JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ametoa taarifa za tukio la Askari kujiua kwa kujipiga risasi kisa mgogoro wa mapenzi.
Amesema tukio la kujiua kwa kujipiga risasi kwa aliyekuwa Askari J.2596 Konstebo wa Polisi Samwel Feston Kaziyote [24] wa kituo kikuu cha Polisi Mbeya.
Ni kwamba, Oktoba 02, 2023 majira ya saa 2:15 usiku huko maeneo ya Mtaa wa Mzumbe Forest ya zamani, Jijini Mbeya Askari huyo alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake papo hapo.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la Benki na kisha kuondoka na silaha bunduki kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.