masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
Comrade Kinana ndio kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu kabisa katika ungozi wa CCM kujionea kero za barabara iliyosuswa na Awamu kadhaa( kuanzia alipochaguliwa Waziri wa Ujenzi-Magufuli, Awamu ya Mkapa) katika ujenzi wa barabara nchini.
Hapa mtandaoni tumelalamika sana , bila mafanikio, ubovu na ufinyu wa barabara hii kuu iendayao Malawi, Zambia na Congo.
Kutokana na tatizo hili, hasa pale Tunduma, malori yana paki lane moja.
Lane ya pili iliyobaki ndio yanapishana magari yote, na lane hiyo haizidi mita tatu na nusu!
(picha inajieleza)
Ni kero...... kero...... kero!!
Comrade Kinana kajionea pale Tunduma, Songwe, foleni ya malori yenye shehena ambayo wakati mwingine inaenda hadi kilometa 15 hadi 20 kurudi nyuma.
Awamu ya hasa mwendazake , iliisusa kabisa mikoa hii ya Nyanda za Juu Kusini kwa hii barabara ya Dar es salaam mpaka Songwe.
Funga kazi ni ubovu wa barabara kuanzia Igawa nadi Songwe.
Barabarahii finyu yenye mashimo na viraka lukuki, inapita katikati ya Jiji la Mbeya na kusababaisha kero na ajali zisizo na kifani.
Tnamshukuru sana Comrade Kinana kwa kuikumbusha Serikali wajibu wake uliotekelezwa kwa mikoa hii ya Nyanda za Juu kusini.