Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

imebainika kuwa ALIYEPANGA DEAL LA KUMUINGIA SLAA KWA KUPITIA JOSEPHINE NI ....BERNARD MEMBE ...NA KUWAPA TISS ROADMAP NI MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI

HII IMEONESHA UWEZO DUNI KABISA WA KIMIKAKATI WA MEMBE KWA MARA NYINGINE ...,AMBAO UNAMUAHAEIBIA MAGUFULI
 
uchaguzi uliogubikwa na udini.
Padri mstaafu vs Askofu gwajima.
mmoja anadaiwa kuchepuka, mwingine 'mshenga' wa mwanasiasa.
Viongozi wa dini katikati ya vijembe vya siasa za uchaguzi.
Maneno wnayoongea ni vizuri tuanze kuwakagua
viongozi wetu wa dini. Ni kweli hicho wanachohubiri ndio wanachomaanisha?
Ni zamu ya viongozi wa dini ndani ya ulingo wa siasa.
 
gwajima ana cheo gani chadema?
kwanini ni maaskofu tu ndo wanajiingiza kwenye siasa, na hatusikii masheikh na maimamu? what wrong kwenye ukristo?

..magamba akili zenu nyeusi sn;yani mnakituma kikaragosi chenu kikamseme Gwajima mkaona poa tu..ila Gwajima kuja kukijibu kikaragosi chenu...eti ooh kwann maaskofu wanajiingiza kwenye siasa? hamjui akili zenu fupi uko ugambani ndio chanzo.? siku nyingine msikitume kikaragosi muone km kuna mtu atahangaika na nyie.!
#zerowahed!
 
Tatizo ni JK. Alipaswa kuwa mkali kidogo. Ameshusha hadhi ya urais na mamlaka zote za serikali. Yaani yeye kila kitu ni kucheka tu na kugawa vyeo kwa marafiki zake. Matokeo yake ndo haya sasa. Huwezi kujua yupi ni yupi na nchi inakwenda tu kama boya. Rais ajaye atakuwa na kazi kubwa kurudisha hadhi ya taasisi ya urais na taasisi nyinginezo za nchi. Hovyo kabisa!

Maneno juu ya usalama wa wa taifa ni makali mno harafu hajasema anawalipua na bomu gani tunakoelekea sio kuzuri kama taifa.
 
Kidogo kidogo anaweza kutoka na 'ubunge' wa kuteuliwa huyu Askofu, ameonyesha nia ya upambanaji wa dhati na ana kundi kubwa analoongoza.

"UKAWA" wamecheza pele kumshawishi huyu bwana ili awashawishi viongozi wa dini. Pengo tu ndiye walitofautina
 
Ivi hawa takokuru wanafanya kazi gani nasikia rushwa rushwa wausika awakamatwi wamuajili dk slaa awasaidi sasa hana kazi
 
Hiyo msg aliylionesha inasomekaje?
Issue ya ushenga kasemaje?
Kwahiyo kumbe Slaa ni muongo hakuambiwa na Gwajima kuhusu maaskofu kuhongwa.
Gwajima mbona anaongelea zaidi ndoa ya Slaa kuliko hoja?
Gwajima ana uzoefu na ndoa ni Askofu na ameoa mbona yeye ni muasherati pia? (hili nina ushahidi ndio maana nimeandika)
 
gwajima ana cheo gani chadema?
kwanini ni maaskofu tu ndo wanajiingiza kwenye siasa, na hatusikii masheikh na maimamu? what wrong kwenye ukristo?

Gwajima si anajulikana mpiga dili kitambo tu!?

Kashfa kashfa pia ,,, Gwajima hamna kitu yule.
 
Ivi Dr. wa MIHOGO aliamua kuoa kwa sbb gani?
 
Jamani alichokisema Gwajima ni kua Dr. Slaa hajajiuzulu kwa sababu ya ujio wa Lowasa bali ni shinikizo toka kwa mkewe na ndicho alichofafanua Askofu Gwajima na ndio maana akaonyesha na sms aliyotumiwa na Slaa kua anaachana na Siasa.
 
Yan ni bora dr slaa aliona aende nje mapema, angeiweka wap aibu hii!
 
Huu uchaguzi strategy zinazotumika si mchezo-Lowassa yuko background halafu wapambe,s are leaving no stone unturned- Kubenea nae mbeya kamaliza kabisa Mwakyembe-yaani CCM sijui watapenya vipi- yaani kama tuko mamtoni vile

Mwana nipe link ya kubenea kummaliza Mwakyembe
 
Ndugu watanzania wote ungana nami kwa Taarifa za Uhakika kutoka katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Askofu Gwajima sasa hivi.

Vituo vya TV vilivyoko hewani ni Channel 10 na Sibuka TV

More updates to follow!

12:28 PM
Waandishi wa habari waliofika mpaka ni kutoka:
Radio:
BBC, DW, RADIO ONE, CLOUDS FM, EAST AFRICA RADIO, WAPO RADIO na E-fm

Television:
Clouds Tv, Channel 10, Mlimani Tv, EA TV na Sibuka Tv

Bado waandishi wanaingia kwa wingi!

UPDATE
Askofu Gwajima ameshafika hapa Landmark Hotel, wageni na waandishi wanamsubiri Ukumbini
=========

Gwajima anaonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu kustaafu kwake siasa

Gwajima: Kama Dr. Slaa anakaja aje atoke hapa akane aone mambo ya mshenga yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.

Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe rose garden. Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. Alisema ameshawaambia watu yeye atakuwa first lady, siku iliyofata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.

Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi tena. Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hio sio kwa mumuone Slaa mbaya. Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea milele.

Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.

Mchungaji Max: Ilifika mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo, yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. Mpaka juzi nilikuwa nawasiliane nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi kuchomoka.

Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa mkewe, Dr tumeshampoteza.

Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia, nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi kuona mambo haya. Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini, mashetani yalikuwa yanamrudia.

Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna tatizo limetokea.

Slaa Serena alisema kwenye mkutano wa CHADEMA watu waliletwa na malori na mabasi, mlioenda mjiulize ni kweli? Mtu anaesema uongo wa mchana, anasema Gwajima anasema maaskofu wa katoliki wamepewa hela. Kanisa katoliki ndio kanisa credible sana duniani.

Kwanini Slaa amesema! Kwanza kuwaondolea credibility, maaskofu hawa wamemsomesha, leo maaskofu 30 anawasingizia. Kwa mtu unaemuamini Slaa unaweza kusema anasema kweli lakini nimekuonyesha mazingira kwanini!

Anatukana maaskofu wa protestant na katoliki, nani aliemtuma! Slaa aliulizwa unalindwa na usalama wa taifa? Alisema kweli, watu wa usalama wanambeba kwenda Serena, Azam na Star Tv kutukana maaskofu. Maaskofu hawaruhusiwi kujihusisha na siasa lakini ni wapiga kura, Je, atakupa kura! Je waumini wao watakupa kura! Strategy hii imeshindikana wafikirie nyingine. Bahati mbaya hii ilikuwa silaha yao ya mwisho.

Mababa askofu wa kanisa katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa, anasema nilikuwa nazunguka kwenye ndege na Lowassa. Mimi nina ndege yangu na siombi kibali kuzungumza mtu.

Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie ndio mnatukana maaskofu, usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee kampeni zake kwa amani.

Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha, nitasema Slaa alivyokutana na watu wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama mtapomuongoza tena huyo mtu wenu wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na macho yenu hamtafungua tena

Uadalifu wa Slaa
Gwajima: Alisema baba askofu lazima mtubu, najiuliza yeye ni msafi kuliko sisi? Slaa aliacha wito ambalo ni tatizo tayari, zaidi ya kuacha wito ukaoa! Nikija tena nitaleta watoto aliowazaa na uhusiano wa yeye kutoka. Ukaa na mke na watoto ukatelekeza, haitoshi ukaenda kuoa mke wa mtu mwingine. Kamili akaweka zuio mahakamani.

Slaa alisema Ridhwani nauza madawa ya kulevya, leo Slaa ndio anao aliowasema, anaemuongoza Slaa akome na akome kabisa. Watu wa usalama kazi yenu ni kulinda nchi iwe na amani na sio kuichafua.

Kinachosumbua ni wakati na majira, 20 kabla ya kristo kulikuwa ana mtu aliehubiri ubudha, akaijaza Ubudha kwa sababu yalikuwa majira yake. Baada ya hapo, karne ya kwanza alitokea Yesu kristo na kukutana na upinzani wa ajabu, ukifika wakati waksema wamemkamata.

Kweli ukiizika ina tabia ya kufufuka na ukiizika haiwezi kufa tena, akaja kutokea Mtume Muhammad japo alipata upinzani mkubwa leo Uislam umeenea sana. Nami niseme mfate majira, msishindane nayo. Tanzania ni kubwa kuliko watanzania.


UPDATE
Askofu Gwajima amemaliza Press Conference na waandishi wa habari na alipokua akiondoka na gari yake aina ya Hummer watu wengi wakijipanga kando ya barabara huku bodaboda wakimfuata kwa nyuma wakiimba kuwa yeye ni JEMBE na kumpigia makofi
Mbona hueleweki wewe na huyo Gwajima wenu,naona anaongelea tu safari zake na mke wake London sijui na mambo binafsi ya mke wakeDr Slaa,kama Gwajima ndio eti kajibu huo utumbo,ajibu ishu alizozisema Dr Slaa na sio hizo porojo za kilofa,IQ ya Gwajima ni zero ,eti halafu katoka na Hummer nini bana inasaidia nini kujibu makombora ya Dr Slaa,kwa akili hizo za kushabikia maadamu kasema mtu ambaye ni pro Lowassa bila hata kufikiria mnazidi kumpadisha chati mzee Mkapa,msiwe malofa wa kufikiri ndugu zanguni,nchi hii kamwe haitaendeshwa na genge la wahuni,Tanzania sio club ni nchi.
 
Hivi bado una muona Gwajima kwamba ni mchungaji,Kweli Shetani amekupiga upofu.Huyo ni mtumishi wa Shetani kabisa.Biblia inasema "mtawafahamu kwa matendo yao." Matendo ya Gwajima sio ya mtoto wa Mungu kabisa.Sina haja kuyataja, unayajua.Biblia inaongeza kusema,"tokeni kati yao mkatengwe na nao."Toka huko,utaishia jehanam.
Unatoa wapi ujasiri wa kumuita mchungaji kuwa ni mpuuzi? Hapo ulipo tu umeme wamekukatia
 
Back
Top Bottom