Aaaah. Mambo gani tena haya Arteta na Arsenal? Nimelala vizuri nikijua nitaamka na kujikuta nimeketi zangu fresh kileleni nikiwachora kina Livakuku.
Yaani tumeshindwaje kuwapiga hawa hammers? Sitaki hata kujua. Kwa ujinga huu mimi naona tuachane na kutafuta ubingwa, tuwape Livakuku baraka zetu waupambanie wao. Tutumie muda huu kuboresha kikosi, haswa upande wa ushambuliaji. Halafu tufanye moja kati ya haya mawili:
1. Fukuzia mbali kabisa Arteta.
2. Baki na Arteta lakini yeye na timu nzima waanze sessions na wanasaikolojia washughulikie hiyo block inayowafanya washindwe kutimiza vitu simple tu kama kushinda mechi za lazima kabisa, tena dhidi ya wapinzani dhaifu kuliko Arsenal.