Mhandisi Bishanga: Barabara ya TANZAM inayojengwa kwa njia nne kutoka Igawa (Mbeya) hadi Tunduma (Songwe) km. 218, inagharimu trilioni 1.33

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Serikali ya awamu ya sita imeendelea kufungua Nchi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo Mkoani Songwe ikiwemo ujenzi wa barabara ya kimkakati ya TANZAM inayojengwa kwa njia nne kutoka Igawa (Mbeya) hadi Tunduma (Songwe) yenye urefu wa km. 218 kwa gharama ya shilingi trilioni 1.33

Pia Kuna ujenzi wa barabara ya lami kutoka Tunduma kuelekea Mkoani Katavi, kwenda Kigoma hadi Manyovu kuelekea Nchi Jirani ya Burundi, barabara hizo ni muhimu kwa sababu zina magari mengi, zinakuza uchumi wa Mkoa na kuongeza pato la Taifa, na ni lango kuu la Nchi za SADC kwani jumla ya asilimia 75 ya mizigo ambayo inatoka katika Bandari zetu za Dar- es Salaam na Tanga inapita katika mpaka wa Tunduma.

Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga ameeleza hayo tarehe 24 Novemba 2023, alipohojiwa na Waandishi wa Habari muda mfupi kabla ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutembelea na kukagua ujenzi barabara ya lami kutoka Ruanda - Nyimbili - Hasamba - Izyila - Itumba km 79.67 na Mahenje- Hasamba - Vwawa km 31.8; Sehemu ya kwanza Ruanda - Idiwili Kilomita 21, kipande cha kwanza km 1.2.

Barabara nyingine ni kutoka Mpemba kwenda Isongole mpakani mwa Malawi ambayo tayari imeshakamilika kwa km 50; barabara ya Iyula kwenda Ileje ambayo itapunguza umbali wa safari kwa km 25 alafu ina muunganiko kwenda Malawi na Zambia, barabara ya Mlowo kwenda Kamsamba inaunganisha Mkoa wa Songwe na Rukwa ina jumla ya km 130 mwaka huu imepangwa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa zaidi ya km 50 na mchepuo wake kutoka Utambalila kwenda Chitete Makao Makuu ya Wilaya ya Momba kuna mpango wa kujengwa lami tayari tumeweka lami kwenye maeneo ya Ofisi za majengo ya Serikali.

Ameongeza kuwa kwa ujumla hali ya Barabara Mkoa wa Songwe ni nzuri zote zinapitika bila shida katika majimbo yote na kwamba katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suhulu Hassan imeelekeza jumla ya Shilingi bilioni 9 katika Mkoa wa huo kwa ajili ya matengenezo na shilingi bilioni 2.6 kwa upande wa Maendeleo.
 
Back
Top Bottom