Askari ajitoa uhai kwa kuupoteza msafara wa Kikwete Tarime!!!

Nadhani waliomuweka mahabusu nao wana panick zao labda walitaka waonekane wanatenda kazi, nadhani adhabu yake ingekuwa kumsimamisha kazi kaw siku mbili tatu na kumrudisha chuo cha polisi japo kwa mwezi ili ajifunze. Nadhani baadhi ya haya matatizo yanasababishwa na kutokuwa na miongozi kabambe ya aina ya adhabu wanazoweza pewa watumishi baada ya makosa fulani fulani, hii ni kwa idara zoto za serikali si polis tu. Kama kuna miongozo yoyote basi ipitiwe tena ili mambo kama haya yasijirudie.
 
kuna habari kuwa huyu askar ameuwawa na askari mwenzake....baada ya kujibishana kwa mda mkuu wake akapata na hasira akaamua kumshooot....
 
Watanzania bwana ! Hivi tumelogwa ? Yaani tunaambiwa huyo binti kajipiga risasi akiwa mahabusu na sisi tunaamini hivyo. Yanikumbusha swali la Mwalimu Nyerere kwa mwandishi wa habari Nairobi Kenya - akitokea jamaa akadai mimi ndiye babaako, utaandika hivyo ? Jamani toka lini mahabusu akawa na silaha ? Tuwe na akili kidogo.
 
kama kweli huyo askari alikuwa mgeni kwenye kazi kwa nini alipewa kazi ya kujaribu kwenye msafara mkubwa kama huo, kwa nini ajifunzie kazi kwa mkuu wa nchi, hivi hakuna mtu alinayefanya risk assesment ya masafara mkubwa kama wa raisi, hivi hapo walipokata bogi ingekuwaje kama jamaa angevamiawa?

lakini la pili na la kusikisha ni jinsi ya kuhandle issue kama hizo, hapo muhusika mkuu anawekwa pembeni, kwa uhakika mkubwa huyo Dada alikuwa anaelekezwa au alikuwa anapewa maelekezo na mtu aliyekuwa well informed lakini hata kama alikosea kwa nini aproach ya vitisho ilitumika?
 
ukweli ni kwamba... kuna mtu anahusika na kifo cha huyu mdada... halafu mtu amejipiga risasi vipi? soma tena habari uone maajabu ya alivyojiua..
 
Polisi ajiua kwa kuupoteza msafara wa Rais Kikwete,AJIPIGA RISASI AKIWA RUMANDE Monday, 05 July 2010 07:47

Anthony Mayunga, Tarime
Mwananchi

SAA chache tu baada ya msafara wa Rais Jakaya Kikwete, kuingia katika Kanisa a Anglikana, ili kuhudhuria sherehe za kuwekwa wakfu Askofu, askari polisi wa kike WP Suzana, amejiua kwa kujipiga risasi baada ya kuwekwa mahabusu kwa kosa la kuupoteza njia, msafara wa Rais.

Habari zilisema tukio hilo lililogeuka kuwa gumzo katika mji huo, lilitokea saa 8 mchana wa jana, katika Kituo cha Polisi Tarime, muda mfupi baada ya askari huyo kuwekwa chini ya ulinzi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Dk Charles Samson, alikiri kuupokea mwili wa askari huyo na kwamba alijipiga risasi upande wa kushoto wa kifua.

Kwa mujibu wa Mganga huyo, risasi hiyo ilipenya na kutokea nyuma ya bega.

"Ni kweli amejiua kwa kujipiga risasi ambayo imetokea nyuma ya bega. Kwa ufupi ni kwamba eneo hilo ni sehemu ya moyo, nimemfanyia uchunguzi wa awali na
kuthibitisha kuwa amekufa,"alisema.

Alisema taarifa kuhusu tukio hilo alizipata akiwa katika msafara wa Rais na kwamba alipokwenda kumfanyia uchunguzi marehemu, alibaini kuwa alikata roho muda mfupi,baada ya kujipiga risasi.

"Kitaalam kilichosabaisha kifo ni risasi maana nimefanya uchunguzi na kubaini, nasubiri uchunguzi mkubwa tukiwa na polisi ili tuwakabidhi maiti kwa ajili ya hatua nyingine,"alisema kwa masikitiko.

"Sijui nini kimempelekea kujiua maana huo ni uamuzi mzito sana aliochukua," alisisitiza Mganga mkuu.

Kwa upande wake, mhudumu wa chumba cha maiti katika hospitali hiyo, Samweli Malindi, alisema marehemu alifikishwa katika katika chumba hicho kwa kutumia gari la polisi.

"Walisema amejiua kwa sababu ya kuongoza vibaya msafara wa Rais na kuwekwa mahabusu," alisema.

Chanzo kimoja cha uhakika kutoka ndani ya jeshi hilo, kililiambia
gazeti hili kuwa kiini cha askari huyo kujiua ni kuwekwa mahabusu huku akitishiwa kuchukuliwa hatua kali zaidi.

Chanzo hicho kilisema msafara wa Rais ulitakiwa kuingia kwa mkuu wa wilaya, kabla ya kwenda kanisani, lakini yeye aliruhusu magari kwenda moja kwa moja na gari la Rais likielekea kwa mkuu wa wilaya, jambo lililosababisha safara ukagawanyika na baadaye kulazimika kurudi.

"Kitendo hicho kiliwachukiza viongozi na kuamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa askari huyo. Wakati akiwa mapokezi ghafla alichukua bunduki aina ya SMG na kujimiminia risasi tatu na kukata roho papo hapo," kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilidai kuwa askari huyo ni miongoni mwa askari polisi waliotoka chuoni hivi karibuni na kwa hiyo si mzoefu.
Chanzo hicho kilisema katika hali ya kawaida viongozi walipaswa kumsaidia kwa kutumia lugha ambayo vinginevyo isingemfanya ajisikie vibaya na kuchukua uamuzi huo.
Baadhi ya wananchi wakizungumza na Mwananchi walisema hayo ni matatizo ya matumizi ya nguvu ndani ya jeshi.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Polisi ya Tarime/Rorya, Constantine Masawe,alisema alikuwa nje ya ofisi."Niko Dar es Salaam na wala sikuwa na taarifa, amejiua kwa nini, maana sijaambiwa,"alisema.

Rais Kikwete, alikuwa amekwenda Tarime kuhudhuria kuwekwa wakfu kwa Askofu Dk Mwita Akiri.
 
"Kitendo hicho kiliwachukiza viongozi na kuamuru kukamatwa na kuwekwa
mahabusu kwa askari huyo. Wakati akiwa mapokezi ghafla alichukua bunduki aina ya SMG na kujimiminia risasi tatu na kukata roho papo hapo,

really..!!

Alichukua SMG kutoka wapi na ya nani? kwa vile wanasema amajipiga moyoni (ikatolea mgongoni).. halafu ni "risasi tatu".. hivi urefu wa SMG ukoje na aliishika vipi kujipiga risasi tatu moyoni... maana ukiniuliza mimi risasi ya kwanza ilitosha kumuua na kuzuia kupiga risasi nyingine tatu unless baada ya kujipiga risasi ya kwanza alijikuta bado yuko hai, akajipiga ya pili, bado yuko hai na akajipiga ya tatu!
 
Kumbe wanaoongoza msafari ni askari. Basi kuna tatizo katika logistic za misafara ya wakuu wetu. Naamini haitakiwi kuwa hivyo Polisi akiongoza msafara vibaya haimanisi dereva na ma sweeper yafuate amri ya polisi. Au mimi ndo sielewi. Kwa nini wasiwaweke ndani madereva? Kwa nini wasimuweke ndani mkuu wa protocol wa hiyo ziara?

hii ni weakness tena kubwa imekuwa exposed. Aksari 1ja anaweza kuupoteza msafara. haaaahha
 
Nilifahamu tu kuwa huyu dada katolewa KAFARA. Kuna mtu kafanya uzembe na mzigo wamemuachia huyu dada wa watu. Kibinti hata uzoefu hakina, kiliachiwaje msafara wa Rais? Hivi hiki kikosi kinachomzunguka Rais kinafanya kazi kweli? Watu wakisema Rais anadanganywa, wengine mwasema si kweli.

Kitendo cha dada ambaye ni juzijuzi tu kaanza kazi na hana uzeofu wa kazi na nyie mnamleta eti aongoze msafara wa Rais, ni kichekesho. Sijui aliipata hiyo POST kwa kuvua chupi na sasa yamemtokea au ilikuwa bahati yake? Binti hakufahamu kuwa wamemuweka kama chambo na mambo yakienda vibaya kwa uzembe wao, basi yeye ndiye atabebeshwa mzigo.

Ingelikuwa nchi ya SHERIA, wengi wangelipoteza kazi ukianzia na Masha mwenyewe.

From: Polisi ajiua kwa kuupoteza msafara wa Rais Kikwete,AJIPIGA RISASI AKIWA RUMANDE

Sio kosa lako bro,huzijui kazi za POlice ndo maana unatoa maneno ya kashfa kwa marehemu.Lakini kuongoza msafara Sio POST na ni kazi ndogo tu,sababu ni kiasi cha kunyoosha mkono tu na Msafara mzima unafuata hiyo direction ulioionyesha,haihitaji experience,inaweza hata fanywa na askari aliye mafunzoni(acha aliyemaliza),kilichotokea hapa ni askari kunyoosha wrong direction,Na hakuna askari anayeonga ili akapitishe msafara SABABU HALIPWI KWA HILO,na pia hiyo ni kazi isiyo na rushwa.Kitu ambacho na hakika nacho ni kuwa walimpa wrong information(na askari wana tabia ya kurukana linapotokea tatizo).Na la SMG kaipata wapi hilo halisumbui akili,sababu askari wana tabia ya kuoneana huruma pale mmoja wao wa cheo sawa nae anapowekwa lock up,wale walio counter humpa favour ya kukaa pale kwenye benchi badala ya kukaa lock up na watuhumiwa wa kiraia,hapo ndipo alipoipata SMG.Kwa knowledge yangu kuhusu hiyo bunduki,si kwamba mtu anaweza kujiua tu kwa risasi nne bali hata ishirini.Sababu knob ya Rapid N Each,ukiweka Rapid na kupull Triger kwa nguvu zinatoka risasi nyingi kwa mfululizo,hilo si ajabu.Ofcoz inauma sana hao viongozi kushindwa kumchukulia binti mdogo kama huyo,mpaka kumfanya awe extremly desperated.Mungu awatie nguvu ndugu na wazazi wake
 
je technicalities za kumlaumu zipo?, mfano siku chache kabla ya ujio aliambiwa au kuipita njia hiyo ili awe na uelewa wa njia au walitumia tu uzoefu? au wanba mlaumu tu kwa sababu ni mtu wa chini?
 
Soma POST nzima. Nimeshamwambia mwenzio aache KURUKIA TGV kwa mbele.
Wewe kazi ya POLISI unaifahamu? Hebu soma juu ujumbe wa BAK uone pameandikwa wazi kabisa kuwa "Chanzo hicho kilidai kuwa askari huyo ni miongoni mwa askari polisi waliotoka chuoni hivi karibuni na kwa hiyo si mzoefu.
Chanzo hicho kilisema katika hali ya kawaida viongozi walipaswa kumsaidia kwa kutumia lugha ambayo vinginevyo isingemfanya ajisikie vibaya na kuchukua uamuzi huo."

Mie ni mpenzi sana wa kuangalia Investigation Discovery na tangu niwe naangalia hapo, sijawahi kuona mtu kajiuwa kwa kutumia bunduki na kujipiga risasi moyoni. Kama wewe ni POLISI, sawa tu mkuu ila usinitishe kwa hilo maana na mie nilipitia JKT na kuitumia hiyo bunduki na nilibahatika kwenda mbele hadi kutumia Light Machine gun (na yenyewe pia AK).
Kama ulishaishika hiyo silaha au bunduki yoyote (ukiacha bastola), utagundua kuwa siyo rahisi kabisa kuupindisha mkono na kujipiga moyoni. Milele njia rahisi kabisa kwa bunduki ni kuwa watu huwa wanaula mdomo wa bunduki na ........ na kwa bastola, huwa wanajipiga kichwani upande wa sikio maana ndiyo rahisi. Hii eti kajipiga na SMG, nendeni mkauze hukoo mbele ya safari.

Hivi kuongoza MSAFARA sidhani kama ni vile unafikiri wewe. Kama angelikuwa kasimama barabarani basi angelipoteza msafara mzima na si nusu ya msafara. Nilivyoelewa mie ni kuwa alikuwa ndani ya gari la mbele kama KIONGOZI wa msafara. Hii ikapelekea baadhi ya madereva wa mwanzo kama sikosei walienda sehemu tofauti na yeye akaja na Rais akaenda sehemu tofauti. Maelezo yako ya juu ya kudhani Suzzy alikuwa i Traffic Police hayana maana. Na kama ni kweli basi huyu marehemu alikuwa mgonjwa wa akili kwa kuruhusu baadhi ya magari yaende kanisani na mengine yaende kwa mkuu wa Mkoa.

All in all, huyu dada kwa msafara mzito namna hii, ilitakiwa wawekwe wazoefu. Kwa nini hawakuwekwa wazoefu na akawekwa huyu marehemu, mie nimeweka theory nyingi. Ila watu wanaona moja na kuanza kutukana. Watanzania kweli siku zote tunapenda kujipa maswali MEPESI.
Sawa mkuu, kama nimewaudhi na maswali yangu MABAYA, mnisamehe. Kuleni maisha na maswali mepesi.

We ni muongo,unaongea vitu ambavyo havipo,MIMI SIO POLICE,kiprotocal msafara wa rais hauongozwi hivyo,mbele kunakuwa na rider(mwenye pikipiki),anafuatiwa na gari ya RTO(Regional Traffic Officer),then zinafuata escort mbili au tatu za usalama,pia na gari ya RPC(akiwa mkoani),gari ya rais inakuwa na pamoja na gari ya rearguard ya fieldforce.niambie huyo WP atakaa kwenye gari ipi hapo kuuongoza huo msafara.Huyo WP alikuwa chini kwenye point,kutokana na direction yake rider alikosea na kuna gari zilimfuata,inawezekana kabisa kuna watu walijua msafara unatakiwa uende wapi,ndo maana ukatokea huo mchanganyiko.Na kuhusu SMG inawezekana umezisahau(kama kweli ulipita hiyo JKT yako),Kuna SMG(tena nyingi),zina vitako vya chuma vya kukunja,ukiikunja inakuwa fupi kama uzi gun,na inawezekana kabisa kujielekezea na kujipiga na police wetu wanazo hizo nyingi kuliko za vitako virefu.Kuhusu hiyo LMG yako hainihusu,hatupo kushindana nani katumia bunduki ipi na ipi.
 
Kwenye nyekundu hapo: Unajuaje kama hiyo SMG ilikunjwa au ni ile yenye kitako kifupi?? Inaonekana unafanya vitu under assumption zaidi. Sina nia ya kukupinga ila ingependeza kama kungekua na ukweli kuhusu SMG iliyotumika. Ni kweli ilikunjwa? Una uhakika? Uliiona au uliambiwa? Please thibitisha mkuu otherwise unaongea bila facts hapa. Ikiwezekana tungepata hata picha ya hiyo SMG iliyotumika kwenye tukio ili tujiridhishe na maneno yako.
 
Hivi huyu askari alipata wapi silaha akiwa kituoni? Siamini kuwa askari trafiki (tena mwananchi imesema ndiyo katoka mafunzoni) anayeongoza magari ya msafara wa mkuu wa nchi angekuwa na silaha kiholela (Kumbukeni Rais Anwar Sadat alivyouawa kwenye gwaride na skari aliyepenyeza risasi kwenye bunduki ya paredi). Hapa ni lazima kuna security breach kwa hali ya juu. Hapa inaelekea kuna siri nzito - maybe an interogation gone extremely bad, au akatishia kutoa siri ya kuupoteza msafara wenyewe ..... Jeshi la polisi limezoea kuua raia na inanitia mashaka kuwa huenda sasa sasa wameanza kujiua wenyewe, au kuna uzembe wa hali ya juu!!! ......... . Hii inaanza kutia wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa mkuu wetu wa nchi, hebu fikiria:

1) Gari la msafara kuzimika/kukataa kungia gia na kulazimu kuingia kwenye gari nyingine
2) gari aliyohamishiwa kuchomoka tairi baada ya muda mfupi
3) Ikulu kusema hayo ni mabo ya kawaida tu
4) Gari ya msafara kuwekwa mafuta yaliyochakachuliwa
5) Ikulu: Aaah! Mbona ni kawaida tu!
6) Msafara wa raisi kupotea njia
7) Askari alieupoteza kufariki kituoni akiwa mahabusu chini ya ulinzi wa polisi

The bottom line ....................conspirancy theory?

Bila kusahau msafara kupigwa mawe huko Mbeya!!!

Where is the presidential security detail?
 
Kwenye nyekundu hapo: Unajuaje kama hiyo SMG ilikunjwa au ni ile yenye kitako kifupi?? Inaonekana unafanya vitu under assumption zaidi. Sina nia ya kukupinga ila ingependeza kama kungekua na ukweli kuhusu SMG iliyotumika. Ni kweli ilikunjwa? Una uhakika? Uliiona au uliambiwa? Please thibitisha mkuu otherwise unaongea bila facts hapa. Ikiwezekana tungepata hata picha ya hiyo SMG iliyotumika kwenye tukio ili tujiridhishe na maneno yako.

Je hao askari ambao walikuwa wanamhoji walikuwa wapi hadi akajipiga risasi nne? Hapa ni lazima kuna jambo
 
Kwenye nyekundu hapo: Unajuaje kama hiyo SMG ilikunjwa au ni ile yenye kitako kifupi?? Inaonekana unafanya vitu under assumption zaidi. Sina nia ya kukupinga ila ingependeza kama kungekua na ukweli kuhusu SMG iliyotumika. Ni kweli ilikunjwa? Una uhakika? Uliiona au uliambiwa? Please thibitisha mkuu otherwise unaongea bila facts hapa. Ikiwezekana tungepata hata picha ya hiyo SMG iliyotumika kwenye tukio ili tujiridhishe na maneno yako.
You have a point,nilikuwa nazungumzia uwezekano wa mtu kujiua kwa SMG,maana kuna watu wamekataa kuwa haiwezekani mtu kujigeuzia hiyo bunduki.Dhidi ya hapo,mimi sikuwepo eneo la tukio na wala sijui aina ya bunduki iliyotumika,sawsawa na hao wanaosema inawezekana kuna mtu kamuua huyo dada.nadhani umenielewa
 
if u shoot urself in the chest then u have to use a handgun in which case u cant be standing up or conscious long enough to shoot urself 4 times. Labda usalama wazushi wale feki wamemuua maskini. U cant shoot urself in the chest 4 times... especially not when you are in remand, huna ata kamba za viatu, bunduki na risasi zinatoka wapi?
 
Back
Top Bottom