwa first lady, siku iliyofata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.

Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi tena. Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hio sio kwa mumuone Slaa mbaya. Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea milele.

Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.

Mchungaji Max: Ilifika mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo, yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. Mpaka juzi nilikuwa nawasiliane nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi kuchomoka.

Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa mkewe, Dr tumeshampoteza.

Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia, nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi kuona mambo haya. Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini, mashetani yalikuwa yanamrudia.

Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna tatizo limetokea.

Slaa Serena alisema kwenye mkutano wa CHADEMA watu waliletwa na malori na mabasi, mlioenda mjiulize ni kweli? Mtu anaesema uongo wa mchana, anasema Gwajima anasema maaskofu wa katoliki wamepewa hela. Kanisa katoliki ndio kanisa credible sana duniani.

Kwanini Slaa amesema! Kwanza kuwaondolea credibility, maaskofu hawa wamemsomesha, leo maaskofu 30 anawasingizia. Kwa mtu unaemuamini Slaa unaweza kusema anasema kweli lakini nimekuonyesha mazingira kwanini!

Anatukana maaskofu wa protestant na katoliki, nani aliemtuma! Slaa aliulizwa unalindwa na usalama wa taifa? Alisema kweli, watu wa usalama wanambeba kwenda Serena, Azam na Star Tv kutukana maaskofu. Maaskofu hawaruhusiwi kujihusisha na siasa lakini ni wapiga kura, Je, atakupa kura! Je waumini wao watakupa kura! Strategy hii imeshindikana wafikirie nyingine. Bahati mbaya hii ilikuwa silaha yao ya mwisho.

Mababa askofu wa kanisa katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa, anasema nilikuwa nazunguka kwenye ndege na Lowassa. Mimi nina ndege yangu na siombi kibali kuzungumza mtu.

Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie ndio mnatukana maaskofu, usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee kampeni zake kwa amani.

Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha, nitasema Slaa alivyokutana na watu wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama mtapomuongoza tena huyo mtu wenu wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na macho yenu hamtafungua tena

Uadalifu wa Slaa
Gwajima: Alisema baba askofu lazima mtubu, najiuliza yeye ni msafi kuliko sisi? Slaa aliacha wito ambalo ni tatizo tayari, zaidi ya kuacha wito ukaoa! Nikija tena nitaleta watoto aliowazaa na uhusiano wa yeye kutoka. Ukaa na mke na watoto ukatelekeza, haitoshi ukaenda kuoa mke wa mtu mwingine. Kamili akaweka zuio mahakamani.

Slaa alisema Ridhwani nauza madawa ya kulevya, leo Slaa ndio anao aliowasema, anaemuongoza Slaa akome na akome kabisa. Watu wa usalama kazi yenu ni kulinda nchi iwe na amani na sio kuichafua.

Kinachosumbua ni wakati na majira, 20 kabla ya kristo kulikuwa ana mtu aliehubiri ubudha, akaijaza Ubudha kwa sababu yalikuwa majira yake. Baada ya hapo, karne ya kwanza alitokea Yesu kristo na kukutana na upinzani wa ajabu, ukifika wakati waksema wamemkamata.

Kweli ukiizika ina tabia ya kufufuka na ukiizika haiwezi kufa tena, akaja kutokea Mtume Muhammad japo alipata upinzani mkubwa leo Uislam umeenea sana. Nami niseme mfate majira, msishindane nayo. Tanzania ni kubwa kuliko watanzania.

Mimi simuelewi kabisa huyu Gwajima, sasa yy ni mchungaji/au ni kada wa Chadema, anaongea mambo ya kisiasa kabisa na kutetea hija za kisiasa wakati yeye ni mtu wa dini, au ndo ametumwa na CHADEMA katika harakati za kuzima hoja za Slaa, anajimaliza kabisa kiroho, na wala waumini wenye uelewa wasigeweza kumuamini tena....ya kaisari mwachie kaisari na ya Mungu ampe Mungu
 
nyie kama mnapata muda wa kufuatilia watu wapuuzi kama akina gwajima kazi za kuwapatia kipato mnazifanya saa ngapi?

Kwan ww ulivyokuwa unamshobikea Padre Slaa kwani huwa anakufanya nn?
 
mkutano wa gwajima waandishi wameonekana kumshangilia Lowasa na kuamua kumzomea muuliza swali ambaye hakupangwa pale alipombana gwajima! Huyu mtu analitakia nini taifa hili?
 
Back
Top Bottom