Tarime: Askari Polisi ashikiliwa akidaiwa kumuua dereva bodaboda kwa risasi, RPC asema Askari anastahili kuwajibika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Jeshi la Polisi linamshikilia askari wake mwenye utambulisho wa H 4489 PC Kululetela, kutokana na kosa la kumfyatulia risasi iliyomjeruhi hadi kumsababishia mauti mwendesha bodaboda, Ng'ondi Marwa (22), mkazi wa mjini Tarime.

Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Polisi Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarakikya amesema kuwa askari huyo kutoka Kituo cha Polisi Sirari anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Tarime na kwamba upelelezi wa kesi yake utakamilika mapema kwa hatua zaidi za kisheria.

Kwa mujibu wa RPC Sarakikya, Marwa amepigwa risasi kwenye paja la kulia akiwa katika kitongoji cha Nyansisine kijijini Kubiterere, Ijumaa Machi 31, 2023 saa mbili asubuhi.

Ameongeza kuwa kijana huyo amefariki Dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime na kwamba mwili wake umehifadhiwa hospitalini hapo kusubiri uchunguzi zaidi na taratibu za mazishi.

photo_2023-04-01_08-22-25.jpg
 
Jeshi la Polisi linamshikilia askari wake mwenye utambulisho wa H 4489 PC Kululetela, kutokana na kosa la kumfyatulia risasi iliyomjeruhi hadi kumsababishia mauti mwendesha bodaboda, Ng'ondi Marwa (22), mkazi wa mjini Tarime.

Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Polisi Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarakikya amewambia waandishi wa habari ofisini kuwa askari huyo kutoka Kituo cha Polisi Sirari anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Tarime na kwamba upelelezi wa kesi yake utakamilika mapema kwa hatua zaidi za kisheria.

Kwa mujibu wa RPC Sarakikya, Marwa amepigwa risasi kwenye paja la kulia akiwa katika kitongoji cha Nyansisine kijijini Kubiterere, Ijumaa Machi 31, 2023 saa mbili asubuhi.

Ameongeza kuwa kijana huyo amefariki Dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime na kwamba mwili wake umehifadhiwa hospitalini hapo kusubiri uchunguzi zaidi na taratibu za mazishi.

Tarime kama Tarime
 
Kule mkoa wa geita, nyumbani kwa shujaa wa afrika magufuli. Bodaboda alipouawa na polisi walitoa kichapo kwa asikali na kisha kukitia moto kituo cha polisi.

Toka waitara amwage choz., wakurya siwaamini tena dhidi ya ukakamavu wenu.
 
Back
Top Bottom