Angalia Wananchi Wanamlazimisha Rais Wao Asimame

Angalia Wananchi Wanamlazimisha Rais Wao Asimame

Mkuu suala sio kasi ya msafara, kasi inaweza kuwa ni ndogo lakini ule utashi wa mwananchi kuingia barabarani ukawa haupo.

Ukiitazama hiyo clip utaona hao watu wanavyoanza kujiandaa kupungia mikono ili gari isimame tangu wakati gari ya kwanza kabisa inakatiza mbele ya macho yao.

Hao watu wanaangalia taarifa za habari za TBC, ITV na nyingine, wanaona utashi wa rais jinsi ulivyo katika kutatua shida zao. Wanasikia yale maneno kwamba maendeleo ya kweli hayana chama, na mwisho wanaamua kuingilia msafara japo wapewe neno la faraja.

Phillipo sina wasiwasi na uwezo wako katika kutetea unachoamini. Je ww, rais pamoja na wananchi mnaamini matatizo yanatatuliwa kwa kusimamisha msafara wa rais? Iwapo rais hatokaa apite kwenye eneo ulipo tatizo lako halitokaa litatuliwe? Sasa kama ni hivyo kwa nini rais asipite nchi nzima mtaa kwa mtaa na kijiji kwa kijiji ili atatue kero? Hilo ni igizo kama maigizo mengine kaka.
 
Ni kawaida kwa nchi kama zetu mkuu wa nchi akipita lazima watu wasimame na wamshsngilie japo kinafiki kwani nani hajipendi? Tumetawaliwa na nidhamu ya woga hasa huko pembezoni. Siyo kweli kama watu wanayafurahia haya maisha magumu hapana mtu anayependa kuwa homless. Hata wakati wa apartheid South Africa Botha naye wali m treat vizuri kwa kuogopa usalama wao siyo kama walikuwa wanampenda

Sent using Jamii Forums mobile app

Cc: Phillipo Bukililo
 
Phillipo sina wasiwasi na uwezo wako katika kutetea unachoamini. Je ww, rais pamoja na wananchi mnaamini matatizo yanatatuliwa kwa kusimamisha msafara wa rais? Iwapo rais hatokaa apite kwenye eneo ulipo tatizo lako halitokaa litatuliwe? Sasa kama ni hivyo kwa nini rais asipite nchi nzima mtaa kwa mtaa na kijiji kwa kijiji ili atatue kero? Hilo ni igizo kama maigizo mengine kaka.
Hao wanawakilisha kilichomo ndani ya mioyo yao, wanawakilisha uzito wa matamanio yao ya kuona maisha yanabadilika na kuwa bora zaidi.

Kama wanachokiwaza kitakuja kuwa ni uhalisia au kitabakia kuwa ndoto, hilo ni suala jingine.

Huo umati ni changamoto kwa mkuu na wasaidizi wake, kwamba kinachotarajiwa kutoka kwao ni kikubwa.
 
Walijuaje hilo gari ndilo Raisi amepanda? Jamani tuwe Watu, raisi ni raisi hizi mbinu zote zilikuwa zinafaa zamani sana siyo enzi hizi!! Thank
 
Hamna aliyezuiliwa kufanya mikutano, hilo ni chaka tu la upinzani wanajifichia na vilaza kama wewe wanaona ni kweli, mikutano sio lazima ifanyike Dar, hizi ngonjera za kuzuiwa mikutano ni kwamba mbunge wa Hai, mbunge wa Arusha anataka afanyie mkutano dar, sio lazima!
Akafanye mkutano jimboni kwake na media zitakuwapo, ujumbe wake utafika kila kona!

Kwa katiba na Sheria gani inayosema hivyo mkuu!
 
Kwa staili hii ya kuvamia barabarani?? Ebu tutumiage akili hata kama haumkubali jpm!
Hapo sawa kasimaishwa na wananchi waliokuwa na taarifa ya ujio wake na wakahamasishwa wakajiandaa kwenda kujipanga barabarani kumsubiri huku wakiwa na maelekezo ya namna ya kuanza kumsimamisha kama inavyoonekana kwenye video ambapo wamesubiri hadi gari la tatu ambalo ndio alikuwemo Mtukufu ndio wakaanza kupiga kelele na kuashiria gari lisimame.

Kama hawakuwa na taarifa wasingejitokeza kwa wingi huo, ngojera tushazizoea hapo wenye PhD ya maganda ya korosho ndio wataamini hicho kitendo mnacholazima tuamini.
 
Wakati mzee Lowassa anapigiwa deki barabara ili aweze kupita, ile haikuwa ni sehemu ya maigizo.

Ila rais JPM anaposimamishwa njiani ni sehemu ya maigizo!!.

Kuna ugonjwa mbaya sana unaitwa mapenzi, ukiugua ugonjwa huo hauwezi kukitazama kitu na kukihukumu kwa haki.
 
Na kwa nini hayuko salama wakati anapendwa sana na watu wote?

Anapendwa sana na Watu wote hapo uongo kabisa umejuaje! Huku tu Facebook siyo wote wanampenda hiyo Watu wote inatoka wapi! Umejuaje pia anapendwa sana! Unajua jua halihitaji kampeni juu ya uwepo wake!!
 
Anachosema Msigwa ni kweli.Mnasimamishwa na traffic kwa zaidi ya Massa mawili akipota ati Rais alilakiwa na watu waliojipanga barabarani wakati watu wamesimamishwa muda mrefu tena kwa lazima.

Acheni mambo ya ujima,yalikuwepo enzi za JKN na yeye akayaona hawana.maana akayaacha.Duh umasikini wa akili ni hatari sana
Watanzania tumezoea kukalilishwa,kwa hy hy video hujaiona au? Kulazimishwa kuja barabarani wangesimama na akapita bila kuzuiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila hao wananchi waliweza usimamisha, mtake msitake hao wananchi sio wasanii, hawakuwa sehemu ya "stage act!!"
Kubalini tu hii sindano imewagusa kuliko maana sio alama nzuri 2025!

Kumbe lengo ni ndoto za 2025 nilidhani raisi anapanda dala dala then unasimamisha ovyo sana
 
Mimi sijali kama alisimamishwa au alisimama kwasalimia wananchi. Yeye ni rais anaweza kutumia utaratibu wowote kuzungumza na wananchi. Ndio maana haongei mwisho wa mwezi. Ni utaratibu wake. Sioni sababu ya watu kutoa povu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hawa wanaoshangaa hawana kazi kwao,nini cha kushangaza,mm hakuna mtu wa kunisababisha kuacha kazi na kumshangaa dunia hii,hata aje Obama,, ila kama napewa hela huko naenda,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anachosema Msigwa ni kweli.Mnasimamishwa na traffic kwa zaidi ya Massa mawili akipota ati Rais alilakiwa na watu waliojipanga barabarani wakati watu wamesimamishwa muda mrefu tena kwa lazima.

Acheni mambo ya ujima,yalikuwepo enzi za JKN na yeye akayaona hawana.maana akayaacha.Duh umasikini wa akili ni hatari sana
Wewe kichwani huna kitu
video huioni!!
 
Back
Top Bottom