Askari ajitoa uhai kwa kuupoteza msafara wa Kikwete Tarime!!!

Hatutaki bla bla, jamii inahitaji ripoti kamili na siyo maelezo ya kupangwa.

Jamani, hasa waandishi wa habari hivi ni kwa nini mmsimuulize saidi mwema ni ripoti ngapi za Polisi mpaka sasa hivi ziko pending na hajiwekwa wazi, Je haoini kama na hii itakuwa vivyo hivyo?
 
Nasubiri kusikia hasa maelezo ya kwanini WP aliuawa - japo habari za awali zilisema ati amejiua. Polisi hawawezi kuchunguza hili inahitajika ofisi ya Tume za Haki za Binadamu kufanya hivyo au chombo kingine huru.



Sikiliza vizuri kile ambacho IGP Mwema anasema; halafu sikiliza kile asichokisema.
 
Last edited by a moderator:
IGP anaongea kama layman?? Huyu binti ameuawa tu lakini hawataki kusema ukweli. Kwa taarifa zilizopo ni kuwa walizozana na mkuu wake wa kazi na ktk mabishano mkuu wake wa kazi ndo alimpiga risasi Suzani na si kweli kwamba alijipiga risasi mwenyewe.
 
Kwa kanuni za polisi duniani kote ukishawekwa "under arrest" kama ilivyotokea kwa huyo mdada unakuwa "disarmed." Haingii akilini eti mtu
kawekwa lock up kaachiwa na silaha yake, hata kama alikuwa polisi.
 
Jasusi.. mkuu umemiss hapo... hakupijipiga risasi akiwa lock up.. kapigwa akiwa ofisini kwa mkuu wake, milango ikiwa imefungwa. Miye mtu wa kwanza kumtia pingu ni huyo mkuu.. maana ndio mtu pekee anayeweza kutuelezea mtu anaweza vipi kuijpiga risasi nne moyoni kabla hajafa.
 
Hivi wakati anaingia huko ofisini kwa mkuu, mkuu mwenyewe alikuwemo ndani? Au hakuwemo? Maana inaongelewa haisemwi kama mkuu alikuwa humo ofisini au la! Kinachosemwa tu ni kwamba alikimbilia huko na akafunga mlango na akapiga risasi akiwa huko ndani. Huko ndani ya ofisi alikuwa peke yake? Kama alikuwepo huyo mkuu wake mbona haisemwi hiii?
 
Aisee, hii ya kupigwa risasi makes sense tulishaleweshwa siasa za TZ, sasa two ways out either tumuombe Slaa alibebe maana Zitto kapoa, ama kama kuna namna junior police officers ama TAMWA ama Legal and Human Right Center watalivalia njuga jamani kwa hii nchi ilivyoharibika hakuna by standers, leo kwa mwenzako unaona jambo dogo kesho litakufika na wewe hebu watanzania tufike mahali tusema 'no more', for how long shall they kill our colleagues while we stand aside and look? are we saying its just a destiny?
 
Hivi wakati anaingia huko ofisini kwa mkuu, mkuu mwenyewe alikuwemo ndani? Au hakuwemo? Maana inaongelewa haisemwi kama mkuu alikuwa humo ofisini au la! Kinachosemwa tu ni kwamba alikimbilia huko na akafunga mlango na akapiga risasi akiwa huko ndani. Huko ndani ya ofisi alikuwa peke yake? Kama alikuwepo huyo mkuu wake mbona haisemwi hiii?

Babuyao.. hujasikiliza vizuri... zingatia hayo niliyoyabold ukisikiliza tena...
 
kuna siku Mungu atachukizwa na huu uonevu, atashusha gharika la ajali kwa viongozi wajuu wanaohusika na utoaji wa uhai/dhulumu haki za watu wasiokua na hatia.

Ee Mungu naomba uwape utu viongozi wetu wenye mamlaka, watende yaliyo ya haki kwa wale wanaowaongoza,,,AMEN.
mkuu bado hapa hujatusaidia namna ya kukomesha huu mtiririko wa matukio hasi kwenye jeshi letu
 
Hapa kuna kitu kikubwa kilikuwa kinataka kufanyika na kwa bahati mbaya kikaenda mrama sasa ili stori inoge/ieleweke kwa wananchi dada yetu kachukuliwa kapigwa zake za kifua stori imeishia hapo!!Nasikia kuna wazee wa "system" walishaapa mkulu hataongoza zaidi ya miaka 5!Ngoja tuone picha litaisha vipi??
 
Mie nafikiri BINTI aliwatolea uvivu. Makosa walifanya wao na wakataka kumtupia zigo mtoto wa watu.

Wakakuta NEW GENERATION siyo ma YES SIR kiasi hicho. Ukazuka ugomvi mkali sana na binti kusema "hakufanya makosa".

Jitu zima ovyo likachukia na likam-mwagia binti risasi.

Kama kawaida ya POLISI dunia nzima, MSHIKAMANO ni SHERIA.

Watamlinda mwenzao kwa udi na uvumba. Ndiyo maana wamezika harakaharaka.

Taratibu ukweli tutaupata. Habari zikizidi kuwekwa wazi, wataanza wenyewe kusema ukweli.
 
kwa nchi za wenzetu wana organisation zinaitwa INDEPENDENT POLICE COMPLAINTS COMMISSION etc hawa ndio wangechukua hii kesi na sio polisi au serikali kuunda tume ya uchunguzi,hio ni kesi ya ngedere hakimu nyani......
 
Hizi thread za huyu askari aliye jiuwa zingeunganishwa na kuwa moja tu.
 
Kifo cha polisi Tarime utata
Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 6th July 2010 @ 17:36


UCHUNGUZI wa awali wa Polisi kuhusu tukio la askari wa kike, WP Susan Kabanza (22), aliyejiua kwa sababu za kupoteza msafara wa Rais Jakaya Kikwete wilayani Tarime, mkoani Mara juzi, umeibua utata baada ya kudaiwa kuwa alitaka kuwaua wenzake kabla ya kujiua.

Hali hiyo ilidhihirika kwa kilichoelezwa kuwa, Susan baada ya kuamriwa na wakuu wake arejee eneo la kazi (kituo cha Polisi) baada ya kukosea kuongoza msafara, wakati akifanya makabidhiano ya zamu, alinyakua bunduki na kukimbilia chumba cha Mkuu wa Kituo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, Susan akiwa katika chumba hicho, alibana mlango kwa komeo na wenzake walipomtaka afungue huku wakigusa kitasa, alifyatua risasi moja mlangoni ikawakosa na wakati wakijiandaa kuvunja mlango walisikia risasi nyingine kutoka ndani ya chumba hicho.

"Walipofungua mlango, walikuta amejipiga risasi na ameshakufa na wakamchukua na kumpeleka hospitali, hii taarifa hata hivyo bado hatuna uhakika nayo na ndiyo sababu nimeunda Tume ya watu wanne kuchunguza tukio hilo," alisema IGP Mwema.

Alisema Tume hiyo yenye mwanamke mmoja, itaongozwa na Kamishna wa Operesheni, Paul Chagonja na itafanya kazi kwa wiki moja kuanzia leo, ili kubaini mambo makuu matatu, aliyoyataja kuwa ni kujua chanzo cha kifo, ukweli wa yaliyotokea na njia za kuepusha matukio ya namna hiyo.

Mwema alisema Tume hiyo itachunguza pia sababu ya askari mwingine Noel Njenga (33) aliyekuwa Chuo cha Polisi, Dar es Salaam, kujiua kwa risasi siku moja kabla ya Susan.

Mwema, ambaye awali aliwaambia waandishi kuwa Jeshi hilo lipo katika wakati mgumu wa majonzi na simanzi kutokana na vifo vya askari hao wawili, alisema baada ya wiki moja, ataweka wazi matokeo ya uchunguzi wa vifo hivyo, ili jamii ielewe kilichotokea maana yamesemwa mengi.

Miongoni mwa mambo yaliyosemwa na kuandikwa, ambayo waandishi walimtaka Mwema afafanue na kuwaeleza kuwa yatabainishwa baada ya matokeo ya Tume, ni pamoja na kuhusisha kifo cha Susan na makaripio ya maofisa wa Usalama wa Taifa, kuwekwa rumande na wakuu wake wa kazi na kauli za kuogofya dhidi yake.

"Kama alipatwa msukosuko wa wakuu wake wa kazi, au aliwekwa rumande kama baadhi yenu mlivyoandika, au hili nililoeleza kuwa alinyakua silaha na kukimbilia chumba cha mkuu wake wa kituo na kujipiga risasi baada ya kupiga moja mlangoni, itajulikana baada ya wiki hiyo moja," alisema Mwema.

Mwema akielezea mazingira ya awali ya kazi yaliyomsibu Susan kabla ya kifo chake, alisema siku hiyo askari huyo mwenyeji wa Mwanza, alikuwa zamu katika chumba cha mashitaka na kituo cha Polisi ambacho ni karibu na njia ulikokuwa unapita msafara wa Rais, ambapo wakuu wake wa kazi walimpanga kwenda kuelekeza msafara huo.

"Akiwa pale kuna njia panda, lakini zote zinakwenda Ikulu Ndogo kwa DC (Mkuu wa Wilaya), ulipofika msafara wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Mara, aliulizwa njia ya kwenda kwa Mkuu wa Wilaya, akawaelekeza nyingine na msafara wa Rais ambao ulikuwa unakwenda huko huko ulipofika eneo hilo, akauelekeza njia nyingine ndipo RPC mbele alipobaini wamepotezana," alifafanua Mwema.

Alisema baada ya RPC kubaini hilo, taarifa zilipelekwa kuwa askari huyo abadilishwe na aje mwingine kuchukua nafasi yake, kwa kuwa amekosea kuelekeza msafara na ndipo hilo lilipofanyika na yeye (Susan) kurejea kituoni kukabidhi zamu kwa wenzake.

"Akiwa kituoni, alifika askari Magereza na mtuhumiwa, hivyo kukawa na pilika za hapa na pale na unajua katika makabidhiano silaha ni miongoni mwa vitu vinavyokabidhiwa. "Ghafla wenzake wanasema walishangaa kuona amekimbilia chumba cha Mkuu wa Kituo akiwa na bunduki na ndipo alipofyatua risasi mlangoni na nyingine kujipiga pale alipotakiwa kufungua mlango kabla hawajauvunja, walipoingia ndani walikuta amekufa," alisema Mwema.

Hata hivyo alikiri kuwa taarifa hizo ni za awali, hivyo zinaweza zisiwe sahihi na ndiyo sababu ameunda Tume kuchunguza suala hilo kwa kuwa hata kauli za wakuu wake zinaweza kumsababisha kuchukua hatua hiyo, au hofu ama msongo wa mawazo, kutokana na hali ya maisha kiuchumi na kijamii.


 
Mie nafikiri BINTI aliwatolea uvivu. Makosa walifanya wao na wakataka kumtupia zigo mtoto wa watu.

Wakakuta NEW GENERATION siyo ma YES SIR kiasi hicho. Ukazuka ugomvi mkali sana na binti kusema "hakufanya makosa".

Jitu zima ovyo likachukia na likam-mwagia binti risasi.

Kama kawaida ya POLISI dunia nzima, MSHIKAMANO ni SHERIA.

Watamlinda mwenzao kwa udi na uvumba. Ndiyo maana wamezika harakaharaka.

Taratibu ukweli tutaupata. Habari zikizidi kuwekwa wazi, wataanza wenyewe kusema ukweli.


Sikonge, I think what you described here is exactly what happened.
 
Kama kawaida ya JF watu washatoa hukumu kabla ya hiyo tume kutoa taarifa ya uchunguzi wa ilo tukio la askari kujiuwa.
 
Back
Top Bottom