TANZIA Kahama: Mwenyekiti wa Wazazi (CCM) kata ya Ulowa ajiua kwa kujipiga risasi

uwe hodari

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
3,990
8,367
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ( CCM) kata ya Ulowa wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Safari Manjala amejiua kwa kujipiga risasi shingoni asubuhi ya leo.

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo chanzo chake hakijajulikana.

----
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limesema linaendelea na uchunguzi kufuatia tukio la Mkulima Safari Manjala mkazi wa kijiji Ilomelo Kata ya Ulowa katika Halmashauri ya Ushetu mkoani humo kujiua kwa risasi nyumbani kwake leo Septemba 8, 2023.

Akizungumza na GoldFM kamishna msaidizi wa polisi KENNETH MBWANO amewataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi na pindi wanapokuwa na changamoto ni vyema wakatafuta Ushauri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho Jeffason Ezekia, amesema kwa mujibu wa maelezo ya Ndugu wa marehemu, siku ya jana Marehemu alishiriki shughuli zake za kawaida ikiwemo maandalizi ya Vitalu vya mbegu za Tumbaku (Mabedi) kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo, kitendo cha kujitoa uhai alichokifanya leo majira ya saa 2 asubuhi kinaacha maswali juu kilichosababisha kujiua.

Jeffason ameongeza kuwa hatua nyingine za kiusalama zimechukuliwa ikiwemo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Ushetu ambalo limefika eneo la Tukio kwa ajili ya uchunguzi ikiwemo kuchukua silaha iliyotumiwa na marehemu na taratibu nyingine za kiuchunguzi.

ITV.png


Credit: ITV

--

Siku mbili baada ya mfanyabiashara maarufu wa tumbaku mkoani Shinyanga, Safari Manjala (54) kudaiwa kujiua kwa kujipiga risasi chini ya kidevu, inadaiwa marehemu alifikia hatua hiyo baada ya kufilisika.

Hata hivyo, Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kennedy Mgani alipoulizwa Septemba 9, 2023 na Mwananchi, alisema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Manjala ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Kata ya Ulowa wilayani Kahama, alijiua Septemba 8, 2023 saa mbili asubuhi baada ya kurudi kutokea kwenye shamba lake la miti kijiji cha Ilomelo, Halmashauri ya Ushetu.

Akizungumza kwa njia ya simu jana kaka wa marehemu, Mihayo Manjala alisema marehemu aliyekuwa akihudumiwa na chama cha msingi (Amcos) Iginhyabalimi, aliingiziwa fedha na kampuni ya Mkwawa siku tatu kabla ya kujiua na kuwalipa wakulima wake wote.

Baada ya kukamilisha malipo hayo kwa wakulima, alianza kulalamika kuishiwa fedha.

“Sijajua vyema lakini aliwalipa wakulima wake wote hela ikaisha, sikuongea naye tangu alipotoka kuwalipa wakulima wake. Marafiki zake waliniambia aliwapigia kuwaambia ana shida na hela,” alisema.

Alisema siku ya kuchukua hatua ya kukatisha uhai wake alipiga simu kwa Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani akitafuta namna ya kupata pesa, hata hivyo mbunge huyo alimwomba amsubiri atoke bungeni, lakini baada ya muda alichukua hatua ya kuondoa uhai wake.

"Muda mwingi marehemu alikuwa akilalamikia kukosa pesa, baada ya kulipwa na yeye kulipa madeni, hiyo inaweza kuwa sababu. Asubuhi alimpigia simu mbunge akimuelezea mambo ya hela, lakini hata nusu saa haikupita akajipiga risasi," alisema Mihayo.

Diwani wa Kata ya Ulowa, Pascal Mayengo alisema siku mbili kabla ya Manjala kujiua, alimweleza tayari ameshaanza kuandaa vitalu vya mbegu ya tumbaku.

“Kwenye maongezi yetu tulizungumzia changamoto ya kampuni ambayo tulifanya nayo biashara kuchelewesha malipo yetu, ila yeye alilipwa wiki moja ilizopita, watu wanajiuliza kwa nini amechukua hatua hiyo,

Nafikiri ni msongo wa mawazo, hali yake ya uchumi iliyumba kipato chake kwa mwaka kilikuwa Sh700 milioni hadi Sh800 milioni lakini mwaka huu alipata Sh160 milioni tu,” alisema.

Alisema kuna wakati mradi wa kituo cha mafuta ya mfanyabiashara huyo kiliacha kutoa huduma jambo ambalo lilimuumiza kichwa mfanyabiashara kutokana na mtikisiko huo wa kiuchumi.

Diwani huyo alisema baada ya kupata taarifa hizo, alimpigia Mbunge wa Ushetu kumuarifu tukio hilo, ndipo alipomueleza kuwa mfanyabiashara huyo kabla ya kuchukua maamuzi hayo, alimpigia kumuomba hela naye akamuomba amalizie vikao vya Bunge ndipo wazungumze vyema.

“Manjala aliniambia atakwenda kwenye vitalu vyake vya mbegu na alipokwenda huko aliporudi alipaki gari lake na kujipiga risasi,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom