Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Imeisoma, na wewe soma ya kwangu
Nishaisoma. Au niwe clear. Hicho kipande cha Arteta kilishatembea sana insta nilikiona kabla ya leo.

Website iliyokupa hiyo taarifa ndiyo website ambayo imesema Kroenke hajawahi kuspend pesa kwa ajili ya Arsenal.

Na ni webiste hiyo hiyo inasema Kroenke mmiliki wa Rams anaspend 1 Billion Us dollars a year kwa ajili ya Rams.

Basi tuchukulie katoa hiyo 45 Million kwa ajili ya Partey kama unavyolazimisha iwe, ameimiliki timu kwa muda gani? Unahisi yeye kuspend 45M ni sahihi huku kwenye timu nyingine anatumia Billions?

Kwa unavyofikiria kama anaweza tu kutoa pesa mfukoni na kuwapa menejiment wanunue mchezaji unadhani FFP itakua inaangalia tu hilo tukio?

Unafikiri ni kwanini kampuni yake imeingia ubia ili itoe pesa ya usajili na hatoi tena mfukoni kama wewe unavyoamini? Unajua kama hiyo kampuni ina mwezi tu tangu iingie ubia na Arsenal?
 
Sijawahi kukimbia uzi mzee, ni majukumu ya kikazi tu sometime unakuwa ktk mazingira ambayo so rafiki na social networks ..

All in all

Everton 1 Cheltako O

Tuishi humo Kwanza,
Hzo nyingine zote kelele
Tuishi humu Arse8 0-1 Burnley mfungaji ni Aubameyang
 
Mourinho aliwarushia kijembe Arsenal (na timu zingine) walipomwacha Ancelotti na kumchukua Arteta. Alisema siku hizi timu zinataka kusajili kocha "mpya kabisa" ambaye kwenye rekodi yake ana zero defeats. Kwamba ukiangalia Ancelotti tayari kafungwa mechi mia ngapi huko unamwona garassa tu. Ila Arteta ni sawa na gari jipya zero kms run!

Arsenal na United zilichemka kwa hawa makocha amateaurs.
 
Maforward ndiyo walinzi namba mbili wa set pieces, baada ya CBs.
 
Aisee hizi timu mbili mashabiki wengi hawajui kuwa matatizo ya msingi yanaanza kwa wamiliki. Mimi pia huwa naona namna gani Mashabiki wa United hawajui tatizo lao la msingi lilivyo kwenye umiliki. Nimegundua kuwa ni ngumu sana kuelewesha mashabiki walio wengi kuhusu hilo. Acha tu ziendelee hashtags. Sasa ni #ArtetaOut.
 
Miezi kadhaa nyuma zilikuja tetesi kwamba Arsenal inamfuatilia Dominick, jana zinakuja taarifa kwamba Arsenal haikupeleka hata ofa na Dominick anajiunga na Leipzig.

Kama vile hakuna mpango wa kurecover.

Arteta na Luiz haziivi. Inadaiwa Luiz anavujisha taarifa za klabu na Arteta amewaambia wachezaji yeyote ambaye amevujisha taarifa atapotea.

Wachezaji baadhi walikasirika na jinsi Arteta alivyoiongelea kadi nyekundu ya Pepe. Bado sijamsikia akiiongelea kadi ya Xhaka ila naamini itakua ni yaleyale.

Gabriel kasema msinune. Mnahitajika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…