Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 121
- 202
Askari namba H.4489 PC Kululetela wa kituo cha Polis Sirari Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya anadaiwa kushikiriwa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ng’ondi Marwa Masiaga (22) kutokana na kumfyatulia risasi kwa uzembe na kupekea majeraha yaliyopelekea kutokwa damu nyingi.
Taarifa ya Jeshi la Polisi kutoka Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya inaeleza kuwa Askari huyo kwa uzembe wake mwenyewe na bila uhalali wowote alimfyatulia risasi raia huyo asiyekuwa na hatia na kumjeruhi kwenye paja lake la mguu wa kulia.
Madhura huyo imeelezwa kuwa alikimbizwa katika hospitali ya Tarime ambapo alifariki Dunia wakati akipatiwa matibabu. Ambapo imeelezwa kuwa uchunguzi wa awali umebai kuwa alifariki kutokana na kutoka damu nyingi.
Kufuatia tukio hilo imeripotiwa kuwa askari huyo anashikiriwa na upelelezi wa tukio hilo unaendelea na kuwa utakamirishwa mapema, huku taarifa hiyo iliyotolewa Machi 31, 2023 inaeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ukisubiri uchunguzi wa kitabibu.
Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app