Trilioni 1.33 kutumikakwa kwenye ujenzi wa barabara ya lami, njia nne yenye urefu wa kilomita 218 kutoka Igawa Mkoani Mbeya hadi Tunduma Mkoani Songwe

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Serikali imepanga kutumia zaidi ya shilingi trilioni 1.33 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami, njia nne yenye urefu wa kilomita 218 kutoka Igawa Mkoani Mbeya hadi Tunduma Mkoani Songwe lengo ni kupunguza msongamano wa magari katika barabara hiyo ambayo ni namba moja kwa kusafirisha mizigo mingi hapa Nchini.

Mradi huo utahusisha pia ujenzi wa barabara ya mchepuo kutoka Inyala - Uyole hadi Songwe wenye urefu wa kilomita 48 ambayo itapita nje ya Jiji la Mbeya.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mha. Godfrey Kasekenya ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Novemba 2023 alipopewa nafasi ya kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Ruanda Wilayani Mbozi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye katika ziara yake Mkoani Songwe leo alitembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya lami kutoka Ruanda - Nyimbili - Hasamba - Izyila - Itumba km 79.67 na Mahenje- Hasamba - Vwawa km 31.8; Sehemu ya kwanza Ruanda - Idiwili km 21, kipande cha kwanza km 1.2 na muendelezo km 21.1.

Amesema asilimia 70 ya mizigo inayopita na kutoka katika Bandari ya Dar- es Salam kwenda na Nchi za SADC inapita katika barabara hiyo “hapa Ruanda kumefanyiwa usanifu kutakuwa na keep-left kikubwa sana, kwa ajili ya kuunga barabara hii ambayo tunaitanua kwa kuwa ni kero kwa sababu magari ni mengi, Songwe ndio langu kuu la Nchi za SADC kwani ukitaka kwenda Nchi Jirani za Congo, Zambia, Malawi, Zimbabwe lazima upite Songwe’’.

Amesema tayari Serikali imeshatangaza tenda kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo ambao ni moja wapo ya ile miradi yenye jumla ya kilomita 2,035 ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaitekeleza Nchi nzima kwa mpigo kwa kutumia utaratibu wa EPC + F na kwamba hizo 218 kwenye ujenzi zitagawanywa mara nne kila kipande kitakuwa na Mkandarasi wake ili kuharakisha utekelezaji wa mradi.

Akizungumzia mradi uliokaguliwa na Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mha. Kasekenya amesema una upekee wake Tanzania nzima kwani kwenye utekelezaji wake pamoja na kwamba Mkandarasi ameanza kujenga kilomita 2, Mhe. Rais Dkt. Samia ametoa maelekezo kwamba katika kilomita 21 za kwanza zigawanywe katika vipande vinne kwa maana ya kila mmoja kilomita 5 kisha wapewe kazi ya Ujenzi Wakandarasi Wanawake ikiwa ni kuwawezesha, kuwainua na kuwajengea.
 
Sijafika Mbeya siku nying.

Huo ujenzi kuanzia Igawa umeanza? Maana tangu mwaka unasikika Tu.
 
Hizo habari kila mwaka tunazisikia,hizi ni porojo za kisiasa,waache siasa waanze kazi tuwaamini.
 
Back
Top Bottom