Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hadi dakika hii siamini tumefungwa fungwa vipi, kuubonda kote kule!

Ila Nina uhakika ata tukirudiana nao kesho kutwa jmoss labda tujitahidi tusiruhusu goal
Ila kuwatia goal, naona haiwezekani kabisa

Kuna Muda timu nzima ya westham ilikua ndani ya box lao, odegard mtafuta mashimo Jana alikua hajui afanye Nini Sasa
 
LEICESTER wanachukua Ubingwa walijikuta Nafasi ambayo hawakuitegemea, Ukiangalia Mzunguko wa Pili ilikuwa ni suala la Mwalimu zaidi. ARTETA Mwalimu mzuri lakini bado ni Mwanafunzi aliye kazini, Hawezi jua Kupambana na Pressure kwake Binafsi na kwa Wachezaji wake. {Na ana "EGO" kuamini anajua kumbe bado sana}

Game Nyingi kwa sasa Timu zikicheza na Arsenal zimeamua kuiheshimu na zinawadhuru sana kupitia Utumiaji nafasi, Jana unamaliza na Nafasi za Wazi zaidi ya 5 bila Goli halafu unawaza Ubingwa! Haaland ama Salah washatoka hiyo hatua, Ukitaka Ubingwa nenda nao Jino kwa Jino, Kuwa na ST/CF uhakika ambao kuwapata January ni Bahati nasibu. KDB akirudi kwa CITY ni kama Sajili Mpya.

ARSENAL imekuwa inafungwa aina ya Magoli yanafanana sana karibuni, Imekuwa kama Mbinu ya walimu wa Timu nyingine. Mnafungwa sana Mipira ya Kutenga, Kona, Faulo, kitu ambacho Mlikuwa hamna kabisa msimu ulopita!
Arteta ana ego,, au wewe ndiio una ego juu ya Arsenal na Arteta,!?

Mbona mnajitungia vitu from no where,!?
 
Nyie Aseno ni zaidi ya mbwa. Mnacheza na kibonde afu mnanichania mkeka? Hamtakuja kushinda kombe lolote lile la maana; nawalaani. Mtaishia tu kushinda makombe ya Emirates cup wapuuzi nyie!
Eet laana ,,,wewe nani uipe timu yetu Laana,

Tuliko toka na tunako kwenda ni bora zaidi.. kinacho wa uma na mnaumia nijinsi tuna oneshe mwanga wa kuja kuchukua vyote..
 
Mhuni hamis77 kajifukia baada ya timu kupoteana ili aje ajibu hoja za watu humu. Najua atakuja na turufu moja ya kujilinda kwamba King Kai ndio sababu ya wao kushindwa kuchukua alama 3 maana kwa uwepo wake mngecheza aerial balls nyingi,angefanya pressing na kusaidia overloading maeneo ya pembeni na kufanya movements kudanyanya difendaz wa Hammers watoke katikati.

Mwisho mzuri katika football kwa fan yeyote yule ni matokeo mazuri na wala sio possession kubwa au kupiga chenga nyingi pamoja na takwimu uchwara za touches in opponents box,ni vitu jamaa anatumia sana kuwajaza wanae humu ndani.
 
What a christmas present from The Hammers to all football fans around the world!
 
Binafsi sina tatizo na hao mashabiki wa timu zingine wanaoleta karaha humu ndani maana ni haki yao kama ambavyo tunapeleka karaha kwenye majukwaa yao.

Shida yangu ni hao wanaosema ni mashabiki wa Arsenal alafu wanasema haiwezi kuchukua ubingwa bila kutoa sababu za kimpira zaidi utasikia mara Arteta hana uzoefu, mara hatuna wachezaji wa kushindania ubingwa au mara tumu ina wachezaji wawili tu waliokamilika. Yaan ni watu wanaongea ovyo ovyo tu kama walevi. Tulitarajia timu ikifungwa au ikishinda basi tuje na maoni na mitazamo ya kimpira kwamba timu yetu imefungwa kwasababu kadha wa kadha au tumeshinda lkn bado tunatakiwa kurekebisha 1,2

Kwa wale ambao mnaisifia Liverpool nawakumbusha nyuma kidogo, baada ya Liverpool kucheza final ya UCL 2006/2007 timu ilianza kupoteana kidogo kidogo mpaka kufikia kushindwa kufuzu kucheza UCL 2010/2011 na imemchukua liver misimu mitano kurudi UCL.

Liver ilianza kurudi kwenye form chini ya kocha Roggers mpaka alipokuja kuichukua krop 2016/2017 ikiwa tayari imeanza kuwaka lkn bado ilimchukua Krop zaidi ya misimu 4 kuchukua Epl. Cha ajabu ni kwamba Arteta kaichukua Arsenal ikiwa hoi taabani lkn katumia misimu miwili tu kuirudisha timu kwenye form na sasa ni msimu wa pili tangu timu ikae vizuri na kuanza kushindania makombe lkn bado kuna mtu anakwambia hatuna timu ya ushindani wakati mpaka sasa ipo nafasi ya pili kwa point 2 nyuma ya anaeongoza ligi.

Kuna wengine wanakuja na hoja ya kocha kukosa uzoefu, sawa ila tujiulize ili upate uzoefu inatakiwa ufanye nini? Je ni lazima kuwa na uzoefu ndo ufanye vizuri? Unai ni kocha mzoefu, je alifanya vizuri?. Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka wakati Pep anaochukua Barca kutoka Rigkard je alikuwa na uzoefu?? Zidane je???.

Nadhani wana-Arsenal tusijadili kama kwa kukandia kama ambavyo tunawakandia watani zetu wa timu zingine hilo tuwaachie wao kama tunavyowakandia kwenye majukwaa yao
Unajua mpira kaka, Kuna kima umu hazijui bolu Kama Lina matokeo matatu..

Sisi tunajua team yetu ime struggle for how long, na ndio Kwanzaa msimu wa pili arsenal imeludi kweny reli.
 
ya Saliba kuanza kupewa nafasi ya kucheza ulikuwa umewahi kuona kuwa ni complete player? Rice kabla ya kuja Arsenal kwa misimu kadhaa uliwahi kuona kuwa ni complete player? Unaweza kututhibishia??? Au ndo porojo za kuangalia mpira 1990. Huwezi kuwa serious wewe
Wewe Hamis a.k.a AaronArsenal naona umefufua id yako ya zamani baada ya kudhalilika na utoto unaoujaza hapa jukwaani.

Mchezaji akicheza mechi 3 tu unajua kabisa huyu anajua na amekamilika au la. Sasa akina GJ, ode na zin kila siku wanarukaruka tu.
 
Mkuu ni wewe kweli au kuna mtu anachezea simu yako?
Yuko wapi hamis77 Castr na HENRY14
Mkuu computerarsenal ni mtu ambae amenyooka ndio maana hata mashabiki wenzake wa Arsenyo hua wanamuona kama msaliti.
Huyu jamaa sio wale bendera hufata upepo kila anachosema Masingeli na chawa wake basi na wao lazima wasapoti, computerarsenal timu ikifanya vizuri lazima asifie na ikizingua atakosoa, huyu jamaa ni mtu huru ambae hakubali akili yake kushikiliwa na watu ambao humu wanajiona wao ndio wana hati miliki ya timu.
 
Eet laana ,,,wewe nani uipe timu yetu Laana,

Tuliko toka na tunako kwenda ni bora zaidi.. kinacho wa uma na mnaumia nijinsi tuna oneshe mwanga wa kuja kuchukua vyote..
Huo "mwanga" umeuonyesha tangu lini? Utaishia hivyo hivyo na tamaa zako za fisi ukidhani mkono utadindoka ule hadi njaa za makombe zitakuua
 
Binafsi sina tatizo na hao mashabiki wa timu zingine wanaoleta karaha humu ndani maana ni haki yao kama ambavyo tunapeleka karaha kwenye majukwaa yao.

Shida yangu ni hao wanaosema ni mashabiki wa Arsenal alafu wanasema haiwezi kuchukua ubingwa bila kutoa sababu za kimpira zaidi utasikia mara Arteta hana uzoefu, mara hatuna wachezaji wa kushindania ubingwa au mara tumu ina wachezaji wawili tu waliokamilika. Yaan ni watu wanaongea ovyo ovyo tu kama walevi. Tulitarajia timu ikifungwa au ikishinda basi tuje na maoni na mitazamo ya kimpira kwamba timu yetu imefungwa kwasababu kadha wa kadha au tumeshinda lkn bado tunatakiwa kurekebisha 1,2

Kwa wale ambao mnaisifia Liverpool nawakumbusha nyuma kidogo, baada ya Liverpool kucheza final ya UCL 2006/2007 timu ilianza kupoteana kidogo kidogo mpaka kufikia kushindwa kufuzu kucheza UCL 2010/2011 na imemchukua liver misimu mitano kurudi UCL.

Liver ilianza kurudi kwenye form chini ya kocha Roggers mpaka alipokuja kuichukua krop 2016/2017 ikiwa tayari imeanza kuwaka lkn bado ilimchukua Krop zaidi ya misimu 4 kuchukua Epl. Cha ajabu ni kwamba Arteta kaichukua Arsenal ikiwa hoi taabani lkn katumia misimu miwili tu kuirudisha timu kwenye form na sasa ni msimu wa pili tangu timu ikae vizuri na kuanza kushindania makombe lkn bado kuna mtu anakwambia hatuna timu ya ushindani wakati mpaka sasa ipo nafasi ya pili kwa point 2 nyuma ya anaeongoza ligi.

Kuna wengine wanakuja na hoja ya kocha kukosa uzoefu, sawa ila tujiulize ili upate uzoefu inatakiwa ufanye nini? Je ni lazima kuwa na uzoefu ndo ufanye vizuri? Unai ni kocha mzoefu, je alifanya vizuri?. Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka wakati Pep anaochukua Barca kutoka Rigkard je alikuwa na uzoefu?? Zidane je???.

Nadhani wana-Arsenal tusijadili kama kwa kukandia kama ambavyo tunawakandia watani zetu wa timu zingine hilo tuwaachie wao kama tunavyowakandia kwenye majukwaa yao
Kwa nafasi aliyokaa Arteta last season katika 1st position for 284 days na Trophy hakubeba ingekuwa Klopp au Guardiola kombe angebeba na season hii ni yale yale kama ya last season position ambayo anatakiwa kukaa akishinda anaikosa so nothing new kwa Arsenal ya sasa tupo na tutakumbushana kocha una miaka 5 still unajenga timu ambayo ikitaka position nzuri unakosa ni mazoea na tushazoea

Kuna sentence unasema tujadili nini kirekebishike kwani kilichotokea jana na last season refer 10 games za mwisho utofauti wake ni nini sasa?
 
Mkuu computerarsenal ni mtu ambae amenyooka ndio maana hata mashabiki wenzake wa Arsenyo hua wanamuona kama msaliti.
Huyu jamaa sio wale bendera hufata upepo kila anachosema Masingeli na chawa wake basi na wao lazima wasapoti, computerarsenal timu ikifanya vizuri lazima asifie na ikizingua atakosoa, huyu jamaa ni mtu huru ambae hakubali akili yake kushikiliwa na watu ambao humu wanajiona wao ndio wana hati miliki ya timu.
🫡🫡🫡🫡
 
Ukweli Mchungu ni kwamba ARSENAL ni timu Nzuri lakini sio TISHIO Kariba ya INVINCIBLES sababu ya CHARACTERS zilokuwa Leo Hii, Arsenal CPT ni ODE, ila tizama INVINCIBLES Timu yote walikuwa na Uwezo wa Kuwa Manahodha. Nadiriki kusema Players Wanaweza Ingia ARSENAL ya INVINCIBLES wanaweza wasizidi 3 {Kwangu ni RICE, SALIBA Mwingine Mmoja atakuwa SUB}.
Kuna Baadhi humu wanajua Mpira haswa hadi unajiuliza Inakuwaje mtu kama huyu naye anaingizwa kwenye falsafa za KINAZI kama za SIMBA na YANGA kwamba ni mazuri yetu tu!!
TUPENDE MPIRA TUSIPENDE TIMU.

Arteta ana ego,, au wewe ndiio una ego juu ya Arsenal na Arteta,!?

Mbona mnajitungia vitu from no where,!?
HILI Ndo Tatizo kubwa Mpo nalo Mashabiki wengi wa ARSENAL humu ndani, Mtu akitoa hoja Hamji na Hoja kwa sababu amesema ambacho hamjapenda ila zinakuwa Porojo na Kejeli. Kuna hatua inafikaga Mnatoa Mpaka MATUSI!

Chatta g DEL BOSQUE, LUIS ARAGONES, hawa ilikuwa kizazi cha mwisho wa walimu wa Kispain wenye Umri ulosogea, BENITEZ alifanya Mapinduzi wakaanza aminiana na Umri mdogo, tizama PEP Mpaka leo jamaa ni Mbaguzi haswa, ENRIQUE anaamini ni Bora haswa, Xavi karibuni tu hapa alitaka aminisha Dunia kwamba kina GAVI na PEDRI ni zaidi ya Frenkie De Jong. Ni mengi juu yao wao watizame wanaamini Mpira upo kwao!

ARTETA ni kiburi, Huwezi amini aina ya Mchezaji kama Nketiah na Nielsen kama Plan B na wakati huo unataka Shindana, Kuna namna amemwacha Balogun kirahisi sana lakini angeweza wapa Mengi tofauti na Nketiah.

Kundi kubwa hapa halisemi Mna timu Mbovu, ila wanaamini bado ina mapungufu kadhaa kuwa Tishio na kuna wachezaji wengi wa kawaida ambao hao mnashindania nao Ubingwa wanaeza wasiingie kwenye Kikosi chao bora cha kwanza. Ila wewe na wengine wa aina yako huwa hamtaki amini kuhusu Hilo, na anayetoa Maoni ya aina Hiyo mnamwita Mamluki ama na Chuki!
 
🫡🫡🫡🫡
Mkuu wewe ni mtu huru, hua tunafurahia comments zako pale unapo pongeza timu inapofanya vizuri, tunakuunga mkono pale unapotoa ushauri kuhusu maboresho yanayohitajika kwenye timu, na pia tunasimama na wewe pale unapoamua kukosoa kwenye yale makosa yote yanayoonekana iwe ni kocha, wachezaji au management.
Hiki unachokifanya ndio maana halisi ya uhuru wa maoni, humu kuna watu wanataka mashabiki wote wawe kama maroboti (mtazamo mmoja) kitu ambacho hakiwezekani.
 
Wewe Hamis a.k.a AaronArsenal naona umefufua id yako ya zamani baada ya kudhalilika na utoto unaoujaza hapa jukwaani.

Mchezaji akicheza mechi 3 tu unajua kabisa huyu anajua na amekamilika au la. Sasa akina GJ, ode na zin kila siku wanarukaruka tu.
Unaona sasa ulivyomkalili Hamis, kwani una ugonvi nae!!?? Kuhusu Id hii kuwa ni ya Hamis hilo nakupuuza kwa kuwa halina maana. Kwahiyo kwa hoja yako ni kwamba ukimtizama mchezaji kwa mechi 3 tu tayari unajua huyu ni complete au sio complete. Je unaweza ukatusaidia vigezo vigezo vya kimpira unavyotumia kwa hizo mechi 3 kuthibitisha?
 
Back
Top Bottom